Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kweli siasa hazina rafiki wa kudumu. Lakini acha watoane manundu, watasaidia kujenga upinzani wa kweli kama baadhi yao wataamua kuondoka CCM.

Wakati wakiandamwa na Magufuli, Samia alikuwa anashinda kutwa nzima na January akilewa na kuvuta sigara zake.

Samia alikuwa na hali ngumu mpaka akafanya aliyoyafanya na Makonda. Magufuli alijua kuwa kuwa January ndiye alikuwa mtunza siri mkubwa wa Samia na ndo sababu ya kumtoa kwenye baraza wakati huo.

Chuki anayoijenga dhidi ya January kwa kuogopa uchaguzi wa 2025 itamtengeneza Magufuli mwingine. Hakuna mtu yoyote ndani ya CCM aliyeamini kuwa Magufuli angekuwa rais 2015 mbali na mtandao wa Kikwete na Lowassa kutumia mabilioni kumuandama toka 2005.

Siasa ni kuvumilia hata wale usiokubaliana nao kama Mkapa alivyofanya kwa Kikwete na Kikwete akafanya kwa Magufuli. Ikitokea January akiupata urais siku moja, sina hakika watoto wa Samia wataendelea kuishi nchi ukizingatia wizi walioufanya.

Tujifunze namna Magufuli alivyomtendea Kikwete na watu wengine kutokana na hasira yake kwa waliomsulubu. Tusubiri, tuone.
Kitana mc
 
Mama anaupiga mwingi, bado mwigulu na yule Wa mambo ya Ndani. Akiwatoa hao Mama aje atuombe kura😂😂😂 alisikika mlevi mmoja
 
My Take
Cheo ni dhamana, maisha yaendelee 🙏🙏👇👇

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt, Moses Kasiluka, viongozi hao ni kama ifuatavyo;-

  1. Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anachukua nafasi ya Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  2. Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);
  3. Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Odisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  4. Balozi Mahmoud ThabitKombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy, anachukua nafasi ya Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  5. Mhe. Cosato Dvid Chumi (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiki. Mhe. Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi;
  6. Mhe. Deus Clement Sangu (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  7. Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Mhe. Londo anachukua nafasi ya Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  8. Bw. Eliakim Chacha Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huu Bw. Maswi alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA);
  9. Bi Mary Gasper Makondo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Makondo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Bi. Makondo anachukua nafasi ya Bi. Rehema Sefu ambaye amestaafu.
  10. Bw. Kiseo Yusuph Nzowa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Nzowa alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikuli;
  11. Bw. Musa Haji Ali ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Ali alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
  12. Bw. Louis Peter Bura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Bw. Bura anachukua nafasi ya Bw. Said Juma Nkumba ambaye amepangiwa majukumu mengine;
  13. Bi. Kemirembe Rose Lwota amehamishwa kutoka Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;
  14. Dkt. Vincent Biyegela Mashinji amehamishwa kutoka Wilaya ya Serengeti kuwa Mkuu wa Wilaya Manyoni;
  15. Dkt. Maulid Sleiman Madeni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti;
  16. Bw. Afraha Nassoro Hassan amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Seringeti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Bw. Hassan anachukua nafasi ya Bw. William Anyitike Mwakalambile ambaye uteuzi wake umetenguliwa na;
  17. Bw. Dennis Kwame Simba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Kabla ya uteuzi huu Bw. Simba alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Pia soma DOKEZO - Nape, Makamba kuondolewa Baraza la Mawaziri
Fyekeo linaendelea 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C9xPy1HNDLB/?igsh=MWVlY3NrcWxjd2h0MQ==
 
Mama wa kuupiga mwingi sasa naona kaamua mwaka huu..kama siyo kukosa ile penalty angepiga Hat trick Kabisa
IMG-20240723-WA0044(1).jpg
 
Ila Nape alinikera kwa ile kauli yake. Aliongea kwa dharau Sana.
 
Mama wa kuupiga mwingi sasa naona kaamua mwaka huu..kama siyo kukosa ile penalty angepiga Hat trick Kabisa
View attachment 3050258
Ila honestly kuna viongozi wanateuliwa lakini in reality hawana uwezo wa kuongoza na hata akili kichwani hawana au Wana akili za kawaida sana.
Binafs Nape uwezo wake wa kiakili ni wa kawaida sana
 
Mwigulu ndio watu waliomshika mama hawezi kumtoa
 
Mama apite pale kwa Mama Manka apige peps ya bariiiid ashushie na Pecon kidogo kidogo

Maka amejua kunifurahisha

Ingependeza Maharage na Januari wachunguzwe haraka sana wanatuhuma nyingi aana hawa!
 
Hawa vijana wa waasisi wa CCM walimdharau Rais baada ya kulewa madaraka. Kauli za Nape hazikuwa na busara.

View attachment 3048330

Naye Januari kupitia dada yake Mwamvita ndiye alikuwa anamlipa Mange Kimambi kwa yale matusi.View attachment 3048332

Hata hivyo Rais Samia ni mpole sana. Mungu ambariki
Duh! Huyu Nepi Hakuona aibu kuvua nguo nchi Namna hii na kuichafua Meza kuu
 
Lile jumba lioneni vilevile lina kila aina ya binadamu unaowajua wewe yani wanyambilisi sura mbaya moyo wa shetani na ndio wanaofiti kuwa pale. Angalia matukio yafuatayo:

Mbape mauye kabla hajatumbuliwa wanyambilisi walitumwa wamcheki yuko kwenye mudi gani high au low wakarudisha majibu yuko high ananyemka sebene wale wanyambilisi watabe wenye kazi zao wakasema hapahapa tunamkatia luku mara umeme ziiiiiiiii.

Matukio ya kinyambilisi ni mengi na mengine yanalenga kumtweza aliyejikweza na hivyo kumlia timing ya kinyambilisi mwengo wa kobe kumkata kichwa usicheze na lile jumba walio mule wote ni watu wenye roho mbaya wale wenyewewenyewe weusi warefu wembamba acha hawa tunaowaona kwenye tv kila siku wapo wenyewe wanyambilisi wanyambidenga hao wakipewa kazi na iwe kazi kweli hawakosei ng'oo achana na vile vipoyoyo vilivyomnyambilisi LISUTAL hii ardhi ya mchonga ione hivihivi.
 
Ila Nape alikera Sana. Kipindi sensitive Cha uchaguzi na kutokuaminiana unakuja kutoa kauli ya kijinga vile. Aende kabisa na asirudi Tena.
 
Back
Top Bottom