Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Alikosea sana, bangi aliyovuta ile siku asivute tena.

Kwa hili mama kafanya vizuri, wanaoleta mafarakano sio wa kuvumiliwa.
Usifurahie ukidhani ametupwa, CCM huogeshana na kuvishwa nguo mpya kisha hurejeshwa ukumbini kwa shangwe.
Majina mengi ya mwanzo kasoro Silaa ni warithi wa koo za watawala.
 
Safi Samia,naona mbwa alikuzoea sana,akataka muingie wote msikitini.
Watu wanauliza km kila kitu amefanya Mama Hawa Mawaziri na Wabunge wamefanya nini maana wote wakisimama ni kusemasema tu Mama kafanya Mama kafanya sawa Mama kafanya je! Wewe ukiwa km Mbunge au Waziri umefanya nini? Hakuna? PIGA Chini
 
Kuongea Vipi na Wapi mboni haikuvuma km hii ya Bwana Nape muasisi wa Bao la Mkono na kutolea maelezo jinsi gani linavyokua?
Watanzania tujifunze kutunza kumbukumbu, huyo unayemsifu ni yule aliyewahi kusema " kura wapigieni upande wa pili lakini mjue CCM ndiyo itakayounda serikali", hii haina tofauti na "bao la mkono", je, na yeye ajitengue?
 
Nani ninayemsifu na Wapi nilipomsifu?!
 
My Take
Cheo ni dhamana, maisha yaendelee 🙏🙏👇👇

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt, Moses Kasiluka, viongozi hao ni kama ifuatavyo;-

  1. Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anachukua nafasi ya Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  2. Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);
  3. Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Odisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  4. Balozi Mahmoud ThabitKombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy, anachukua nafasi ya Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  5. Mhe. Cosato Dvid Chumi (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiki. Mhe. Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi;
  6. Mhe. Deus Clement Sangu (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  7. Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Mhe. Londo anachukua nafasi ya Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  8. Bw. Eliakim Chacha Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huu Bw. Maswi alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA);
  9. Bi Mary Gasper Makondo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Makondo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Bi. Makondo anachukua nafasi ya Bi. Rehema Sefu ambaye amestaafu.
  10. Bw. Kiseo Yusuph Nzowa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Nzowa alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikuli;
  11. Bw. Musa Haji Ali ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Ali alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
  12. Bw. Louis Peter Bura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Bw. Bura anachukua nafasi ya Bw. Said Juma Nkumba ambaye amepangiwa majukumu mengine;
  13. Bi. Kemirembe Rose Lwota amehamishwa kutoka Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;
  14. Dkt. Vincent Biyegela Mashinji amehamishwa kutoka Wilaya ya Serengeti kuwa Mkuu wa Wilaya Manyoni;
  15. Dkt. Maulid Sleiman Madeni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti;
  16. Bw. Afraha Nassoro Hassan amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Seringeti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Bw. Hassan anachukua nafasi ya Bw. William Anyitike Mwakalambile ambaye uteuzi wake umetenguliwa na;
  17. Bw. Dennis Kwame Simba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Kabla ya uteuzi huu Bw. Simba alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Pia soma DOKEZO - Nape, Makamba kuondolewa Baraza la Mawaziri
Safi sana Mama anaupiga mwingi bado mmoja!
 
Mnawasingizia tu enzi za Magu mlisema Kigogo14 ni Zito na Makamba tena mmehamia kwa Mange??
Yale matusi alikuwa anaandika Junuari kisha anampa dada yake Mwamvita. Naye Mwamvita anayapeleka kwa Mange Kimambi.

Immediately Januari alipopata kazi ya kuwa Waziri wa Nishati, Mwamvita akaacha kazi Vodacom South na kuja hapa nchini. Yeye Mwamvita ndiye mmiliki wa kampuni ya Customer Care inayofanya kazi za TANESCO
 
Sasa kufanya kazi Tanesco kuna shisa gani kama ana deliver?
 
My Take
Cheo ni dhamana, maisha yaendelee 🙏🙏👇👇

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt, Moses Kasiluka, viongozi hao ni kama ifuatavyo;-

  1. Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anachukua nafasi ya Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  2. Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);
  3. Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Odisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  4. Balozi Mahmoud ThabitKombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy, anachukua nafasi ya Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  5. Mhe. Cosato Dvid Chumi (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiki. Mhe. Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi;
  6. Mhe. Deus Clement Sangu (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  7. Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Mhe. Londo anachukua nafasi ya Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  8. Bw. Eliakim Chacha Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huu Bw. Maswi alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA);
  9. Bi Mary Gasper Makondo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Makondo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Bi. Makondo anachukua nafasi ya Bi. Rehema Sefu ambaye amestaafu.
  10. Bw. Kiseo Yusuph Nzowa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Nzowa alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikuli;
  11. Bw. Musa Haji Ali ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Ali alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
  12. Bw. Louis Peter Bura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Bw. Bura anachukua nafasi ya Bw. Said Juma Nkumba ambaye amepangiwa majukumu mengine;
  13. Bi. Kemirembe Rose Lwota amehamishwa kutoka Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;
  14. Dkt. Vincent Biyegela Mashinji amehamishwa kutoka Wilaya ya Serengeti kuwa Mkuu wa Wilaya Manyoni;
  15. Dkt. Maulid Sleiman Madeni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti;
  16. Bw. Afraha Nassoro Hassan amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Seringeti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Bw. Hassan anachukua nafasi ya Bw. William Anyitike Mwakalambile ambaye uteuzi wake umetenguliwa na;
  17. Bw. Dennis Kwame Simba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Kabla ya uteuzi huu Bw. Simba alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Pia soma DOKEZO - Nape, Makamba kuondolewa Baraza la Mawaziri
Usiniambie; nadhani habari hii siyo kweli.

View: https://www.youtube.com/watch?v=l1eDuFoVrho
 
britanicca nakuaminia. Kuanzia leo hata ukiandika kuwa mende anatoa maziwa nitakuamini.

Uliandika wiki moja iliyopita kuwa mama akimaliza ziara ya Katavi Nape na Makamba wataondolewa. Na imetokea.

Kabla ya hapo ulitabiri uteuzi wa DGCI Mombo.
Britannica heshima kwake, nadhani yuko karibu na jiko maana anayaona yaliyomo kwenye chungu mapema sana
 
Back
Top Bottom