Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan siku ya leo amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali katika nyadhifa za serikali na bodi za kitaifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:

- Balozi Dkt. Habib Galsus Kambanga ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda.
- Dkt. Amina Suleiman Msengwa ameteuliwa kuwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Msengwa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Anachukua nafasi ya Dkt. Albina Chuwa ambaye amemaliza muda wake.
- Jaji Dkt. Ntemi Nimiwila Kilekamajenga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Masoko na Mitaji. Anachukua nafasi ya Jaji Dkt. Deo John Nangela, aliyechaguliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
- Prof. Aurelia Kamuzora ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa kwa kipindi cha pili.
- Bw. Abdulmajid Nsekela ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Chai Tanzania, akichukua nafasi ya Bw. Mustafa Hamis Umande ambaye amemaliza muda wake.
- Prof. Hozen Kahesi Mayaya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) kwa kipindi cha pili.