Uteuzi: Rais Samia amteua CEO wa CRDB Abdulmajid Nsekela kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chai, Habib Kambanga kuwa balozi wa Rwanda

Uteuzi: Rais Samia amteua CEO wa CRDB Abdulmajid Nsekela kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chai, Habib Kambanga kuwa balozi wa Rwanda

Wakuu,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan siku ya leo amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali katika nyadhifa za serikali na bodi za kitaifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:

  1. Balozi Dkt. Habib Galsus Kambanga ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda.
  2. Dkt. Amina Suleiman Msengwa ameteuliwa kuwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Msengwa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Anachukua nafasi ya Dkt. Albina Chuwa ambaye amemaliza muda wake.
  3. Jaji Dkt. Ntemi Nimiwila Kilekamajenga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Masoko na Mitaji. Anachukua nafasi ya Jaji Dkt. Deo John Nangela, aliyechaguliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
  4. Prof. Aurelia Kamuzora ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa kwa kipindi cha pili.
  5. Bw. Abdulmajid Nsekela ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Chai Tanzania, akichukua nafasi ya Bw. Mustafa Hamis Umande ambaye amemaliza muda wake.
  6. Prof. Hozen Kahesi Mayaya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) kwa kipindi cha pili.

View attachment 3235512
Mwenye nacho ataongezewa
 
Inaonekana Rwanda alileta jenerali Tanzania na sasa Tanzania imejibu mapigo kwa kumteua Deputy Director General TISS kuwa balozi wa Tanzania nchini Rwanda

TOKA MAKTABA :

Jenerali Patrick Nyamvumba Ameteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Tanzania​

iliyoandikwa na Jean de la Croix Tabaro

Februari 28, 202411:08 asubuhi

Screenshot-from-2024-02-28-11-04-16.jpg

Jenerali Patrick Nyamvumba
Kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Rais Paul Kagame jana usiku kilipendekeza Jenerali Patrick Nyamvumba kuwa balozi (Kamishna Mkuu) wa Rwanda nchini Tanzania.
Jenerali Nyamvumba atachukua nafasi kutoka kwa Fatou Harerimana ambaye alipendekezwa kuwa balozi (Kamishna Mkuu) mpya wa Jamhuri ya Rwanda nchini Pakistan
Ngoja tuone nakumbuka yule aliyekuwa DG wa TISS Alli Siwa aliwahi teuliwa kwenda huko huko Rwanda , Kagame alichelewa sana kuithibitisha ile hati yake ya uteuzi kutoka uteuzi 2014 akamthibitisha 2015.
 
Nimependa Kagame kupelekewa Deputy Director wa TISS kama Balozi kwaajili ya ku-monitor vihatarishi vya PK katika Ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kati na hasa Usalama wa Tanzania 👊
Anaweza kukataliwa boss wake Siwa alichukua mwaka kuthibitishwa hati ya uteuzi.
 
Nimependa Kagame kupelekewa Deputy Director wa TISS kama Balozi kwaajili ya ku-monitor vihatarishi vya PK katika Ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kati na hasa Usalama wa Tanzania 👊
Umeona cv pale mzuri pia kwenye maswala ya ugaidi na kule msumbiji wale waliosumbua kibiti wametulizwa na Kagame
 
Umeona cv pale mzuri pia kwenye maswala ya ugaidi na kule msumbiji wale waliosumbua kibiti wametulizwa na Kagame
Jamaa ni mzuri kwenye ujasusi pamoja na hayo mambo ya ugaidi.

Kwahiyo huenda akasaidia kumtuliza PK
 
Huyu maza ni mdini sn, kateua karibu wote watu wa Ijumaa
UPUMBAVU MTUPU!
Watu wenye tabia za kiyahudi hata mpewe nini hamuwezi kuridhika!.
Hebu weka list ya wakuu wa mikoa , wakuu wa wilaya na Baraza Zima la mawaziri ili tuone wa ijumaa wangapi na wajumapili wangapi ?!
Naamini kwa sehemu hizo tatu tu itatosha kutuonyesha ni dini ipi ina watu wengi serikalini!.
Huko kwa makatibu wakuu na makatibu tawala tusifike !
Wagalatia kuweni na haya basi!
Mimi ni mfuatiliaji sana wa watu wanaoteuliwa na waliowahi kuteuliwa hata kabla sijazaliwa!.
Nilichokigundua ni kwamba tangu serikali ya Nyerere, Mwinyi, mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa hii ya Samia,
NAFASI ZA WAISLAMU HAZIJAWAHI KUWA NYINGI KUSHINDA NAFASI ZA WAVAA MISALABA SERIKALINI.!.
Awamu zote sita waislamu hawajawahi kufika hata 35% ya watumishi wa umma.
Lakini ni bahati mbaya ilioje kwamba kila raisi muislamu akimteua mtumishi muislamu kushika nafasi fulani lazima atokee mbwa fulani abweke eti RAIS KAFANYA UDINI bila kuangalia WAVAA MISALABA WALIOPO SERIKALINI NI ASILIMIA NGAPI UKILINGANISHA NA WAISLAMU ?!.
 
Ngoja tuone nakumbuka yule aliyekuwa DG wa TISS Alli Siwa aliwahi teuliwa kwenda huko huko Rwanda , Kagame alichelewa sana kuithibitisha ile hati yake ya uteuzi kutoka uteuzi 2014 akamthibitisha 2015.
Na IGP mangu naye si alipelekwa Rwanda na magu
 
Atasaidia kuwatuliza magaidi........kwa PK ngoma sio nyepesi hivyo
Ni kweli usemacho Mkuu, ila itafanya PK apunguze baadhi ya mawaa yake akishajua uzito wa mtu aliyeenda kwake
 
Back
Top Bottom