Tatizo la ajira linahusishwa katika uteuzi kwann? Mtu anaandika vijana hawatapata ajira........
Hata Mabeyo kuna siku aliingia jeshini kama kijana aliyepata ajira mpya.
Mabeyo alipotoka ameshika Mkunda, naye aliingia hapo bila kuwa na cheo chochote, kazi yoyote na bila uzoefu wowote na leo kaachiwa nafasi.
Sasa hiyo nafasi alitakiwa apewe graduate au nini kilitakiwa ili kusiwe na malalamiko ya ajira? Huwezi kumpa mtu asiye na uzoefu na haaminiki nafasi nyeti. HAIWEZEKANI. Yaani kijana umetoka chuo cha misitu huko puuu wewe ni mkurugenzi mpya bodi ya utalii?
Kuna siku Mabeyo atampisha mwingine hiyo nafasi mpya aliyopewa, na huyo mwingine huenda sasa hivi anapata uzoefu wa kazi sehemu fulani baada ya kuajiriwa huko nyuma akiwa fresh bila uzoefu.
Kila wakati kuna vijana wapya wanaingia jeshini. Hao ni Macdf wajao, wakuu wa vikosi wajao na kuna siku watapewa nafasi za ukurugenzi, ubalozi n.k
HAKUNA UHUSIANO WA UKOSEFU WA AJIRA NA NAFASI ZA UTEUZI SABABU KILA CHEO KIPYA NI FURSA MPYA KWA MWINGINE KUPATA NAFASI ILIYOACHWA NA ALIYEPEWA CHEO KIPYA.