Uteuzi: Rais Samia ateua Mabalozi pamoja na kuvunja Bodi ya TCRA

Uteuzi: Rais Samia ateua Mabalozi pamoja na kuvunja Bodi ya TCRA

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi na kuvunja bodi kama ifuatavyo:

1. Amemteua Balozi James Gilawa Bwana kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika kusini. Balozi Bwana anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi ambaye amestaafu.

2. Amemteua Balozi Said Hussein Massoro kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait. Balozi Massoro anachukua nafasi ya Balozi Said Shaib Mussa ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

3. Amemteua Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC). Kabla ya uteuzi huu Bw. Mkeyenge alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC). Bw. Mkeyenge anachukua nafasi ya Dkt. Elirehema Doriye ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

4. Amevunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia tarehe 07 Novemba, 2023.

Zuhura Yunus

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

20231109_005605.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi na kuvunja bodi kama ifuatavyo:

Amemteua Balozi James Gilawa Bwana kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika kusini. Balozi Bwana anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi ambaye amestaafu.

Amemteua Balozi Said Hussein Massoro kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait. Balozi Massoro anachukua nafasi ya Balozi Said Shaib Mussa ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Amemteua Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC). Kabla ya uteuzi huu Bw. Mkeyenge alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC). Bw. Mkeyenge anachukua nafasi ya Dkt. Elirehema Doriye ambaye atapangiwa kazi nyingine. Uteuzi huu unaanza mara moja.

Amevunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia tarehe 07 Novemba, 2023.


1699481088407.png
 
Nani tena? Balozi Said Hussein Massoro aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa halafu akatenguliwa mwezi August 2023, sasa mwezi November 2023 ateuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait.

Balozi Said Hussein Massoro kabla ya uteuzi wa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa mapema mwaka huu January 2023, alipata kuhudumu kama Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa kisha mwezi January 2023 kupandishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa. Miaka ya nyuma aliwahi pia kuwa Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania Beijing China

2019
16 May 2019
Beijing, China
 
WanaJF walipata kuuliza swali hili lakini hatukupata majibu ya kuridhisha au ufafanuzi tukapata uelewa. Je Mawakili wasomi na wanasheria nguli mnasemaje :

 
DR MAMBO AMP aliuliza swali hili hapa JF :
Jana katika pita pita zangu nilikutana na Taarifa kutoka ikulu ikisema kuwa Rais amemteua Bw Hussein Massoro Kuwa balozi na kumuweka Balozi Ali Idi Siwa kuwa DG mpya TISS. (kongole kwake).

Japo jambo hilo lilizua mijadala mingi ikiwemo uwepo wa Tengua tengua Ya Wakurugenzi wa TISS kwa kipindi kifupi cha miaka mitano Ambapo mpaka sasa Wakurugenzi wapatao 3 tayari wamekwisha badilishwa, Na wengi wakahoji kuhusu Usalama wa Taarifa za kiulinzi za nchi na Kusema Huko TISS kuna siri gani Inayofanya kubadilishwa kwa Wakurugenzi mara kwa mara?.

Lakini Hilo sio swala kubwa Sana,kubwa ni kwamba Mama kwa kumteua Rt.DG kuwa Balozi, amepingana na sheria Ya usalama wa Taifa iliyopitishwa na Bunge mwaka July,2023 kifungu cha 6(6) Ambayo inatoa marufuku kwa Mkurugenzi wa TISS kuchaguliwa kushika nyadhifa yoyote ya kiutumishi katika sector yoyote ya Umma au nyadhifa yoyote ya kisiasa.

Au ilipotungwa sheria hiyo ilikuwa Tamu sehemu ya mamlaka ya TISS ila sehemu ya upande wa utawala haikuonekana
 
Back
Top Bottom