Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Makobaz watupu.Ilikuwaje hii bodi ikawa na watu ambao wote wana mrengo mmoja wa dini? Yaani wooote ni dini moja?
View attachment 2808312
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Makobaz watupu.Ilikuwaje hii bodi ikawa na watu ambao wote wana mrengo mmoja wa dini? Yaani wooote ni dini moja?
View attachment 2808312
Brother GENTAMYCINE umetisha sana kwenye ule utabiri wako wa simba kufungwa. Niliahidi kukuogopa natekeleza ahadi yangu. Heshima yako tenaNaona aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Usalama wa Taifa ( DGIS ) Massoro kamtupa mbali Kuwait ili asiwe anayajua tena TISS na asiwe anaendelea kupiga Majungu na aliowaacha Idarani huku akiwa na Usununu ( Hasira ) ya Kutenguliwa na kupewa Balozi Siwa iliyokuwa nafasi yake.
Kama migodini kuna shift sembuse haoUsiku wa manane, teuzi zinafanywa na bodi kuvunjwa,
Tiss hawalali 😂
Dada Sharifa Ikulu, AiseeeTaaifa hii imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais - IKULU Nov 9, 2023
View attachment 2808307
Na uzuri Salio lipo sio kama kijana anayeambiwa akajiajiri huku katoka chuo🤣😂🤣doriye katumbuliwa
Hatahivyo kashakula vya kutosha
Akajiajiri sasa
Waweke utaratibu kwamba kila baada ya miaka kadhaa bodi ziwe zinavunjwa, tupate uzoefu wa wengineBodi ya TCRA iliyovunjwa imeshiba CV , tatizo gani limewakumba hawa wasomi :
Mhandisi Othman Sharif Khatib
Mwenyekiti wa Bodi
Mhandisi Othman Sharif Khatib ni Mtaalamu na Mhandisi wa Mawasiliano ya Simu mwenye uzoefu wa miaka mingi kwenye sekta ya mawasiliano na amekuwa kwenye utumishi wa umma katika nafasi mbalimbali ndani ya Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na taasisi zake. Aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA)(TCRA) Septemba 2022.
Mhandisi Khatib ana shahada ya Uzamivu ya Sayansi katika Uhandisi wa Mawasiliano ya Simu kutoka Chuo Kikuu cha Hochschule für Vehrkehrswessen cha Dresden, Ujerumani. Amepata mafunzo mbalimbali ya mawasiliano ya simu, uongozi na usimamizi wa sekta ya mawasiliano kwenye vyuo mbalimbali vya kimataifa.
Bw. Khalfan S. Saleh
Makamu Mwenyekiti
Bw. Khalfan S. Saleh ni Mtumishi wa Serikali katika Ofisi ya Rais. Ana Shahada ya Uzamili katika fani ya Mitandao ya Mawasiliano ya Kielekroniki (MSc Data Telecommunication Networks) kutoka Chuo Kikuu cha Salford, Uingereza. Amekuwa Serikalini kwa zaidi ya miaka 25 ambapo amepata fursa ya kufanyakazi katika Serikali zote mbili, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT). Nafasi alizowahi kushika ni pamoja na Balozi Mdogo katika Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar na Mpigachapa Mkuu wa Serikali na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.
Dkt. Mzee Suleiman Mndewa
Mjumbe wa Bodi
Dkt. Mndewa ana shahada ya Uzamivu (Ph.D.) katika Optoelectronic Information Engineering ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Tekinolojia cha Huazhong, Wuhan – China; Shahada ya Uzamili ya Information Technology ya Chuo Kikuu cha Griffiths, Queensland, Australia; Shahada ya Kwanza ya Science in Electronics ya Chuo Kikuu cha Osmania Hyderabad cha India na Cheti cha Full Technicians cha Uhandisi wa Umeme cha Chuo cha Ufundi Karume, Zanzibar.
Kwa sasa ni Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Miundombinu, Mawasiliano na Usafirishaji, Zanzibar. Ni mjumbe wa timu ya wataalamu wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB kuanzia mwaka 2004. Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni pamoja na Mkurugenzi wa Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Chuo Kikuu cha Dodoma; Mshauri wa masuala ya TEHAMA kwenye Serikali ya Tanzania na mjumbe na msimamizi wa timu ya wataalamu kuhusu mtandao na miundombinu kwa ajili ya mradi wa serikali mtandao (e-government), Zanzibar
Dkt. Fatuma Simba Ikuja
Mjumbe wa Bodi
Dkt. Fatuma Simba Ikuja ni Mhadhiri na Mtafiti katika Idara ya Sayansi ya Kompyuta na Uhandisi, Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CoICT), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Akiwa na uzoefu na utaalamu mkubwa, Ikuja hushiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali na majukumu ya ushauri katika uga wake. Maeneo yake ya utafiti yanajumuisha mitandao ya mawasiliano ya kasi, Elimu kwa njia ya Mtandao, usalama wa mtandao na uhandisi wa programu za TEHAMA. Dkt. Ikuja pia huwafundisha wanafunzi wa shahada ya uzamili katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha (NM-AIST) kama kazi ya muda wa ziada, pia, anafundisha kozi za shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Dkt. Ikuja amesimamia wanafunzi mbalimbali wa shahada za uzamili na uzamivu katika safari zao za kitaaluma. Amehudumu kama mtahini wa ndani na nje kwa maandiko ya wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu katika UDSM na NM-AIST. Aidha, Dkt. Ikuja ni mjumbe wa Bodi ya Wahariri wa Jarida la Tanzania la Uhandisi na Teknolojia (TJET), Tanzania Journal of Engineering and Technology. Utaalamu wake pia unatambuliwa kupitia jukumu lake kama mchambuzi wa maandiko ya kitaalamu yakiwemo ya mikutano ya IEEE Africon (2015, 2021) na IFIP WG 9.4.
Mwezi Novemba 2021, Dkt. Ikuja aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Elimu Mtandao (CVL) cha UDSM, ambacho kinawezesha utoaji elimu kwa njia ya mtandao unaowezeshwa na TEHAMA. Pia alifanya kazi kama Mtaalamu wa Ushirikiano wa kisekta katika UDSM akihudumu kwa miaka mitano (2016-2021) katika mradi wa Higher Education for Economic Transformation (HEET) uliofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Zaidi ya kujihusisha na masuala ya taaluma, Dkt. Ikuja anapendelea ubunifu na ujasiriamali. Anashiriki kikamilifu kama Mwalimu Mwelekezi katika Kituo cha Kuboresha na Kukuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDICTI), ambacho kinahusika kukuza na kuunga mkono bunifu za wanafunzi na wahitimu wa chuo kikuu kuwawezesha kubadilisha mawazo yao kuwa biashara zinazochipukia. Zaidi ya hayo, Dkt. Ikuja anatoa mchango wake kikamilifu katika programu ya "SmartGirlz in ICT", inayoelimisha na kuwezesha wasichana wa shule za sekondari kujifunza masomo na kazi katika fani inayokua ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Programu hii inapata hamasa kutoka mradi wa "Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA" unaoratibiwa na Shirika la Mawasiliano la Kimataifa (ITU) lililoko Geneva.
Bw. Abdallah Batenga Katunzi
Mjumbe wa Bodi
Abdallah Katunzi anafundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam — Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma Tanzania. Ana Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Shahada ya Uzamili ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda. Kwa sasa, anasomea Shahada ya Uzamivu ya Habari na Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya.
Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 19 kama mwandishi wa habari, mwanataaluma, mtafiti na mshauri katika masuala ya Habari na Mawasiliano. Ameandika machapisho kadhaa, na ripoti yake ya utafiti ya hivi karibuni aliyoichapisha kwa ushirikiano na mtafiti mwingine iitwayo “The State of Journalism Reporting in Tanzania” ilitolewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwezi Desemba 2022.
Amekuwa mshauri mwelekezi wa masuala yanayohusu vyombo vya habari na mawasiliano akifanya kazi na mashirika ya kimataifa, yakiwemo UNESCO (Tanzania), Swiss Development Cooperation (SDC) Tanzania, africaemediterraneo lenye makao yake nchini Italia, Natural Resources Governance Institute (NRGI), Florida International Research IWASH Initiative Limited (Marekani), DW Akademie (Ujerumani), GIZ (Tanzania), Friedrich Ebert Stiftung (FES-Tanzania), Geneva Centre for Security Sector Governance (DCAF), Norwegian Church Aid (NCA), na African Centre for Media Excellence (ACME) ya Uganda.
Amekuwa mshauri mwelekezi kwa taasisi za Serikali zikiwemo Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET). Pia, amefanya kazi na mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na Baraza la Habari Tanzania, Tanzania Media Foundation (TMF), na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA).
Kwa sasa anasimamia mradi wa utafiti wa vyombo vya habari nchini unaojulikana kama “Mradi wa Ubora wa Maudhui ya vyombo vya Habari Tanzania” (University of Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (UDSM-SJMC) – Yearbook on Media Quality in Tanzania ), mradi huu unachunguza ubora wa uripoti wa vyombo vya habari kila mwaka nchini. Mwezi Mei 2023, alitunukiwa tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye kipengele cha tafiti zilizofikia wadau wengi (outreach research project) kwenye maonyesho ya nane ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwaka 2022 alikuwa Mratibu wa Kitaifa wa Siku ya Redio ya Umoja wa Mataifa nchini iliyoadhimishwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Bi. Rehema Jessica Khalid
Mjumbe wa Bodi
Rehema Jessica Khalid ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania mwenye Shahada ya Uzamili ya Sheria, iliyojikita katika Sheria za Kampuni. Ana Shahada ya Kwanza ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Bangalore, India. Kwa sasa ni Katibu na Mwanasheria Mkuu wa Mkulazi Holding Company Limited (MHCL).
Nafasi nyingine alizowahi kushika ni pamoja na Mshirika kwenye Kampuni ya Wanasheria ya Precise Law Attorneys kuanzia Agosti 2018 hadi Juni 2019, Mkuu wa Idara inayosimamia majukumu ya kampuni na masuala ya kisheria ya Zantel kati ya Juni 2014 na Julai 2018, Mwanasheria Mwandamizi wa Mkono and Company Advocates kati ya Januari 2007 na Juni 2014.
Rehema Jessica Khalid ni mjumbe wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Taasisi ya Wakurugenzi (IoDT) Tanzania na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
Source : https://www.tcra.go.tz/administration/board-members
Ilikuwaje hii bodi ikawa na watu ambao wote wana mrengo mmoja wa dini? Yaani wooote ni dini moja?
View attachment 2808312
Mbaya zaidi wote ni wazanzibar, tukisema maza ni mdini sn muwe mnatuelewa.Ilikuwaje hii bodi ikawa na watu ambao wote wana mrengo mmoja wa dini? Yaani wooote ni dini moja?
View attachment 2808312
Bodi zote huwa ni miaka 2.5Waweke utaratibu kwamba kila baada ya miaka kadhaa bodi ziwe zinavunjwa, tupate uzoefu wa wengine
Aisee!Ilikuwaje hii bodi ikawa na watu ambao wote wana mrengo mmoja wa dini? Yaani wooote ni dini moja?
View attachment 2808312
Maza kwake Katiba na sheria siyo kituDR MAMBO AMP aliuliza swali hili hapa JF :
Jana katika pita pita zangu nilikutana na Taarifa kutoka ikulu ikisema kuwa Rais amemteua Bw Hussein Massoro Kuwa balozi na kumuweka Balozi Ali Idi Siwa kuwa DG mpya TISS. (kongole kwake).
Japo jambo hilo lilizua mijadala mingi ikiwemo uwepo wa Tengua tengua Ya Wakurugenzi wa TISS kwa kipindi kifupi cha miaka mitano Ambapo mpaka sasa Wakurugenzi wapatao 3 tayari wamekwisha badilishwa, Na wengi wakahoji kuhusu Usalama wa Taarifa za kiulinzi za nchi na Kusema Huko TISS kuna siri gani Inayofanya kubadilishwa kwa Wakurugenzi mara kwa mara?.
Lakini Hilo sio swala kubwa Sana,kubwa ni kwamba Mama kwa kumteua Rt.DG kuwa Balozi, amepingana na sheria Ya usalama wa Taifa iliyopitishwa na Bunge mwaka July,2023 kifungu cha 6(6) Ambayo inatoa marufuku kwa Mkurugenzi wa TISS kuchaguliwa kushika nyadhifa yoyote ya kiutumishi katika sector yoyote ya Umma au nyadhifa yoyote ya kisiasa.
Au ilipotungwa sheria hiyo ilikuwa Tamu sehemu ya mamlaka ya TISS ila sehemu ya upande wa utawala haikuonekana
Punguza ujingaKuna uwezekano Kwa sasa kuwa ile dini, CCM na Serikali ni kitu kimoja.
Kujinusuru hapo kunahitajika akili na mbinu Za ziada 2025.
H ha ha ha aaaaaaaaLabda wameamua kwenda kusaidia Gaza. Tuweni positive, sio kila kitu negative.
Kudumisha.Ilikuwaje hii bodi ikawa na watu ambao wote wana mrengo mmoja wa dini? Yaani wooote ni dini moja?
View attachment 2808312
Ondoa mabangi yako huku .nenda kaandamane kama ulivyoahidi nasiyo kuja kujificha huku tapeli mkubwa wewe 😄😄😄Mbaya zaidi wote ni wazanzibar, tukisema maza ni mdini sn muwe mnatuelewa.