Uteuzi: Rais Samia Ateua Viongozi Wapya ATCL na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Uteuzi: Rais Samia Ateua Viongozi Wapya ATCL na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko muhimu katika uongozi wa taasisi mbili nchini kwa kuteua viongozi wapya.

Taarifa kutoka Ikulu iliyotolewa tarehe 11 Novemba 2024 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, inaeleza uteuzi huo uliaanza rasmi tarehe 9 Novemba 2024.

photo_2024-11-11_21-08-27.jpg

Profesa Harun Jeremia Mapesa ameteuliwa kuwa akichukua nafasi ya Profesa Shadrack Mwakalila ambaye amemaliza muda wake. Kabla ya uteuzi huu, Prof. Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, akiweka rekodi nzuri ya utaalamu na uzoefu katika elimu ya juu.

Soma Pia: Uteuzi: Dkt. Leonard Akwilapo ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)

Aidha, Mhandisi Peter Rudolf Ulanga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), akichukua nafasi ya Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amestaafu.
 
Na huyo Bi sharifa Nyanga uteuzi wake wa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ulifanyika kimyakimya nini.
Hongera kwa kujaza nafasi iliyoacha na zuhura yunus
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko muhimu katika uongozi wa taasisi mbili nchini kwa kuteua viongozi wapya.

Taarifa kutoka Ikulu iliyotolewa tarehe 11 Novemba 2024 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, inaeleza uteuzi huo uliaanza rasmi tarehe 9 Novemba 2024.

Profesa Harun Jeremia Mapesa ameteuliwa kuwa akichukua nafasi ya Profesa Shadrack Mwakalila ambaye amemaliza muda wake. Kabla ya uteuzi huu, Prof. Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, akiweka rekodi nzuri ya utaalamu na uzoefu katika elimu ya juu.

Soma Pia: Uteuzi: Dkt. Leonard Akwilapo ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)

Aidha, Mhandisi Peter Rudolf Ulanga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), akichukua nafasi ya Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amestaafu.
Hongera kwao kwa uteuzi wa kulitumikia Taifa kazi iendelee.
 
K
Hata kama ni connection wangemtangaza kama anavyotangaza teuzi nyingine.
Ila nimeona kuna teuzi za watoto wa wakubwa hazitangazwi sijui ni kwa sababu ya kuona aibu
Kama Nani kateuliwa kimya kimya
 
K

Kama Nani kateuliwa kimya kimya
Zahara Muhidin Michuzi.
Rose Robert Manumba.
Nitafutie pdf inayoonyesha walivyopangiwa hivyo vituo vyao vya kazi walipo sasa.
Hawa watoto wa wakubwa wapo kwenye nafasi walizopo kiupendeleo kabisa hawana sifa wala uzoefu unaotakiwa kwa kazi hizo.
Na pia utendaji wao ni wa hovyo
 
Rais Samia yupo na anapiga kazi. Mlitaka atokee kwenye TV ndyo mwamini?
 
Udini umetawala sana awamu hii
Unaacha kujadili hoja za msingi unakimbilia udini? Unachokifanya hapo no kuuprote udini wenyewe bila kujua jambo ambalo ni hatar sana kwa mustakabal wa taifa letu. Hata ID yako inajieleza. Nawachukia sana watu wanaojenga hoja zao kwa kivuli cha dini xa wakoloni.
Aibu kwako na hutafanikiwa kuwagawa watu kwa ujinga wako wa kujidai mdini sana
 
Back
Top Bottom