UTEUZI: Rais Samia Suluhu amteua Balozi Hussein A. Kattanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Bashiru Ali ateuliwa kuwa Mbunge

UTEUZI: Rais Samia Suluhu amteua Balozi Hussein A. Kattanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Bashiru Ali ateuliwa kuwa Mbunge

Kongole kwako Dkt.Bashiru Ally kwa uteuzi wa Ubunge hakika hapo ulipo sasa ni swala la muda tu pengine tusishangae kusikia ukiteuliwa nafasi ya uwaziri , usidhohofike kutoka nafasi ya KMK hadi M.P.....
Bora hata apewe uwaziri kuliko kumwacha pale alipokuwa. Ilikuwa hatari.
Hongera zake hata hivyo, hajarudi mikono mitupu.
 
Kama kweli amemuacha Bashiru Ali kwa sababu ya zile tuhuma atakuwa amekosea sana.

Tuhuma zile kama zina ukweli Bashiru hakustahili uteuzi wa aina yoyote.
 
Pongezi nyingi kwa katibu Mkuu Mpya mhe. Hussein Katanga hakika unastahili kwa nafasi hiyo.

1. ni mzoefu ktk mambo ya uongozi.

2. mbunifu na mtu mwenye malengo na maono/ visionary leader.

3.mchapa kazi
Hakika Mhe. Rais hajakosea hata kidogo.

kwa mwendo huu wa Mh. Rais ni wazi kabisa serikali yake itaenda barabara bila kikwwazo.
 
Kama kweli amemuacha Bashiru Ali kwa sababu ya zile tuhuma atakuwa amekosea sana.
Tuhuma zile kama zina ukweli Bashiru hakustahili uteuzi wa aina yoyote.
Kwa nafasi aliyokuwa nayo huwezi ukamtoa halafu umrudishe nyumbani acheze na watoto,ni bora bungeni akatengeneza hoja kwa serikali
 
Hii nchi ili itawalike kwa uzuri ni sharti katiba ifanyiwe marekebisho. Rais ana mamlaka ya kufanya ajuavyo yeye na si kufuata sheria
Sasa huyu Samia ndiye tumuidhinishe atawale milele sio yule waliyekuwa wanamtaka!
 
Naona uteuzi wa leo umebalance kwa zile team mbili zilizokuwa zinavutana kimyakimya.
Japo Gang limepigwa vibaya kwa kumwondoa Kakiru pale ikulu.
 
Kwa nafasi aliyokuwa nayo huwezi ukamtoa halafu umrudishe nyumbani acheze na watoto,ni bora bungeni akatengeneza hoja kwa serikali
Basi wangempa hata ubalozi ili akae mbali na Ikulu.
Yaani amefanya kazi Ikulu mwezi mmoja tu!!!
 
kweli haya maisha ni mzuungouko,

tuishi kwa kupendane, chuki na fitina havifai, hujui huyo unaye mfanyia fitina kesho atakuwa nani, hakika Mungu ndiiye ajuaye.
Mungu Mbariki Katibu Mkuu mpya Mhe. Hussein Katanga.

Karibu baba tuendeleze kurudumu la taifa.
 
Hii ya leo sijapata tetesi zake au ndo mama kaanza kuziba zisileak
 
Back
Top Bottom