UTEUZI: Rais Samia Suluhu amteua Balozi Hussein A. Kattanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Bashiru Ali ateuliwa kuwa Mbunge

UTEUZI: Rais Samia Suluhu amteua Balozi Hussein A. Kattanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Bashiru Ali ateuliwa kuwa Mbunge

Sahauni hii ni vita mama tiali anautazama uraisi si kwa awamu moja bali kwa awamu mbili ndio maana anajaribu kupangua watu wa makundi ambayo katika safari yake ya kisiasa yanaweza kumkwamisha

Tazama nafasi kama TAMISEMI kuwa ummi
Huyu mama ni strategy ya mama mkuu kustabalize mikoani hadi wilayani kwa kutengeneza mtandao wake
Nafasi ya katibu kiongozi ni strategy ya mama
Hapa tunaona kuwa bashiru kateuliwa kuwa Mbunge lakini hii ni danganya toto mama anatumia akili na hesabu kubwa hapa bashiri katumbuliwa kwa ganzi ili maumivu sisi tusiyaone lakini kitendo cha bashiru kupelekwa bungeni ni sawa ametupwa kwa sasa hana ushawishi tena kwenye serikali na kwenye chama.

Tusubili mama atakapo teuliwa kuwa mwenyeketi hapo hutaona mazishi ya Bashiru na polepole kisiasa ndio kwa heli.

Sent from my SM-J400F using JamiiForums mobile app
Nimekuelewa mkuu[emoji122][emoji122]
 
Mama sio strong enough ku-deal na hawa watu.Huyu alipaswa kuachwa kam alivyo tu na si kupewa ubunge.

Msishangae akampa uwaziri.

Huyu mama sijui kama ataweza kulipiga chini lile kundi la SUKUMA GANG.
Bado wanacontrol wizara zile - Nishati na Madini
 
Hapa nampongeza Mama Samia,Niliwahi kuwaza kwamba Marehemu alitumia emotion kumteua Bashiru kuwa katibu mkuu, yaani alipewa ubalozi kwa ajili ya cheo. Ukiacha tuu kwamba ni hatari kumuweka Mhaya Ikulu, bado tuu alikuwa hajafikia vigezo vya kawaida kabisa. Sababu yule ni academician mkuu.

Nawapongeza wote kwa kupata nafasi mpya
Mkuu kwa nini unatutusi, kwani sisi sio wa tz,?acha ubaguzi bwana
 
Kifupi Bashiru Ali katolewa kwenye Chama na Magufuli aachie chama wengine wenyewe wenye chama Na Raisi Samia kamtupa nje ya serikalu aende huko bungeni . now Case closed.Thanks Mama Samia

Watanzania tuko fit
 
Mkuu kwa nini unatutusi, kwani sisi sio wa tz,?acha ubaguzi bwana
Hapana Mkuu, ninyi ni watu wazuri sana waungwana mno sema yale mambo ya mpe mruke mpe mruke ndiyo ninayochukia.Ila sina tatizo kabisa na Wahaya
 
Ila siasa zinahitaji uvumilivu sana.Yaani kazi yake imeishia kuandaa kiapo cha makamu wa raisi na kutupwa nje kabisa ya mfumo.Maana kuna watu aliwapiga biti sana ndani ya serikali akiwa katibu mkuu.
 
Mkuu Katiba inatakiwa ibadirishwe yote siyo marekebisho..
Unaweza kumzomea mgombea urais wa chama furani kwenye kampeni, siku akishinda anakutafuta alikulipizie.
Utakula makonzi mpaka kichwa kichakae
Uko sahihi mkuu katiba hii ni mbovu sana
 
Watanzania usiwaone kimya sio wajinga kama nchi nyingi za jirani na nje wanavyotuona ukiona kobe kainama sio kalala au mjinga anatunga sheria au anawaza namna gani akutandike!
 
Mnisaidie tutaendelea kumuita Balozi Bashiru Ally au tutamuita mheshimiwa Bashiru Ally.
 
Kutoka Katibu Mkuu wa CCM, Katibu Mkuu Kiongozi hadi mbunge wa kuteuliwa hii inaitwa from GLORY to ASHES!
Wenzio wanaangali mpunga wewe unaangalia jina la cheo!

Tena hapo alipo ni mwendo wa mpunga hadi 2025
 
Bashiru mwezi wa 2 alikuwa anaishi nyumba ya Katibu mkuu CCM ya chama, mwezi wa 3 akahamia nyumba ya Katibu mkuu kiongozi na leo anahamia nyumbani kwake Msewe barabara ya chuo kikuu😂😂😂 Hakika huu ni utalii wa ndani.
 
Kitendo cha kutengua uteuzi au nafasi ya Bashiru Ali Kakurwa kutoka nafasi ya Katibu Mkuu kiongozi hadi kuwa mbunge ni kitendo cha kuonyesha kujali na kuheshimu utawala wa kisheria.

Nafasi ya Katibu Mkuu kiongozi haipaswi kukaliwa na mwanasiasa kama alivyo Bashiru Kakurwa.
Duh.....Yaani jamaa amedumu wiki 3 tu kwene nafasi hii ya KMK..!!!!!
Something big is being cooking!!! Kuna 2 things hapa:
  1. Yawezekana Bushiri Ali anatupwa Japan...!!
  2. Reshuffle ya Baraza la Mawaziri inanukia na huyu Bushiri akapachikwa kwenye Uwaziri au PM....???
Let's wait and see.......!!?
 
Back
Top Bottom