UTEUZI: Rais wa Zanzibar amemteua Jaji George Joseph kazi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi

UTEUZI: Rais wa Zanzibar amemteua Jaji George Joseph kazi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi

Jaji George Joseph Kazi ameteuliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ataapishwa tarehe 28 Agosti, 2023 saa 8 Mchana Ikulu Zanzibar na wajumbe wa Tume hiyo. Uteuzi wake unaanza leo 24 Agosti, 2023.

Pia ameteua wajumbe mbalimbali wa tume hiyo; Jaji Aziza Iddi Suwedi, Ndugu Idrisa Haji Jecha, Ndugu Juma Haji Ussi, Ndugu Halima Mohamed Said, Ndugu Ayoub Bakar Hamad na Ndugu Awadh Ali Said.

Yaani watu wote mliocomment mmebase kwenye dini ila hamjaona kuwa timu mwenyeji kachagua referee wa mchezo Mwenyewe, bado tuna safari ndefu ya kwenda.
 
Ahueni na minority nao wamekumbukwa katika nafasi za juu serikalini. Maana haiwezekani serikali yote imejaa watu wa imani moja pekee.

Muhimu tu katika maisha yake yote ya kuitumikia hiyo nafasi, kamwe asijaribu kuiga nyendo za Jecha Salim Jecha.
Nafikiri huyo ni TX toka Jamhuri ya Tanganyika
 
Ahueni na minority nao wamekumbukwa katika nafasi za juu serikalini. Maana haiwezekani serikali yote imejaa watu wa imani moja pekee.

Muhimu tu katika maisha yake yote ya kuitumikia hiyo nafasi, kamwe asijaribu kuiga nyendo za Jecha Salim Jecha.
Mbona hivi lakini kwani jina ndo uthibitisho wa imani yake??
 
Mbona hivi lakini kwani jina ndo uthibitisho wa imani yake??
Kwa hiyo unataka kusema mtu mwenye jina kama hilo anaweza kirahisi tu kuwa mmoja wa ndugu yetu katika imaan!

Hilo sahau aisee!!
 
Back
Top Bottom