Uteuzi Septemba 2, 2024: Rais Samia ateua na kuhamisha vituo vya kazi viongozi mbalimbali

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa na kuhamishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo:

A: Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya
1. Luteni Kanali Fredrick Faustin Komba ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji;

2. Bw. Mohamed Mussa Mtulyakwaku ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mtulyakwaku alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba; na

3. Bw. Olivanues Paul Thomas ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Thomas alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia.

B: Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya
1. Mhe. Halima Habib Okash amehamishwa kutoka Wilaya ya Bagamoyo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba;

2. Mhe. Gerald Romuald Mongella amehamishwa kutoka Wilaya ya Chemba kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua;

3. Mhe. Dkt. Rashid Mohamed Chuachua amehamishwa kutoka Wilaya ya Kaliua kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma;

4. Mhe. Salum Hamis Abdallah Kali amehamishwa kutoka Wilaya ya Kigoma kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido;

5. Mhe. Shaibu Issa Ndemanga amehamishwa kutoka Wilaya ya Lindi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo;

6. Mhe. Victoria Charles Mwanziva amehamishwa kutoka Wilaya ya Ludewa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi;

7. Mhe. Abdallah Mussa Mwaipaya amehamishwa kutoka Wilaya ya Mwanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara;

8. Mhe. Mwanahamisi Athumani Mukunda amehamishwa kutoka Wilaya ya Mtwara kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga;

9. Mhe. Emmanuela Kaganda Mtatifikolo amehamishwa kutoka Wilaya ya Arumeru kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati;

10
. Mhe. Lazaro Jacob Twange amehamishwa kutoka Wilaya ya Babati kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai;

11
. Mhe. Amir Mohamed Mkalipa amehamishwa kutoka Wilaya ya Hai kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru;

12.
Mhe. Dkt. Khalfan Boniface Haule amehamishwa kutoka Wilaya ya Musoma kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya;

13. Mhe. Juma Issa Chikoka amehamishwa kutoka Wilaya ya Rorya kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma; na

14. Mhe. Zakaria Saili Mwansasu amehamishwa kutoka Wilaya ya Uyui kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe.

C: Uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya
1. Bw. Mohamed Juma Ngasinda ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba; na

2. Bw. Shabani Shabani Hamimu ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia.

D: Uhamisho wa Makatibu Tawala wa Wilaya
1. Bi. Warda Abdallah Obathany amehamishwa kutoka Wilaya ya Iramba
kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni; na

2. Bi. Stella Edward Msofe amehamishwa kutoka Wilaya ya Kinondoni kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba.

E: Uhamisho wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
1. Bi. Hanan Mohamed Bafagh amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti; na

2. Bw. Hemedi Said Magaro amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

F: Uteuzi wa Wakuu wa Taasisi na Mwenyekiti wa Bodi
1. Bw. Mick Lutechura Kiliba ameteuliwa kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kiliba alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu;

2. Bw. Macrice Daniel Mbodo ameteuliwa kuwa Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania (TPC); na

3. Bw. Eliud Betri Sanga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

PIA SOMA
- Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya

Kila la heri kwao ,aamin [emoji2956]

#Nchi Kwanza [emoji7]
 
Lucas Mwashambwa ili akina Samia wakuheshimu jiheshimu. Maandiko yako yanatia kinyaa na kutapisha watu. Hizo sifa unazoandika zinakudhalilisha kiasi cha kuonekana umebeba usaha kichwani badala ya ubongo.
Wanaoteua wanajua zipi ni sifa na pongezi halisia, na zipi zinatolewa kama rushwa ya kumpofusha anayesifiwa.

Fikiria mtu anamwita Rais Samia ni komandoo wa vita, mara chuma cha reli!! Si unajua kabisa kuwa huyu anamdhihaki.
 
Wapi Lucas Mwashambwa, Msigwa?
Mkeka umegoma kusoma?
Wana nuksi?
Ila Mwashambwa wangemwonea huruma, wampe hata utendaji wa wa kijiji. Maana mpaka kujidhalilisha kwa kiwango anachoonesha hapa JF, ni dhahiri milango yote ya kupata maisha kwake imefunga. Kilichobakia ni kujidhalilisha alimradi tumbo lishibe.

Kwa mtu mwenye options nyingi za maisha hawezi kukubali kujidhalilisha kama ambavyo amekuwa akifanya.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa na kuhamishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo:

A: Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya
1. Luteni Kanali Fredrick Faustin Komba ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji;

2. Bw. Mohamed Mussa Mtulyakwaku ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mtulyakwaku alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba; na

3. Bw. Olivanues Paul Thomas ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Thomas alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia.

B: Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya
1. Mhe. Halima Habib Okash amehamishwa kutoka Wilaya ya Bagamoyo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba;

2. Mhe. Gerald Romuald Mongella amehamishwa kutoka Wilaya ya Chemba kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua;

3. Mhe. Dkt. Rashid Mohamed Chuachua amehamishwa kutoka Wilaya ya Kaliua kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma;

4. Mhe. Salum Hamis Abdallah Kali amehamishwa kutoka Wilaya ya Kigoma kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido;

5. Mhe. Shaibu Issa Ndemanga amehamishwa kutoka Wilaya ya Lindi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo;

6. Mhe. Victoria Charles Mwanziva amehamishwa kutoka Wilaya ya Ludewa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi;

7. Mhe. Abdallah Mussa Mwaipaya amehamishwa kutoka Wilaya ya Mwanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara;

8. Mhe. Mwanahamisi Athumani Mukunda amehamishwa kutoka Wilaya ya Mtwara kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga;

9. Mhe. Emmanuela Kaganda Mtatifikolo amehamishwa kutoka Wilaya ya Arumeru kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati;

10
. Mhe. Lazaro Jacob Twange amehamishwa kutoka Wilaya ya Babati kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai;

11
. Mhe. Amir Mohamed Mkalipa amehamishwa kutoka Wilaya ya Hai kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru;

12.
Mhe. Dkt. Khalfan Boniface Haule amehamishwa kutoka Wilaya ya Musoma kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya;

13. Mhe. Juma Issa Chikoka amehamishwa kutoka Wilaya ya Rorya kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma; na

14. Mhe. Zakaria Saili Mwansasu amehamishwa kutoka Wilaya ya Uyui kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe.

C: Uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya
1. Bw. Mohamed Juma Ngasinda ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba; na

2. Bw. Shabani Shabani Hamimu ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia.

D: Uhamisho wa Makatibu Tawala wa Wilaya
1. Bi. Warda Abdallah Obathany amehamishwa kutoka Wilaya ya Iramba
kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni; na

2. Bi. Stella Edward Msofe amehamishwa kutoka Wilaya ya Kinondoni kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba.

E: Uhamisho wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
1. Bi. Hanan Mohamed Bafagh amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti; na

2. Bw. Hemedi Said Magaro amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

F: Uteuzi wa Wakuu wa Taasisi na Mwenyekiti wa Bodi
1. Bw. Mick Lutechura Kiliba ameteuliwa kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kiliba alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu;

2. Bw. Macrice Daniel Mbodo ameteuliwa kuwa Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania (TPC); na

3. Bw. Eliud Betri Sanga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

PIA SOMA
- Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya

Luteni Kanali Fredrick Faustin Komba ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji;

Huyu ni mwanajeshi. Katiba inatamka wanajeshi wote hawapaswi kuwa wanachama wa any political party.

Sote tunajua, mkuu wa wilaya ana cheo ndani ya CCM ngazi ya wilaya kama mjumbe wa Kamati ya Siasa.

Kanali anaingia humo kama nani ikiwa Katiba inamkataa?
 
Back
Top Bottom