Uteuzi Septemba 2, 2024: Rais Samia ateua na kuhamisha vituo vya kazi viongozi mbalimbali

Kiutendaji inaongeza Ari ya utendaji, mkuu wa kitengo akikaa mahali muda mrefu utendaji Huwa unapungua. Mfano mbowe amekuwa mwenyekiti muda mrefu ndio kama CHADEMA imepotea kwenye ramani
inaongeza mzigo kwa serikali ina maana tumbua teua pia inaongeza wapokea viinua mgongo na huduma kedekede wengi maana wanaitwa wastaafu hao. Halafu kama mtu kasababisha wizi, ufisadi, au kafanya makosa kumtumbua tu sio solution inapaswa isiishie hapo achukuliwe hatua kama ni kufikishwa mahakamani afikishwe kwa wizi au matumizi mabovu ya madaraka.
mfano kama mtu alikuwa waziri akaiba bilioni 10 ndani ya mwaka, ukamtumbua na bila kumchukulia hatua. hiyo ni pesa nyingi ambayo asingeweza kuipata kwa mshahara wake hata angekaa kwa miaka yote mitano. so, atakayeingia naye ataiba akijua atakachovuna ni kikubwa hata akitumbuliwa haina neno maana atakuwa kavuna kingi kuliko hata angekaa muda wa miaka mitano akipokea anachostahili.
tumbua tumbua bila kuwafikisha mahakamani na kuwatapisha walichoiba haiwezi kurekebisha chochote
 
Marais wa CCM wanateuana mpaka siku ya mwisho ya kuwa madarakani.

Kikwete alifanya uteuzi siku moja kabla ya kuapishwa Magufuli.
 
Uchawa bwana! Kila kitu mtamkubali hata akienda maliwatoni 😂😂😂😂! Eti kwanza nimshukuru sana... kwa kuamka 😂😂😂
 
Mama hacheki na kima, yale majambazi ya awamu ya tano yanadhani mama atayaona ya muhimu katika uchaguzi, yakiinua ki hwa tu anakata
 
Hajidhalilishi....

Anakisemea chama bora chenye imani 3 kuntu zinazoshahabiana na asili ya maisha ya watanzania [emoji7]

Kuitetea imani ya chama ni bora zaidi ya hizo TEUZI....

Haiwezekani WOTE tukateuliwa kuwa viongozi....

#Nchi Kwanza [emoji450][emoji441][emoji449]

Karibu Al Kasus [emoji2956]
 
Siku anayoteuliwa anapewa KADI ya chama...inakoma siku akitenguliwa na kurudi BARRACKS....

#Nchi Kwanza[emoji2956]
 
Hongera kwao!
Moja ya kazi za ajabu ni hizi ukuu wa wilaya mkoa katibu mkurugenzi wilaya halmashauri kata na tarafa.
Mfano mtu alikua mkuu wa wilaya mwanga , leo anapelekwa mtwara makazi na familia dar!
 
Hongera kwao!
Moja ya kazi za ajabu ni hizi ukuu wa wilaya mkoa katibu mkurugenzi wilaya halmashauri kata na tarafa.
Mfano mtu alikua mkuu wa wilaya mwanga , leo anapelekwa mtwara makazi na familia dar!
Utumishi wa umma....
 
Wanaoteua wanajua zipi ni sifa na pongezi halisia, na zipi zinatolewa kama rushwa ya kumpofusha anayesifiwa.

Fikiria mtu anamwita Rais Samia ni komandoo wa vita, mara chuma cha reli!! Si unajua kabisa kuwa huyu anamdhihaki.
Wewe mwenye akili umeteuliwa wapi .
Mimi nilikua high levels career diplomat pale MFA tangu enzi ya JK na kugeukia mambo mengine. Japo samia hana hizo akili za kutosha lakini amini nakuambia kwa huo utumbo unaoandika humu hata yeye anasikia kinyaa na kichefu chefu..... sifa za mwenye njaa ni kinyaa kwa mpishi.
 
Watekaji wa maporini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…