Wakuu,
Wananchi mmeoana vile nguvu yenu inayoweza kufanya! Kidogo tu wametema bungo, Murilo anaongea kistaarabu kama anaongea na wananchi wa Tanzania😂🤣🤣. Raia hawakuogopa kitu jana, polisi hawakuthubutu kupiga hata risasi moja juu, walijua nini kinaenda kutokea.
Ila watendaji hawa wana makosa gani wakati shida ipo kwenye serikali? Tunajua tatizo lilipo lakini zigo wanaangushiwa kwengine.
Gen Z Mbagala fanyeni kitu tupone😂😂🤣, tupo vizuri, mambo yanaenda vizuri kabisaaa!
=====
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-
(i) Bw. Said Habibu Tunda ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART). Bw. Tunda anachukua nafasi ya Dkt. Athumani Kihamia ambaye uteuzi wake umetenguliwa; na
(ii) Bw. Pius Andrew Ng'ingo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART). Bw. Ng'ingo anachukua nafasi ya Bw. Waziri Kindamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Uteuzi huu unaanza mara moja.
Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu