Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa DCI (Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai). Je, Rais Samia amepotoshwa?

Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa DCI (Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai). Je, Rais Samia amepotoshwa?

Mamlaka ya uteuzi inalipa fadhila kwa msalaba aliobebeshwa DCI mpya,kwa kukubali kutumika au Mamlaka ya uteuzi imepotoshwa.Yote kwa yote Mamlaka ya uteuzi japokuwa haipangiwi nani wakumteua, ni vema ikajitafakari.Kuna ukakasi kwenye baadhi ya teuzi.
 
Nchi hii ina matahira, sorry, watu wa ajabu sana! Ni kulalamika tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu na kujifanya wanajua na kuwajua watu vuzuri mpaka inaboa.
Yaani mtu asifanye kazi yake kisa mna bifu nae mliloambukizwa na bwana wenu mbowe?!!!!!!
Ni majinga kweli. Sijui Mbowe kawa Mungu wao!!?
 
Kingai kama king wa makosa ya jinai

Kazi iendelee!!

Mama apewe heshima yake maana ndye mwenye maamuzi ya mwisho hapa nchini
 
Afande Kingai hakupaswa kupewa nafasi ya DCI hata kidogo, Imani ya Raia kwa huyu mtu ni ndogo sana, Wakati wa kesi ya Mbowe huyu alihusishwa na utesaji na utekaji, Na hata majibu yake mahakamani alijichanganya sana kuhusu kuwahamisha watuhumiwa tokea kituo kimoja cha polisi kwenda kingine na malengo yake kuhusu utesaji

*ndio maana shavu.. No smart people allowed!
Ndyo kashakuwa DCI hivyo, hakuna namna zaidi ya kukaa kimya

Kazi iendelee
 
Kuna mambo mawili nimeona
1.Ama anapewa uteuzi kuwa ni mtoto wa Magufuli kikazi.
2.Au ameandaliwa zengwe aje kutumbuliwa kila kitu kinawezekana.
Ona mjinga mwingine huyu!! Yaani kwamba anaogopwa mpaka awe DCI ndo kisha atumbuliwe!!? Hivi nyie CHADEMA mbona vichwani ni kutupu?
 
Kwa hali hii, tuendelee tu kuipigania Katiba Mpya. Hii ya sasa ni ya hovyo mpaka basi. Maana inampa mwanadamu mamlaka ya kimungu!

Yaani hata leo aamue tu kumteua mfanyakazi wake wa ndani kuwa DC, hakuna wa kumzuia! Wala mumhoji!
Katiba Ni bonge la janga hapa nchini
 
Mungu atusimamie tu ili tusirudi tulikotoka.

All in all, Katiba Mpya huenda ikasaidia kupunguza haya malalamiko yasiyoisha kwenye teuzi mbalimbali.
Tabia ya kulalamika lalamika haitokaa iishe. Mpaka Mbowe astaafishwe
 
Connection ndio mpango mzima, kama maDC wanaweza kuhonga wabaki kwenye vyeo vyao au wapandishwe vyeo, unafikiri hao wanaofanya vetting wanauadilifu gani?
 
Nchi hii ina matahira, sorry, watu wa ajabu sana! Ni kulalamika tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu na kujifanya wanajua na kuwajua watu vuzuri mpaka inaboa.
Yaani mtu asifanye kazi yake kisa mna bifu nae mliloambukizwa na bwana wenu mbowe?!!!!!!
Tumia lugha ya staha,matusi na kejeli hayakusaidii chochote!Heshimu watu wengine na wewe utaheshimiwa,hii ni forum huru kila mtu kuwa na mtazami wake!Ukiona mtu hana mtazamo sawa na wewe,jengeni hoja na kama huna ustagimilivu pita tu kimya kimya kuliko kuanza kutukana watu namna hii!wengine humu ni umri sawa na mama Yako!
 
Uteuzi huu hauligawi Taifa, labda unagawa akili zako wewe na Saccos yako
Muonyeni huyo Kingai kwani hakuna anayeijua kesho yake!
Au hamjifunzi Kwa kinachomtokea Sabaya?
Mlimpa Kichwa hivi hivi,mchuma janga hula na wa kwao!
 
Hata mfano mmoja wa uovu wa kingai sijauona. Umelia sana bila mifano.
 
Kwani hujui ule uchafu aliofanya ilikuwa ni sehemu ya kazi yake?
Wateuzi wakiwa waovu uwe na uhakika wateuliwa watakuwa waovu zaidi.
 
Kwani huko kwenu kuna jambo limebadilika tangu afe JPM? Watu ni walewale tu isipokuwa Rais mwingine....

Mama anaupiga mwingi hasa akifanya tuyapendayo,tusiyopenda anakosea.......nchi hii tunachoshana sana
 
CCM ni wale wale huwezi kujua alimfanyia nini Mama yetu Samia
 
Back
Top Bottom