Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa DCI (Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai). Je, Rais Samia amepotoshwa?

Wizara za Mambo ya Nje na Mambo ya Ndani ndiyo viongozi wa itifaki na maadili katika Serikali na ndiyo washauri wakuu wa Rais katika mambo hayo licha ya vetting inayofanywa na kundi ndogo. Hata kama kuna mtu binafsi anampenda Kingai, sijaelewa inakuwaje Rais anashauriwa kufanya jambo ambalo halina tija kwa Rais mwenyewe wala kwa raia ambao Rais anawatumikia! Ilitakiwa katika vetting ielezwe jinsi jamii itakavyopokea uteuzi wa mtu kama Kingai au mtu wa namna hiyo kutoka na raia walivyotambulishwa na vyombo vya habari kuhusu matukio ambayo Kingai amehusishwa. Polisi kamili ni mtu ambaye raia wa kawaida anatakiwa ajisikie amani kuwa karibu naye. Kwani Kingai hawezi kupewa zawadi nyingine ambayo haikorofishi dhamira ya raia kiasi hiki? Namwonea huruma na kumpa pole Rais wetu.

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
Hakika katika teuzi zake za sasa, Rais Samia kaharibu na kakosea sana kwa Ramadhani Kingai...

Huyu bwana vetting yake ya kumshusha (kumfuta kazi kabisa) au kumpandisha cheo ilikuwa ni namna alivyoshughulikia kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe...

Ni dhahiri shahiri kabisa kuwa, alishindwa na hana uelewa wa sheria kwa kiwango kikubwa...

Hastahili kuwa DCI wala hata ukuu wa idara yoyote huko polisi achilia mbali ukuu wa kituo chochote cha polisi...!!

Inashangaza sana kuwa, Rais Samia na washauri wake wooooote ktk kutafuta tafuta kwao wamekosa polisi yeyote mwenye sifa ya kumpa nafasi ya u - DCI kiasi cha kumpachika huyu polisi mjinga mbambika kesi za watu...

Kama ndivyo, basi ndani ya polisi kuna ukame wa professional kwa kiwango cha kutisha sana...!

Rais Samia na CCM yako, mmekaribisha critism isiyo na sababu ambayo mngeweza kuiepuka kwa kufanya maamuzi sahihi tu....


Hapa Rais hatukufichi kwa lolote, tunakuambia wazi kabisa UMEKOSEA, UMEUPIGA MCHACHE MNO...!!
 
wakuu inje ya mada kidogo ivi kati ya mkurugenzi wa makosa ya jinai(DCI) ma mkurugenzi wa mashtaka (DPP) nani ni boss wa mwenzake na je majukumu hayaingiliani maana makosa ya jinai nayo ni mashtaka ufafanuzi
 
Hapa mama kazingua.
Mtu amedhihirisha utupu wa bongo lake kwenye kesi ya Mbowe, unaanzaje kumpa nafasi nyeti kama hiyo?
Birds of feather flock together.
Ccm ni ileile ya walio kaburini na walio hai; baba moya na mama moya.

Ukisema bongolake tupu unamaana gani, we hufahamu kwamba anamabosiwake, naunaamini mabosiwake hawakujua kinacho endelea kwenye kesi ya mbowe.
 
Kingai anajua hadi kesho alipo Moses lijenje.

Samia hapo kwa kingai amembwela vibaya sana.

Ameshauriwa vibaya sana
 
Rais HAPANGIWI.......Ni ukosefu wa ADABU na HESHIMA kuanza kumpangia na kumshinikiza Rais.

Pongezi kwa mteule.
kamwe usisikilize majungu.....piga kazi.
Majungu na fitina havina nafasi katika awamu hii ya 6.
sisi ndo boss wake!!ewananchi ni maboss wa rais!!atapangiwa tuuu
 
Anayefanya Teuzi siyo Samia
 
Habarini wa JF .sisi tusiokuwa na uwezo hata cheo ni mgumu kupata.
baada kusoma mkeka wa uteuzi nimekuta spekta kingai kuwa DCI .
na mtu kuwa level ya DCI kidogo swala la sheria na mienendo ya kesi kuwa vizuri.

Swali tu !
 
Jeshi la Polisi litavunjwa
 
Ukiacha issue ya Mbowe,jamaa yupo vizuri kiutendaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…