Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa DCI (Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai). Je, Rais Samia amepotoshwa?

Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa DCI (Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai). Je, Rais Samia amepotoshwa?

Kwanini kama Taifa tunarudia makosa ya kuteua watu wenye makando kando kama Afande Ramadhani Kingai? Huyu mtu kwa sasa anafahamika na kila Raia kwa matendo yake yaliyojidhihirisha pale Mahakamani wakati wa kesi ya Mbowe

Je, tunasubiri afanye ukatili na unyama wa kiasi gani kwenye hili Taifa?

Tulishajifunza wakati wa JPM umuhimu wa vetting ya viongozi kwa yaliyotokea. Je, bado tunaendelea kujifunza.

Afande Kingai hakupaswa kupewa nafasi ya DCI hata kidogo, Imani ya Raia kwa huyu mtu ni ndogo sana, Wakati wa kesi ya Mbowe huyu alihusishwa na utesaji na utekaji, Na hata majibu yake mahakamani alijichanganya sana kuhusu kuwahamisha watuhumiwa tokea kituo kimoja cha polisi kwenda kingine na malengo yake kuhusu utesaji

Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa Mkurugenzi wa makosa ya jinai unaligawa Taifa ambalo Rais Samia alikuwa anafanya jitihada za kuliunganisha kwa maridhiano

Kwenye kesi ya Mbowe pale mahakamani, Afande Kingai alikuwa shahidi mkuu upande wa jamhuri na ushahidi wake alioutoa pale mahakamani wa kuwanunulia watuhumiwa Mo energy ikawa mwanzo wa watu kuamini huyu Bwana ameshiriki Katika kesi ya mchongo kuanzia kudraft mpaka kupeleka mahakamani.

Afande Kingai alishindwa kujibu maswali ya mawakili wa utetezi hata moja na hata maswali yaliyohusiana na kitendea kazi chake ya General Orders of police ( PGO) alionekana haelewi pale Mahakama ya uhujumu Uchumi.

Ushahidi wa Afande Kingai ambaye alikuwa Shahidi mkuu ulileta mkanganyiko pale Mahakama ya Uhujumu Uchumi na ndio ukawa mwanzo wa watu kufahamu siri ya kesi ya akina Mbowe pamoja na Kikosi kazi maalum kilichojumuisha Afande Goodluck

Maswali ya kujiuliza sisi kama Raia wa nchi hii:

Unawezaje kumpa mtu nafasi ya DCI wakati umma wa Watanzania wanafahamu huyu mtu amechafuka?

Je, huu ndio mwanzo wa watu kubambikiwa kesi za mauaji hapa nchini?

Je, uteuzi huu Bwana Kingai sio ni mwanzo wa kufumua madonda ambayo Rais Samia alishaanza kuyaponya?

Moja ya watu kuzidi kudai Katiba Mpya ni kutokana na uteuzi wa watu aina ya Afande Kingai, Tungekuwa na tume maalum ya kuchuja na kuteua aina ya watu kama Afande Kingai kama Rasimu ya Jaji Warioba alivyopendekeza tusingekuwa na utata
Wizara za Mambo ya Nje na Mambo ya Ndani ndiyo viongozi wa itifaki na maadili katika Serikali na ndiyo washauri wakuu wa Rais katika mambo hayo licha ya vetting inayofanywa na kundi ndogo. Hata kama kuna mtu binafsi anampenda Kingai, sijaelewa inakuwaje Rais anashauriwa kufanya jambo ambalo halina tija kwa Rais mwenyewe wala kwa raia ambao Rais anawatumikia! Ilitakiwa katika vetting ielezwe jinsi jamii itakavyopokea uteuzi wa mtu kama Kingai au mtu wa namna hiyo kutoka na raia walivyotambulishwa na vyombo vya habari kuhusu matukio ambayo Kingai amehusishwa. Polisi kamili ni mtu ambaye raia wa kawaida anatakiwa ajisikie amani kuwa karibu naye. Kwani Kingai hawezi kupewa zawadi nyingine ambayo haikorofishi dhamira ya raia kiasi hiki? Namwonea huruma na kumpa pole Rais wetu.

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
Hakika katika teuzi zake za sasa, Rais Samia kaharibu na kakosea sana kwa Ramadhani Kingai...

Huyu bwana vetting yake ya kumshusha (kumfuta kazi kabisa) au kumpandisha cheo ilikuwa ni namna alivyoshughulikia kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe...

Ni dhahiri shahiri kabisa kuwa, alishindwa na hana uelewa wa sheria kwa kiwango kikubwa...

Hastahili kuwa DCI wala hata ukuu wa idara yoyote huko polisi achilia mbali ukuu wa kituo chochote cha polisi...!!

Inashangaza sana kuwa, Rais Samia na washauri wake wooooote ktk kutafuta tafuta kwao wamekosa polisi yeyote mwenye sifa ya kumpa nafasi ya u - DCI kiasi cha kumpachika huyu polisi mjinga mbambika kesi za watu...

Kama ndivyo, basi ndani ya polisi kuna ukame wa professional kwa kiwango cha kutisha sana...!

Rais Samia na CCM yako, mmekaribisha critism isiyo na sababu ambayo mngeweza kuiepuka kwa kufanya maamuzi sahihi tu....

Hapa Rais hatukufichi kwa lolote, tunakuambia wazi kabisa UMEKOSEA, UMEUPIGA MCHACHE MNO...!!
 
wakuu inje ya mada kidogo ivi kati ya mkurugenzi wa makosa ya jinai(DCI) ma mkurugenzi wa mashtaka (DPP) nani ni boss wa mwenzake na je majukumu hayaingiliani maana makosa ya jinai nayo ni mashtaka ufafanuzi
 
Hapa mama kazingua.
Mtu amedhihirisha utupu wa bongo lake kwenye kesi ya Mbowe, unaanzaje kumpa nafasi nyeti kama hiyo?
Birds of feather flock together.
Ccm ni ileile ya walio kaburini na walio hai; baba moya na mama moya.

Ukisema bongolake tupu unamaana gani, we hufahamu kwamba anamabosiwake, naunaamini mabosiwake hawakujua kinacho endelea kwenye kesi ya mbowe.
 
Kingai anajua hadi kesho alipo Moses lijenje.

Samia hapo kwa kingai amembwela vibaya sana.

Ameshauriwa vibaya sana
 
Rais HAPANGIWI.......Ni ukosefu wa ADABU na HESHIMA kuanza kumpangia na kumshinikiza Rais.

Pongezi kwa mteule.
kamwe usisikilize majungu.....piga kazi.
Majungu na fitina havina nafasi katika awamu hii ya 6.
sisi ndo boss wake!!ewananchi ni maboss wa rais!!atapangiwa tuuu
 
MH Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan kwakweli japo jeshi Zima la polisi limekuwa bovu Sanaa lakini Kuna wachache ambao Wana hofu ya Mungu, na Taasisi kubwa na ya muhimu kama hili jeshi halitakiwi kuwa na kiongozi asiyetoa Haki au Mwongo.

Kama mama una nia kweli ya kulirekebisha watu kama KINGAI hawakupaswa kupewa ofisi kubwa maana kwa UONGO na uonevu aliowafanyia watu akiwa ngazi za chini akiwa Ngazi uliyompa atakuwa mbaya zaidi .

Sio polisi mwenye maadili hasa msingiziaji mporaji wa haki za watu mtesaji ana damu kwenye vganja vyake.

Jiepushe nae, HAWEZI kutenda Haki tunakuomba Unda na kulisuka upya Hili jeshi lililopoteza maana ya jeshi la kusimamia Haki.

Kwa hili nasema WAMBURA SAWA LAKINI SIO KINGAI, HAPANA.
Anayefanya Teuzi siyo Samia
 
Habarini wa JF .sisi tusiokuwa na uwezo hata cheo ni mgumu kupata.
baada kusoma mkeka wa uteuzi nimekuta spekta kingai kuwa DCI .
na mtu kuwa level ya DCI kidogo swala la sheria na mienendo ya kesi kuwa vizuri.

Swali tu !
 
Afande Kingai hakupaswa kupewa nafasi ya DCI hata kidogo, Imani ya Raia kwa huyu mtu ni ndogo sana, Wakati wa kesi ya Mbowe huyu alihusishwa na utesaji na utekaji, Na hata majibu yake mahakamani alijichanganya sana kuhusu kuwahamisha watuhumiwa tokea kituo kimoja cha polisi kwenda kingine na malengo yake kuhusu utesaji

*ndio maana shavu.. No smart people allowed!
Jeshi la Polisi litavunjwa
 
Kwanini kama Taifa tunarudia makosa ya kuteua watu wenye makando kando kama Afande Ramadhani Kingai? Huyu mtu kwa sasa anafahamika na kila Raia kwa matendo yake yaliyojidhihirisha pale Mahakamani wakati wa kesi ya Mbowe

Je, tunasubiri afanye ukatili na unyama wa kiasi gani kwenye hili Taifa?

Tulishajifunza wakati wa JPM umuhimu wa vetting ya viongozi kwa yaliyotokea. Je, bado tunaendelea kujifunza.

Afande Kingai hakupaswa kupewa nafasi ya DCI hata kidogo, Imani ya Raia kwa huyu mtu ni ndogo sana, Wakati wa kesi ya Mbowe huyu alihusishwa na utesaji na utekaji, Na hata majibu yake mahakamani alijichanganya sana kuhusu kuwahamisha watuhumiwa tokea kituo kimoja cha polisi kwenda kingine na malengo yake kuhusu utesaji

Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa Mkurugenzi wa makosa ya jinai unaligawa Taifa ambalo Rais Samia alikuwa anafanya jitihada za kuliunganisha kwa maridhiano

Kwenye kesi ya Mbowe pale mahakamani, Afande Kingai alikuwa shahidi mkuu upande wa jamhuri na ushahidi wake alioutoa pale mahakamani wa kuwanunulia watuhumiwa Mo energy ikawa mwanzo wa watu kuamini huyu Bwana ameshiriki Katika kesi ya mchongo kuanzia kudraft mpaka kupeleka mahakamani.

Afande Kingai alishindwa kujibu maswali ya mawakili wa utetezi hata moja na hata maswali yaliyohusiana na kitendea kazi chake ya General Orders of police ( PGO) alionekana haelewi pale Mahakama ya uhujumu Uchumi.

Ushahidi wa Afande Kingai ambaye alikuwa Shahidi mkuu ulileta mkanganyiko pale Mahakama ya Uhujumu Uchumi na ndio ukawa mwanzo wa watu kufahamu siri ya kesi ya akina Mbowe pamoja na Kikosi kazi maalum kilichojumuisha Afande Goodluck

Maswali ya kujiuliza sisi kama Raia wa nchi hii:

Unawezaje kumpa mtu nafasi ya DCI wakati umma wa Watanzania wanafahamu huyu mtu amechafuka?

Je, huu ndio mwanzo wa watu kubambikiwa kesi za mauaji hapa nchini?

Je, uteuzi huu Bwana Kingai sio ni mwanzo wa kufumua madonda ambayo Rais Samia alishaanza kuyaponya?

Moja ya watu kuzidi kudai Katiba Mpya ni kutokana na uteuzi wa watu aina ya Afande Kingai, Tungekuwa na tume maalum ya kuchuja na kuteua aina ya watu kama Afande Kingai kama Rasimu ya Jaji Warioba alivyopendekeza tusingekuwa na utata
Ukiacha issue ya Mbowe,jamaa yupo vizuri kiutendaji
 
Back
Top Bottom