Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
- Thread starter
-
- #21
Nilichokuhadithia ni kitu halisi na kimetokea. Ni juu yako kukubali au kukataa, uamuzi ni wako na si wa mtu mwingine.Wewe ni kati ya wale waumini wasiojua nini maana ya utumishi ndugu, huwezi kusema kuwa Alex Malasusa kwamba avae utumishi wa baba yake ni kitu kigumu na hakiwezekani daima.
Kama ingekuwa huduma inayorithishwa basi watoto wa mzee kulola wangebeba huduma ya baba yake lakini ona akina Daniel wanaishia kujisifu na hakuna walichofanya kasome kitabu cha 2Samwel Sura zote unaweza kupata majibu ya hichi ulichokiandika na mada mfu
Palipo na ukweli unafiki unaingiaje?Mbona kama unaleta ushuhuda wa kinafiki? Malasusa hakupaswa kurudi kuliongoza kanisa la KKKT, kama waliona Bagonza hafai wangempa yule wa Iringa asiyejulikana misimamo yake ya kisiasa ikoje
Sijui siku hizi, lakini miaka hiyo mlio bongolala mnapungia tu mkielekea Morogoro.Kibaha ilipewa hadhi ya vipaji lini?
Hongera baba askofu Alex Malasusa [emoji120][emoji106][emoji7][emoji2956]Uteuzi wa Askofu Malasusa haukuja hivi hivi.
Ni maajabu ya mipango ya Mungu.
Wengi hawaijui historia ya familia ya Malasusa.
Alex Gehaz Malasusa ni mtoto wa pili wa mchungaji mzee Gehaz Malasusa.
Mzee Gehaz Malasusa alisomea uchungaji miaka ya mwanzoni ya 1960 hadi huko Marekani, ambako alitunukiwa shahada ya Masters katika Theology.
Aliporudi Tanzania ili kuhudumia kanisa, kwa macho ya wachungaji wenziwe alikuwa over qualified kwa wakati ule.
Viongozi wa kanisa Dayosisi ya Mashariki na Pwani(ilikuwa ina eneo kubwa hadi Morogoro miaka hiyo) kwa kuhofia nafasi zao, wakaamua kumuweka mbali sana na makao makuu.
Mzee Gehaz Malasusa akapangwa Morogoro, tena vijijini huko, karibu na Kisaki.
Mchungaji Gehaz hakukataa wito akaenda huko vijijini na Masters yake.
Huko alihubiri na kufanya maajabu.
Aliwahubiri wana vijiji kuacha mila za kizamani ambapo, walikuwa wana waua mapacha.
Familia ikizaa mapacha ilionekana ni mkosi, mapacha na walikuwa wanauwawa.
Kati ya pacha waliookolewa ni mtu mmoja ambaye akaondokea kuwa na akili nyingi zisizo za kawaida.
Huyu mtu yupo hadi leo na anaitwa John Mpapalika.
Natoa huu ushuhuda ili Mungu wacha aitwe Mungu.
John alisoma kutoka vijijini na akafaulu vizuri hadi shule za vìpaji maalum, Kibaha tulikofahamiana.
John aliendelea kupasua masomoni na baada ya high school alienda moja kwa moja hadi Uingereza ambako alisoma na alifikia kiwango cha PhD, mtoto aloyeokolewa na mchungaji mzee Gehaz Malasusa.
Kwa wanao mfahamu John Mpapalika, alikuwa Mkurugenzi pale TCRA, sasa amestaafu.
Huu ushuhuda ulitolewa siku ya misa ya kumsindikiza mchungaji mzee Gehaz Malasusa alipo fariki, pale usharika wa Mbezi Beach KKKT.
Nlipata ushuhuda vile vile wa rafiki yangu aliyeombewa na mchungaji mzee Gehaz Malasusa baada ya kuvamiwa na majambazi.
Wale majambazi walukuja kufariki, wote.
Cha ajabu kwa mzee Malasusa hakulalamikia cheo wala kugombea madaraka maisha yake yote, licha ya kuwa over qualified.
Alitumikia kanisa kama Biblia inavyosema, kuchunga kondoo wa Bwana.
Siku ya kumuaga mchungaji mzee Gehaz Malasusa, kuna maaskofu walipata taabu kujieleza kwa nini walimtupa vijijini, tena Morogoro.
Hivyo kuinuliwa katika uongozi wa juu mtoto wake Alex umekuja si kwa mshangao tu, bali inaonekana kama mipango ya Mungu kumuinua mtoto wa mtumishi wake aliye mtumikia Mungu bila malalamiko yoyote, licha ya kudharauliwa na kuonewa.
Hongera Baba Askofu Alex Gehaz Malasusa, umechaguliwa kwa mpango wa Mungu.
Nimekuuliza ni lini au miaka gani ambayo Kibaha High school ilikuwa designated kuwa Special school ili kujua kama kwa mtu ambaye kwa sasa amestaafu,alipokuwa sekondari Kibaha tayari ilishapewa hadhi ya Special school.Sijui siku hizi, lakini miaka hiyo mlio bongolala mnapungia tu mkielekea Morogoro.
https://kibahasec.sc.tz/Nimekuuliza ni lini au miaka gani ambayo Kibaha High school ilikuwa designated kuwa Special school ili kujua kama kwa mtu ambaye kwa sasa amestaafu,alipokuwa sekondari Kibaha tayari ilishapewa hadhi ya Special school.
Mi nashangaa watu mnavyohangaika.Askofu si kachaguliwa na maaskofu wenzie kwa asilimia zaidi ya 60%, maana yake wanamkubali vizuri tu.Sasa shida ya nini?Mbona kama unaleta ushuhuda wa kinafiki? Malasusa hakupaswa kurudi kuliongoza kanisa la KKKT, kama waliona Bagonza hafai wangempa yule wa Iringa asiyejulikana misimamo yake ya kisiasa ikoje
Ukiwa level ya upeo wa kuona na kushughulikia chawa, huinuki ng'o kifikra.Chawa wamegawanyika kuna akina level ya mwijaku na kuna wengine wapo viongozi makanisani...niseme tu Chawa ni Chawa tu. Kiongozi kama huyu huwezi kusema atasimama upande wa Mungu na haki Bali ataangalia serikali inamtaka afanye nini kwa manufaa ya wanasiasa wanaotalawa na si Mungu.
Imeanzishwa 1965. Nazungumzia kuwa designated kuwa Special school.https://kibahasec.sc.tz/
Soma hapo, itakusaidia.
Naeleza ya ukweli ninayoyafahamu.mleta mada katumwa! yaani ...
Hiyo link umesoma na kuelewa?Imeanzishwa 1965. Nazungumzia kuwa designated kuwa Special school.
Serikali kuitambua Kibaha kuwa vipaji maalum ilikuwa miaka ya ngapi ngapi? Sio kuanzishwa ambayo ni 1965.John alisoma kutoka vijijini na akafaulu vizuri hadi shule za vìpaji maalum, Kibaha tulikofahamiana.
Hiyo link umesoma na kuelewa?
Na lisemwalo lipoo...Ya kuambiwa changanya na za kwako.
Mimi naona tatizo ni hiyo halmashauri yao iliyompendekeza au laa kuna external forces.. Kingine watakuwa na katiba ya hovyo kabisa.Malasusa Ni mhuni Kama wahuni wengine unao wajua.
MTU keshatumikia vipindi viwili bado anaona madaraka matamu anagombea Tena. Hivi Ni kipi kigeni atakileta ambacho hakukifanya kwa miaka nane? Hii Ni sawa na kumpa Wahasira ukuu wa mkoa au uwaziri.
Hivi kkkt hakuna vijana?
KKKT Sasa Ni Kama CCM.
Wanafanya recycling...........