Uteuzi wa Askofu Malasusa ni maajabu ya Mungu!

Uteuzi wa Askofu Malasusa ni maajabu ya Mungu!

Amjue wapi? Jamaa wameamua watuvurugie kanisa, uchaguzi wa kanisa unakua kama CC za vyama! Nashangaa hata hawa waliomchagua najua kuna namna, imefika mahali sisi tunaoabudu kwenye kanisa hili tutaanza kuhoji hizi phd zao!

Kanisa limeanza kua kama Saccos tunalipishwa madeni ya mikopo iliyokopwa, mvua ya sadaka! Wajameni hivi mnadhani washarika wataacha kukimbilia kwa wazee wa “pokeaaaa, jioniii ya leo”!

Kwa uchaguzi huu na matokeo haya, tumeingia chaka! Ni suala la muda tu!
Imani ni suala la mtu na moyo wake.
Kanisa halijawahi kumfungia mtu milango.
Saa wewe kama utaamua kwenda kwa Toboa Tobo, au Mwamposa , huo ni uamuzi wako.
 
Ni maoni yangu.
Upo sawa kabisa kwa kuwa ni maoni yako.
Naamini kuna vigezo vingi sana vinatumika, lakini pia kuna baadhi ya Mapadri wanapenda maisha ya upadri tu na hawapendi kupewa daraja la Uaskofu.

Rumours had it that the late Fr. Saba (aliekua Katibu wa TEC) aliwahi kupendekezwa lakini hakua tayari.
 
Uteuzi wa Askofu Malasusa haukuja hivi hivi.
Ni maajabu ya mipango ya Mungu.
Wengi hawaijui historia ya familia ya Malasusa.
Alex Gehaz Malasusa ni mtoto wa pili wa mchungaji mzee Gehaz Malasusa.
Mzee Gehaz Malasusa alisomea uchungaji miaka ya mwanzoni ya 1960 hadi huko Marekani, ambako alitunukiwa shahada ya Masters katika Theology.

Aliporudi Tanzania ili kuhudumia kanisa, kwa macho ya wachungaji wenziwe alikuwa over qualified kwa wakati ule.

Viongozi wa kanisa Dayosisi ya Mashariki na Pwani(ilikuwa ina eneo kubwa hadi Morogoro miaka hiyo) kwa kuhofia nafasi zao, wakaamua kumuweka mbali sana na makao makuu.

Mzee Gehaz Malasusa akapangwa Morogoro, tena vijijini huko, karibu na Kisaki.
Mchungaji Gehaz hakukataa wito akaenda huko vijijini na Masters yake.
Huko alihubiri na kufanya maajabu.

Aliwahubiri wana vijiji kuacha mila za kizamani ambapo, walikuwa wana waua mapacha.

Familia ikizaa mapacha ilionekana ni mkosi, mapacha na walikuwa wanauwawa.

Kati ya pacha waliookolewa ni mtu mmoja ambaye akaondokea kuwa na akili nyingi zisizo za kawaida.
Huyu mtu yupo hadi leo na anaitwa John Mpapalika.

Natoa huu ushuhuda ili Mungu wacha aitwe Mungu.

John alisoma kutoka vijijini na akafaulu vizuri hadi shule za vìpaji maalum, Kibaha tulikofahamiana.

John aliendelea kupasua masomoni na baada ya high school alienda moja kwa moja hadi Uingereza ambako alisoma na alifikia kiwango cha PhD, mtoto aloyeokolewa na mchungaji mzee Gehaz Malasusa.

Kwa wanao mfahamu John Mpapalika, alikuwa Mkurugenzi pale TCRA, sasa amestaafu.

Huu ushuhuda ulitolewa siku ya misa ya kumsindikiza mchungaji mzee Gehaz Malasusa alipo fariki, pale usharika wa Mbezi Beach KKKT.

Nlipata ushuhuda vile vile wa rafiki yangu aliyeombewa na mchungaji mzee Gehaz Malasusa baada ya kuvamiwa na majambazi.
Wale majambazi walukuja kufariki, wote.

Cha ajabu kwa mzee Malasusa hakulalamikia cheo wala kugombea madaraka maisha yake yote, licha ya kuwa over qualified.
Alitumikia kanisa kama Biblia inavyosema, kuchunga kondoo wa Bwana.
Siku ya kumuaga mchungaji mzee Gehaz Malasusa, kuna maaskofu walipata taabu kujieleza kwa nini walimtupa vijijini, tena Morogoro vijini.

Hivyo kuinuliwa katika uongozi wa juu mtoto wake Alex umekuja si kwa mshangao tu, bali inaonekana kama mipango ya Mungu kumuinua mtoto wa mtumishi wake aliye mtumikia Mungu bila malalamiko yoyote, licha ya kudharauliwa na kuonewa.

Hongera Baba Askofu Alex Gehaz Malasusa, umechaguliwa kwa mpango wa Mungu.
UTEUZI WAKE HAUNA BARAKA ZA MUNGU HUWEZI KUWAKATA WENGINE KWA NIA MBAYA ILI UPITE WEWE
 
UTEUZI WAKE HAUNA BARAKA ZA MUNGU HUWEZI KUWAKATA WENGINE KWA NIA MBAYA ILI UPITE WEWE
Kwa hiyo yeye aliwakata wengine ili yeye ajichague?
Tumia akili kidogo, pale palikuwa na wachugaji na maaskofu zsidi ya 250.
 
Askofu Alex Malasusa hakugombea kuwa mkuu mpya wa KKKT. Jina lake na wengine walipendekezwa kwa Halmashauri Kuu wakapigiwa kura. A.M. akashinda kwa zaidi ya theluthi mbili.
Sio sawa kumchafua mtu yoyote.
Askofu kiongozi wa KKKT haitwi "His Holiness the ......."
 
Back
Top Bottom