Uteuzi wa Biswalo ni kutonesha kidonda cha Umma, lakini akapumzike salama

Uteuzi wa Biswalo ni kutonesha kidonda cha Umma, lakini akapumzike salama

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Uteuzi wa Biswalo Mganga umeniumiza na kunikumbusha maumivu ya taifa hasa kwa wanaharakati, Wafanyabiashara, na yeyote aliyekuwa kinyume na utawala wa Mwendazake, Biswalo alikuwa mkono imara wa mateso ya Watanzania, huyu alikuwa wino halisi wa kitabu cheusi cha utawala uliopita. Biswalo ni roho halisi ya Magufuli katika ulimi wa moto uliokata na kusaga, Biswalo ni silahala hatari ya maangamizi iliyotelekezwa na hayati Magufuli. Biswalo alitakiwa kuwa jela muda huu sio katika ofisi ya umma. Lakini tumtakie utumishi mwema.

Uteuzi huu umenifanya nikumbuke vizuri Kesi 6, alizonifungulia Biswalo Mganga ambazo kwanza ilianzia kwa Hakimu Mh Mkea na kufia palepale aliponipa ushindi na kuionya jamhuri iache kuleta kesi za kijinga isizo na ushahidi nazo, baada ya hapo Biswalo akarudi kwa nguvu na kunifungulia mbili kwa mpigo kwa mahakimu tofauti tofauti, Kesi ya Pili ilianzia kwa Mh Mwijage, kesi ya Tatu ikaanzia kwa Mh Mashauri, Kesi ya Nne ikaanzia kwa Mh Kimario, Kesi ya Tano ikaanzia kwa Mh Mwambapa, Kesi ya Sita ikaanzia kwa Mh Kasonde. Lakini tumtakie utumishi mwema.

Kesi tano zote nilishinda, lakini kesi ya sita ilitembea kwa mahakimu 8 hadi ikaja kutua kwa Hakimu Kasiani Matembele ambae alinifunga miaka mitatu jela ama kulipa fani ya Shilingi milioni tano, Watanzania kwa umoja wenu, mlinilipia fani nikarudi Mbutu kulima bamia nikiwa huru. Ilifika kipindi pale Kisutu kama unakwenda sokoni vile kwa siku unaingia kwa mahakimu wa tatu. Lakini tumtakie utumishi mwema.

Leo Biswalo amekuwa Jaji wa Mahakama Kuu, hili linaumiza sana na kukera, Mtu ambae taifa limetoa machozi ya chuki dhidi yake anatunukiwa Ujaji? Mtu aliyejaza watu katika magereza kwakuwapa kesi zinazoitwa Uhujumu uchumi ama Utakatishaji leo anakwenda kuwa mtoa haki, serious? Oooho aisee dunia duala. Lakini tumtakie utumishi mwema.

Nimepitia kuchungulia sheria kuona nini hasa kimejiri hadi akaondolewa Uendesha Mashitaka na kupandishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Utawala wa Hayati Magufuli ulikuwa waajabu sana, zilitungwa sheria za ajabu sana za kujilinda, awali katiba ya Nchi ilimlinda Rais pekee dhidi ya mashitaka. Kwakuwa Magufuli utawala ulikuwa wa mkono wa Chuma kwelikweli, akaamua kuwapa ulinzi wale aliowatumia kuendesha mkono wa chuma, ambao ni Spika wa Bunge, Jaji Mkuu, Majaji, na Mwendesha Mashitaka (DPP). Lakini tumtakie utumishi mwema.

Ili tujadili tuone kwa mapana kwanini Rais Samia hajamfuta kazi Biswalo, ni lazima tuliangalie suala hili kwa jicho la kisheria, tukijiridhisha kuwa kuna msingi wa kisheria juu ya Biswalo kwakuzingatia ushahidi wa sheria niliouweka hapo chini, kisha tujiridhishe kwamba Utawala wa Mama Samia ni wa Kisheria au wa Kiimla yaani wa Kimagufuligufuli?. Lakini tumtakie utumishi mwema!

Tukikubaliana kuwa Utawala wa Mama Samia ni wa Kisheria, basi kuna sura kuu tatu muhimu sana tunazotakiwa kuziangalia juu ya ishu ya DPP, Kwanza tuelewe kuwa Mwaka 2019, walipitisha sheria inayomlinda DPP (Biswalo) kwamba akishateuliwa na Rais haweza kuondolewa, isipokuwa, akishindwa kutimiza majukumu yake. (mf maradhi), akikiuka maadili (kuna mlolongo), Hadi atakapostaafu au kujiuzulu. Kiujumla DPP hawezi kutumbuliwa, kuna mlolongo mrefu sana ni sawa na CAG, Jaji au Gavana. Swali linaweza kuja sasa, Je Biswalo katumbuliwa? Jibu hapana hajatolewa isipokuwa kapandishwa utumishi, hata mshahara kiutumishi sasa umeongezeka Milioni mbili hivi. Lakini tumtakie utumishi mwema.

Ukiangalia Trent ya Utawala wa Rais kwa siku 30 za mwanzo, Kwamaoni yangu, Rais Mama Samia ameamua kujitofautisha na mtangulizi wake, yeye anaonekana anaamini kwenye utawala wa sheria, na hivyo kila jambo anataka kutenda kwa kufuata msingi wa sheria, hapa ndipo alipofungwa mikono na swala na Biswalo na hata swala la Ndugai kuvunja Katiba kwa kuendelea kukumbatia wabunge wasio na Chama. Kwa maoni yangu naona Mama ameamua atumie plan B, juu ya Biswalo na izingatiwe kuna plan B. anayoweza kuitumia kwa Ndugai pia. Rejea Katiba ya Tanzania Kifung. (Tusimstue Ndugai). Lakini tumtakie utumishi mwema.

Uteuzi wa Biswalo kinadaria (in theory) ni kupanda cheo, Lakini kivitendo (in practically) ni kufukuzwa, kuangushwa na kuondolewa kwenye mfumo wa pesa (ulaji). Option ya kumuondoa Biswalo kwenye mfumo haramu na dharimu aliyokuwepo kwakuangalia sheria hii waliyojitungia utawala uliopita HAKUNA zaidi ya kumpeleka Mahakama Kuu akajisomee magazeti tu huku akipishana na gari ya mshahara.

Nafikiri Rais angetaka kumuondoa ofisini bila njia hii ya kumpeleka mbele, angetakiwa kuunda jopo la kimaadili lenye mlolongo mrefu sana, hadi hatua za mwisho kuchukuliwa ingeweza kuchukua hata hadi miezi saba huko, sasa yanini kusumbuka na mtu ambae unaweza kwenda kumtundika pale juu akaendelea kukauka kama ndafu, ikiwa Humphrey Polepole katoka kuwa Mwenezi Taifa, katundikwa Bungeni, Bashiru katoka kuwa Katibu Mkuu Kiongozi katundikwa Bungeni. Lakini tumtakie utumishi mwema.

Na kwa muundo wa Mahakama sikuhizi ni kuwa kila jaji wa Mahakama Kuu anafanya kazi eneo alilopo, mfano Biswalo akipelekwa Kigoma Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu atakaa Kigoma kulala na kuamka na kushinda mahakamani pale Kigoma, tofauti na alipokuwa DPP alikuwa akizunguka kila kona ya nchi kwenye kesi zote tamutamu alikuwa hakosi. Lakini tumtakie utumishi mwema.

Sisi raia huku nje kwamacho tunaona Biswalo kaula kawa jaji, lakini ndani ya korido za mifumo ya hela Daslamu, Biswalo amepishana na gari ya mshahara, naamini toka moyoni Biswalo analia na kuomboleza, kwake hili ni pigo takatifu, naamini sasa anafunga na kuomba huku akitema mate kulia na kufukia kushoto akiomba siafu huku nyuma wasianze kumpekua hasa wakitilia shaka mabilioni aliyokusanya kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi na utakatishaji wengi kabla sheria ya kutwaa mali ya Plea Bargaining. Lakini tumtakie utumishi mwema.

Binafsi nimeumia na uteuzi huu lakini nilipoona hii sheria, nikaisoma, nikarudi kutafakari mwenendo wa Utawala wa Mama Samia kwa siku hizi 30 za mwanzo nikajiridhisha kuna utofauti mkubwa na utawala uliopita, huyu anachembe za utawala wa sheria, nikaona wazi Mama angefuata Utawala wa Magufuli, naamini angetaka kumuondoa yeyote katika uongozi wa nchi hii angemuonoa, Si Ndugai, si Biswalo si Jaji Mkuu wala yeyotez ni ishu ya nusu saa tu ama uandike barua mwenyewe kujiuzuru ama utenguliwe. Kwenye Utawala wa Magufuli ndio kwa mara ya kwanza tumeshuhudia Majaji wakijiuzuru Ujaji wenyewe, sie tukatema mate kulia, tukafukia kushoto. Lakini tumtakie utumishi mwema.

Nadhani bahati nzuri Mama ameamua kutawala kisheria, hili naona hata Ndugai ameligundua kuwa Mama haingilii mhimili wowote, anachoangalia ni uhuru wa kila mhimili kujiendesha. Kwa maoni yangu, siamini kama Mama anafurahia uvunjaji wa Katiba anaoufanya Ndugai, huenda mbeleni atatumia plan B, ambayo naiona wazi Ndugai anajivika Kitanzi taratibu. Lakini tumtakie utumishi mwema.

Na Yericko Nyerere

images (2).jpeg
IMG_20210512_230451.jpg
 
Du unaandika gazeti bila hata pwenti moja ya maana! Kweli kuna watu wana muda w
Umetoa uchambuzi wa kueleweka sana.. Next step (i hope hili litatokea)! Biswalo atapelekwa Sumbawanga kuwa jaji
Amepuyanga vilaza mna chemotaxis yaani mnajuana kwa vilemba vyenu haka kajamaa ka Nyerere fake kaongo sana kana matangopori hatari.
 
Tatizo wewe ni mkurupukaji soma hapa, halafu uone kama ushabiki wako una mantiki
 
Umetoa uchambuzi wa kueleweka sana.. Next step..(i hope hili litatokea)! Biswalo atapelekwa Sumbawanga kuwa jaji
Alishasema ataendeleza ya mwendazake pia yeye na mwendazake ni kitu kimoja maana yake ndio hio.
Hana jipya.
.Ripoti ya upigaji kimya
. Kutumia hela zetu kumnunulia gari mtu mwenye kuweza kujinunulia gari
.Kuyapa teuzi na kuyaaacha majitu ya hovyo yasiyostahili hata kuitwa mtumishi wa umma yenye kashfa za kuumiza watu.
.Akiwa mjumbe alisapoti katiba mpya kawa dereva kaitupa means alifata posho.
Aliyesema ccm wote ni SAwa hakukosea
.Tusitegemee jipya hapa kigogo was right.
 
Kwahiyo unataka kutuaminisha kwamba Sheria za kumlinda DDP ni Magufuli kazitunga na kuziweka ama zikikuwepo kuanzia mwanzo?
Ni ukweli kwamba hatukubali yanayo fanyika Sasa hivi kwasababu bado tuna mbembekeza mama na kumtizama kwa jicho la kumuomba teuzi na ndiyo maana hatuishi kujikombakomba kwake, aisee! Kama Sheria zikiwekwa na Magufuli kwani mama ailishndwa kuzitengua Sheria hizo,
 
Back
Top Bottom