Uteuzi wa Dkt. Emanuel Nchimbi kama mgombea mwenza urais wa CCM uchaguzi mkuu wa OCT.2025, ni wa kisayansi katika siasa za kisasa.

Uteuzi wa Dkt. Emanuel Nchimbi kama mgombea mwenza urais wa CCM uchaguzi mkuu wa OCT.2025, ni wa kisayansi katika siasa za kisasa.

kwahiyo ndio mijanaume ikaolewe na mijanaume yenzao huko?

ubeligiji ni nani kwanza kwenye bajeti ya Tz gentleman 🐒
Hao wanaume wanao olewa wanalipa kodi kwenye nchi zao , Tanzania inapewa msaada pesa hizo hizo za mashoga kuongeza kwenye bajeti zao
 
Jina la nchimbi limezoeleka sana ndani ya siasa za tanzania. Huyu ukimuweka wapambane na lissu anashindwa asubuhi tu. Huo ndio mzani wa siasa wa ukweli
 
Je, vipi kuhusu kuchaguliwa kwa Tundu Lissu kuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkuu?
niliahidi kutoa maelezo na ufafanuzi wa kina dhidi ya hilo, licha ya kua tayari nimesha lizungumzia kwa kifup kwamba,

ni mapema sana kwa mtaalamu mbobevu kama mimi kueleza hayo bila kukamilisha tafiti ninayoendelea nayo juu ya kwanini hasa imekua hivyo,
.Nitakapokamulisha,
basi nitakua kwenye nafasi nzuri zaid ya kueleza jambo hilo.

Hata hivyo,
hongera kwa wanaChadema wote kwa kutekeleza wajibu wa kidemokrasia kwa amani, licha ya kiwango kikubwa mno cha rushwa kushuhudiwa.

Pamoja na hayo,
ni muhimu zaid kujikita kwenye hoja mahususi mezani gentleman 🐒
 
Jina la nchimbi limezoeleka sana ndani ya siasa za tanzania. Huyu ukimuweka wapambane na lissu anashindwa asubuhi tu. Huo ndio mzani wa siasa wa ukweli
hakuna mazoe kwenye masuala muhimu kama uongozi wa kisiasa hasa wa kitaifa gentleman.

maelezo ya ziada ni porojo na story za pata potea tu 🐒
 
Hao wanaume wanao olewa wanalipa kodi kwenye nchi zao , Tanzania inapewa msaada pesa hizo hizo za mashoga kuongeza kwenye bajeti zao
dah,
ndio maana nawaonea huruma vijana wa kiume wa chama fulani kwasabb watapelekwa kuolewa huko kama sehemu ya kutafutiwa fursa za ajira ng'ambo, dah!

Inasikitisha sana, inafedhehesha sana 🐒
 
dah,
ndio maana nawaonea huruma vijana wa kiume wa chama fulani kwasabb watapelekwa kuolewa huko kama sehemu ya kutafutiwa fursa za ajira ng'ambo, dah!

Inasikitisha sana, inafedhehesha sana 🐒
Mbona watu wapo Ng’ambo kitambo tu wanatafuta maisha, nyie ccm endeleeni kupokea pesa za mashoga kuendesha nchi maana hamna uwezo wa kujitegemea
 
Kwanza umefanyika kimkakati, lakini pia umefanyika kwa muda muafaka kama surprise, lakini kwa kuzingatia sheria na katiba ya CCM, bila kuathiri kwa namna yoyote ile sheria na katiba ya nchi kuhusiana na masuala ya uteuzi wa wagombea uongozi na uchaguzi wenyewe.

Azimio la kumuidhinisha Dr Emmanuel Nchimbi kama mgombea mwenza wa urasi wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania, lilitolewa hadharani na mkutano mkuu maalumu wa CCM taifa, na kuidhinishwa kwa kauli moja za wajumbe wa mkutano mkuu huo maalumu, kwa uthibitisho wa kura za ndio za wajumbe wote wa mkutano mkuu wa Taifa waliohudhuria mkutano ule.

Aina na namna ya uteuzi wa Dr.Emanuel Nchimbi ulivyo fanyika, kwanza imedhibiti makundi ndani ya chama na kuifanya CCM kua moja, yenye nguvu na imara zaidi.
Lakini pia hili limedhihirsha umadhubuti wa CCM na thibitishia ulimwengu kwamba CCM ni jabali la siasa za Tanzania na Africa kwa ujumla.

Umadhubuti na umahiri wa Dr.Samia Suluhu Hassan kiutendaji, utampatia uzoefu na uthubutu wa kutosha Dr.Emmanuel Nchimbi kushika hatamu na dhamana ya uongozi wa kitaifa kwa wakati muafaka.

Kama ilivyo mipango ya maendeleo ya vipindi vifupi, vya kati na vipindi virefu, Chama Cha Mapinduzi CCM, kimetoa uelekeo wa uongozi wa kisiasa waTaifa letu kwa kipindi cha miaka 15 ijayo utakuaje.

Na mpango wa usimamizi wa maendeleo na mustakabali wa uongozi wa Taifa letu ni kwamba, 2025-2030 ni Dr.Samia Suluhu Hassan, na kisha kwa Neema na Baraka za Mungu 2030-2040 ni Dr. Emmanuel Nchimbi.

Una maoni gani my friends, ladies and gentlemen?🐒

Mungu Ibarki Tanzania
Mleteni tu huyo macho mlegezo ndio mtamjua vizuri. Hata mama kujifanya mjanja anaweza asimalize. Ulizeni rafu zake huko nyuma umoja wa vijana.
Hakika tunaenda kukabidhi nchi mikononi kwa wahuni. Ni wakati sasa kuangalia upinzani nani anaweza kuokoa jahazi. Wazalendo ni wakati wa kujipanga sasa.
 
Back
Top Bottom