Si ndio anavyopita na kugawa majiko kwenye ziara yake kwa mtindo wa sandakalawe, sasa kuna methodology hapo ya ku monitor tabia iwapo sample yenyewe anakutana nayo barabarani. Baada ya hapo anaenda kijiji kingine na waliopata majiko wanaendelea na maisha yao, can you call that a research au mtu anaropoka na kutuona wote hamnazo kama yeye.
Huko kwenye vituo vya mafuta Mwigulu anatakiwa astopishe hizo hela haraka mpaka aone strategic plan ya hiyo policy. Jana โMillard Ayoโ waliweka video ya kijana alieahidiwa kumpatia millioni 50 za mkopo wa kufungua kituo cha mafuta. Yaani kakutana nae barabarani tu na makopo yake ya mafuta a nauza. Hakun mafunzo ya awali kuwapa uwezo wa kuendesha biashara, hakuna coaching na usimamizi kuhakikisha vituo vina kuwa sustainable na mambo mengine mengi.
Hivi kweli ukutane na kijana tu barabarani unamuahidi 50 millioni chances are hajui ata distributor wa karibu yake yupo sehemu gani au ata gharama za kuletewa mafuta, hajui EWURA wakimuibukia wakikuta amechakachua adhabu yake and so forth; waziri ana ahidi watu kama hao 50 millioni kirahisi tu.
Mtu kama huyo kweli wa kusimamia majadiliano ya gas ambayo tushapigwa kama uwezo wenyewe wa waziri ndio huo. Na sasa hivi TANESCO wanajiingiza kwenye mikataba ya ovyo kwenye umeme.