Uteuzi wa Katibu Mkuu wa CCM kuwa Katibu Mkuu kiongozi wazua mjadala, Mnyika ajitokeza hadharani kuonyesha masikitiko yake

Mwal

Mwalimu wa chuo kikuu cha umma/ aliyefikia nafasi ya juu, huyo hatoshi kuwa afisa mwandamizi? Labda watusaidie mipaka ya hayo maneno ni kwa mtumishi aliyewahi kushika nafasi zipi
Alishatoka huko na pia uangalie kwa umakini mkubwa hasa suala la siasa.Katibu Mkuu wa Chama kuwa katibu mkuu Kiongozi kuna ukakasi fulani katika demokrasia ya vyama vingi na ukakasi huo unakua mkali zaidi tukitizama yaliyotokea katika chaguzi kuu mbili,serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.Kwa maoni yangu haina siha kwa Taifa (Nasikitikita kutamka hivyo na kama nilivyosikitika kuhusu bunge kurudi kuwa la Chama kimoja)
 
Kama hizi ndio hoja za CHADEMA siku hizi basi nikiri kusema hakuna umuhimu wa upinzani tena. Kama mtu ana sifa na vigezo vya kuteuliwa , hakuna namna kufanywa hivyo
Kile ni cheo cha kiutumishi wa uma, appointment zake zinapaswa zifuate huo mfumo. Sasa kumteua mtu wa chama kuja kuwa msimamizi wa viongozi wa uma, siyo sahihi, kumbuka chama kina mfumo wake. Kama ambavyo imekuwa kwa watangulizi wake, alipaswa atoke utumishi wa uma, na hasa kwenye Tume ya Maadili ya Utumishi wa uma.
 
Mdo chama yawalsa ndg ukae ukijua hilo. Km Act wanavyozitekeleza huko zanziber.
 
Hawa watu wanawa
Hao watu wanaweza jiongezea muda wa kukaa madarakan Wale mema ya nchi hatutakubali
 
Huyu mnyika ndio Bure kabisa. Sasa Alitaka Ateuliwe Yeye? Hajui chama kimachoongoza nchi ndio kina pewa nafasi ya kuteua Viongozi? Au anadhani Ccm itatekeleza Ilani ya chadema? Huu ndio ujinga wa kiwango cha juu kabisa kwa kiongozi mkubwa kama J J Mnyika kutokujua Protocol ya Serikali na chama.
 
Ndio katiba inavyosema?
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† CCM inajivunia sana watu duni kama wewe !
 
Dr Bashiru Ally Kakurwa bado ni mtumishi wa umma pamoja na kwamba ni katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi kwa kuwa bado anatambulika ni mhadhiri wa chuo kikuu cha UDSM (mpaka sasa bado hajajiuzuru wadhifa wa uhadhiri na katibu mkuu CCM) baada ya kuteuliwa hivi juzi kuwa katibu mkuu kiongozi (mkuu wa watumishi wa umma wote nchini na katibu wa baraza la mawaziri)
 
Umeokota wapi huu utopolo wako ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…