Uteuzi wa Kingunge Ngombare Mwiru kwenye bunge la katiba ni dhihaka kwa watanzania

Uteuzi wa Kingunge Ngombare Mwiru kwenye bunge la katiba ni dhihaka kwa watanzania

Wachawi wenzake wameula wa chuya wanadhani atakwenda kuwasemea wakati kwenye rasimu hakuna kipengere kinachoongelea habari za uchawi.Kingunge na wengine kama Bulembo wameteuliwa kwa ajili ya kwenda kupinga serekali 3 na kupigania serekali 2 ziendelee kuwepo hao ni wateule maalumu kwa ajili ya kuipigania CCM.
 
Wakuu hii ndo siri ya Mh. Kingunge kuteuliwa kuwa mjumbe wa bunge la katiba wale makuhadi wa siasa za chuki na uzushi sasa waseme tena.

SIRI ya uteuzi wa mkongwe wa siasa nchini, Kingunge Ngomale-Mwiru, kuingia kwenye Bunge Maalumu la Katiba imefichuka.

Habari ambazo gazeti hili limezipata, zilisema kuwa uteuzi wa mkongwe huyo wa siasa nchini umepitia katika Chama cha Watabibu wa Tiba Asili nchini (ATME).

Habari kutoka ndani ya chama hicho, zinasema kuwa wao wenyewe kwa matakwa yao walilipendekeza jina la mwanasiasa huyo wakiamini kwamba atawazungumzia mambo yanayowahusu ndani ya Bunge hilo linalotarajiwa kuanza Februari 18 mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Mratibu wa ATME taifa, Boniventura Mwalongo, chama cha waganga wa kienyeji kilipendekeza jina la Kingunge na kwa bahati nzuri ameteuliwa.

Alisema kuwa watu wanapaswa kufahamu kuwa Kingunge ni mlezi wa chama hicho tangu mwaka 1999 na hii imetokana na yeye kuwa mstari wa mbele kutetea tiba hiyo ambayo inapigwa vita na wamiliki wa hospitali.

Mwalongo alisema mwanasiasa huyu hata kipindi cha kwanza cha uongozi wa Rais Jakaya Kikwete alipoteuliwa kuwa mbunge, alihakikisha hoja za tiba asili zilipokuwa zikipenyezwa bungeni alikuwa mstari wa mbele kuziongelea tofauti na wabunge wengine.

Alisema walianza kufanya kazi na Kingunge tangu kipindi cha uongozi wa Rais Benjamin Mkapa, alipokuwa Wizara ya Serikali za Mitaa na mara nyingi walikuwa wakikutana naye kwenye mikutano yao kila walipomhitaji.

“Nakumbuka neno alilokuwa akipenda kulitumia ni kwamba sasa nakwenda kuzungumza na ‘wachawi’, akiwa anamaanisha sisi, na kipindi hicho watu walikuwa bado hawajajua thamani yao.

“Sasa kupitia chombo chako mwandishi naomba uueleweshe umma wa Watanzania kwamba Kingunge hajapendelewa na rais kama watu wanavyodhani, bali yeye ni mmoja wa watu walioteuliwa katika makundi maalumu kama rais alivyoagiza awali, hivyo wamuache mzee wa watu akafanye kazi,” alisema mtabibu huyo.

Mwenyekiti wa ATME, Simba Abrahaman Simba, alisema uteuzi wa Kingunge ulifanywa kwa kufuata katiba ya chama chao katika mkutano walioitisha baada ya Rais Kikwete kukaribisha orodha ya majina ya watu kutoka asasi za kiraia na taasisi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Simba, hata wakati wa kikao cha kumteua na kupeleka jina lake kwa Rais Kikwete, Kingunge mwenyewe hakuwepo, hivyo walimpigia simu kumuomba akubali pendekezo la chama hicho kumtaka awe mjunge kupitia kundi lao, jambo ambalo aliliafiki.

Alitaja majina mengine yaliyokuwa katika orodha ya watu waliowapeleka mbali na Kingunge kuwa ni Othman Shem, Richard Chinzepo, Sara Mwakibete, Zahra Mandemla, Heldgade Kiwasira na Baeatrice Madeyane.

Kama vile haitoshi, mwenyekiti huyo alisema hata siku majina ya wajumbe wa Bunge la Katiba yalipotangazwa, Kingunge hakuwa na taarifa hadi walipompigia simu kumfahamisha kwamba rais amemteua.

Juzi katika mkutano wake na waandishi wa habari, Jukwaa la Katiba Tanzania lilihoji uteuzi huo wa Kingunge, kupitia kundi la asasi za kiraia wakati hajawahi kuwa mwanachama wa asasi yoyote.

Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Jukwaa la Katiba, Hebroan Mwakagenda, alisema nafasi 20 walizokuwa wametengewa asasi za kiraia, majina matano ni ya wanasiasa na makada wa CCM.

Alitolea mfano kwa Kingunge, akisema ameingizwa kwenye kundi la asasi wakati hajawahi kuwa na asasi wala hawajawahi kumshuhudia hata kwenye msiba wa mwanaharakati mwenzao.

“Watuambie Kingunge wamemtoa wapi na asasi yake ilisajiliwa wapi na inaitwaje… mimi nimekuwa kwenye asasi kwa miaka 22, lakini sijawahi kumwona hata kwenye msiba wa mwanaharakati mwenzetu, sasa iweje leo hii aibukie kwenye kundi la asasi?” alihoji Mwakagenda.

Kingunge anena
Akizungumza kuhusiana na hilo, wakati alipokuwa akiagwa jana na watabibu hao, Kingunge alisema tangu awali alivyopigiwa simu na ATME alisita kukubali moja kwa moja akijua lazima kuna watu watasema sana kuhusu uteuzi wake.

Hata hivyo aliongeza kwamba baada ya kufikiria sana akaona kama atakataa waliomteua wasingejisikia vizuri na ndiyo maana aliamua kukubali ombi lao.

Kingunge alisema kelele za uteuzi wake katika mambo mbalimbali ya taifa ameshazizoea na kudai kwamba wanaomsema ni wale wanaojua moto wake pindi anapoamua kusimamia na kulitetea jambo flani.

Bunge la Katiba
Kuhusu Bunge la Katiba, mwanasiasa huyo alisema wajumbe wote watakaoingia wanatakiwa kwenda kutunga katiba bora na si katiba mpya kama inavyosemwa.

“Unajua kama ni katiba tayari tunayo siku nyingi, kinachotakiwa ni kuboresha yale mazuri yaliyopo, kuondoa upungufu na kuibua mambo mapya ambayo yatakuwa na faida kwa wananchi,” alisema.

Pia alitumia fursa hiyo kuwaonya wanasiasa au watu wanaodhani katiba inaenda kutungwa kwa ajili ya kuwatengenezea mazingira ya kuendelea kuwa madarakani au kwa wale wasio madarakani kuingia Ikulu.

“Hapa lazima wabunge walioteuliwa watulize kichwa kwelikweli, sio kwenda kusaidia kundi flani kwenda Ikulu au kuendelea kuwa madarakani, kwani mimi pamoja na kuwa CCM, siendi kuwaandikia wao katiba kwani inatakiwa iwe ya matabaka yote,” alisisitiza.

Tiba asili
Kingunge alisema Watanzania bado wamekuwa na dhana potofu kuhusu tiba mbadala na wengine kuifananisha na ushirikina.

Akitolea mfano alisema kwa nchi za Korea, Asia na India zote hizo zilipitiwa na wakoloni, lakini jambo la kwanza walipojikomboa kulishughulikia lilikuwa ni tiba za asili.

Alisema nchi hizo zimekuwa zikitumia tiba inayotokana na mimea na madini yanayopatikana nchini mwao, vitu ambavyo hata Tanzania tunavyo, lakini watu wamekuwa wakividharau.

Pia alisema ieleweke kwamba afya ya wananchi ni suala muhimu na la kwanza, hivyo ushiriki wa ATME umetambuliwa katika katiba kama njia mojawapo ya kuweka misingi ya utoaji tiba nchini.

Mtoa mada.
Kumbuka kuwa Katiba ni kwa kizazi cha sasa na badae.
Nimeona michango yako mingi hailengi kujenga.
Pia umeshindwa kutambua kuwa sio busara kwa mtu mwenye kundi fulani kuwakilisha kundi lingine.
Mfano tu, ungejisikiaje kama Mch Msigwa angewakilisha makundi ya dini, Mbowe angewakilisha wafanyabiashara, Lissu wanaharakati nk.
Please tumia akili kufikiri !
 
Nikisikia tu jina la Kingunge nahisi kichefuchefu!

Huyu mzee anatakiwa alee vijuku na vitukuu tu na sio kumpeleka bungeni!
 
hoja nyepesig.Mleta uzi unafanya sugar coating tu!
 
Huyu mzee naona ana kazi maalumu serekalini.Karibu awamu zote hajawahi kuachwa kuteuliwa kuwa kiongozi serekalini mpaka alipokuja kuomba mwenyewe.Hiyo kazi inaonekana hata mungu haipendi ndiyo maana hana dini.
 
Haka kazee kwanza kabisa haki amini kuwa Mungu yupo kinaamini uchawi na makafara tu lakini kilivyolazwa muhimbili kiliomba tukiombee kwa Mungu Hiki kidingi ni janga la taifa
Ni kweli kwa huyu aliyeteua anathamini mchango wa Waganga wa kienyeji kuliko wa Wapentekoste??
 
Kingnge + profesa maji marefu naona mbungeni giza zito litatawala.
 
ulitaka ateuliwe slaa?

Inathibitisha upuuzi uliokujaa na sio hoja mujarabu??!! Unafahamu bunge la katiba limejaa zaidi 78% ya makada wa CCM??! Na unajua wazi kabisa mapendekezo mengi CCM hamyataki ila mna yenu so kweli hapo kuna katiba ya maslahi ya nchi????!!
 
Hilo bunge la katiba halitaisha bila kutokea jambo kubwa litakaloshtua wengi
 
Hakuna haka ya jaziba, tz pamoja Kuwa Islam 32%, Catholic 38%, Pentecost churches 17% ina 13% ya wapagani akiwemo Mheshimiwa sana Kingunge, lakini niwaombe wachangiaji fafahamu kwamba wananchi wake 93% wanaamini uchawi na kwa wale wasio na habari Tz ni ya 2 Africa ushindi Hu wa kichawi ulipandishwa chati na mchungaji feki Mwasapile aliyewagiribu mpaka viongozi wa Nchi wakaenda kunywa maji ya kipepo. Idadi kubwa ya wawakilishi wetu katika vyombo vya maamuzi ni washirikina, ndio maana unaweza kuona hakuna anayejiuliza kuhusiana na na ndoa ya Tz na Madragon China wanaoamini dini ya mashetani. Kingunge anawakiliaha kindi kubwa sana, ni basi tu kwamba mambo yao si rasmi kikatiba vinginevyo walipaswa wapewe nafasi nyingi zaidi. Hata hivyo hakuna shida kwa sababu wanna uwezo wa kushiriki bila kushirikishwa. Mungu ihurumie Tz.
 
kumekuwa na upotoshaji kuhusu uwakilishi wa kingunge ngombale mwiru katika bunge la katiba kwa ufupi kingunge anawakilisha watu wasio waislamu wala wakristo ,watu wanaoabudu dini za asili over
 
Yani hata sauti ya Ndiooooooooooo hawezi toa yani hana mchango kwa saiz kwa kweli. kama ni ela si wampe tu wanamchosha mzee wetu, uonevu tu
 
Ni dhahiri kwamba J.K. anajaribu kumsaidia Kingunge apate ulaji kidogo!!!!! Hizo TSh. 700,000X90= TSh 63milioni zitamsaidia kwa muda.

Ahsante J.K. kwa huruma yako kwa mzee wetu. Wahurumie wazee wengine basi. Tutakuenzi.
 
Wakati nipotambua kwamba Rais JK amemteua huyu babu kingunge kwenye bunge la katiba hakika nilishangaa sana. Mshangao wangu ulitokana na kurudisha kumbukumbu zangu nyuma kidogo wakat JK alipompumzisha huyu babu ktk uongoz (ubunge wa kuteuliwa) kwa madai kwamba anapaswa kupumzika amelitumikia taifa kwa muda mrefu sana na nguv zimemwishia.

Je leo hii babu Kingunge kikongwe huyu ana jipya gan atakalotoa ktk bunge la katiba zaid ya kwenda kulala bungen au kutoa michango ya kihafidhina? Nina mashaka sana na uteuzi wa kingunge. Wadau nisaidien.

Mshangae zaidi aliyemteuwa
 
Huyu mzee naona ana kazi maalumu serekalini.Karibu awamu zote hajawahi kuachwa kuteuliwa kuwa kiongozi serekalini mpaka alipokuja kuomba mwenyewe.Hiyo kazi inaonekana hata mungu haipendi ndiyo maana hana dini.

Huyu mzee ndiye alikuwa akisaidia kuzuia Makombora yale yaliyokuwa yanamlenga Jei kei enzi za kampeni alivyokuwa akidondoka dondoka hovyo majukwani.
 
Huyu kingunge kwanza afya yake mgogoro kwa uzee hiv kwel ataweza kukaa muda wote wa bunge akiwa imara kufatilia mambo na hoja imara za kulipeleka taifa hatua nyingine ya kupata katiba mpya? Ni afadhali angepewa ile shuhuli yake ya awali ya"MSHAURI WA RAIS" kuliko ktka bunge la katiba. Hata hao waganga wa jad (wachawi) waliompendekeza nao hamnazo hata kama anaenda kutete wachaw hakika wamepoteza nafas kwasabab Hamna jipya kichwan mwa Babu yetu huyu ni mzee sana amechoka apumzike.
 
kumbe huwa kana maufundi, hii noma maana wanaamini point zake za kuwabeba zinaweza kupita tu.
 
Back
Top Bottom