Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa TISS, Said H. Masoro, na Mtazamo wangu

Wabongo Sasa hivi mnapenda credit uchwara.

Huyo ameteuliwa kama Marais wengine walivyoteua huko nyuma. Hakuna jipya.
 
Huu ni mtazamo wako, ngoja tusubiri na mtazamo wa mkongwe Pascal Mayalla ili kujua na yeye atakuja na mtazamo gani kuhusu mkuu huyu wa idara nyeti.

Hakuna mzee mwenye mtazamo tofauti na uliomkuza. Yeye anaamini CCM itatawala milele. Mtu kama huyo hana mtazamo tofauti na huo. Sana sana ataishia kuleta porojo.
 
Dahh . Ila we jamaa unaandika ww!!🤣🤣🤣
 
Nimesema ni kazi yao mojawapo. Hakuna nchi inatenganisha intelligence services na uchumi.
Kwani kipi hakihitaji uongozi na mfumo mzuri wa kisiasa, ni michezo, utalii au nini. Au kipi hakihitaji wasomi nguli wa fani hiyo kupewa uhuru wa kutimiza majukumu, tuseme afya, elimu au jeshi. Au kitu gani TISS ikiwa strong kinaharibika. Kwanza TISS haifanyi kazi yoyote ikiwa yenyewe bali inasaidiana na wizara au taasisi nyingine, kama kuna kesi ya rushwa TAKUKURU watahusika, kama kuna taarifa za kijasusi juu ya mgeni fulani mwenye hatari Uhamiaji watahusika. Sasa iweje unataka tuitenge na uchumi.

"An intelligence agency is a government agency responsible for the collection, analysis, and exploitation of information in support of law enforcement, national security, military, public safety, and [foreign policy objectives]"

Hizo foreign policy objectives hata uchumi upo, kama mfano tunataka kuwa vinara kwenye biashara ya korosho, tunataka kuwa soko la chai Afrika Mashariki hizo ni agenda ambazo intelligence agency inatakiwa ihusike.

Mojawapo ya kazi ni "Covertly influence the outcome of events in favor of national interests, or influence international security".
Hiyo influence in favour of national interests hata uchumi unahusika. Unless useme kama Tanzania haina mpango wowote kiuchumi inazubaa tu.
 
Hujui ukisemacho Mkuu.Ndani ya TISS kuna Dawati la Uchumi unadhani linafanyakazi gani? Hivyo hivyo BCI ya Polisi kuna dawati la uchumi.
 

Hakuna uchumi bila ujasusi.

Uongozi mzuri unapatikanaje?
Au unafikiri vitu vizuri vinapatikana kienyeji?

Kama ulivyosema moja ya Malengo makuu ya ujasusi ni ishu za ulinzi na usalama.
Sasa sijui unaelewaje kuhusu Ulinzi na usalama.

Ulinzi na usalama unajumuisha mfumo mzima wa Maisha ya binadamu,
Masuala ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni n.k.

Sasa utawezaje kuwa na ulinzi na usalama katika uchumi bila ya ujasusi?
Utawezaje kuwa na ulinzi na usalama katika utamaduni pasipo ujasusi?

Hakuna Uongozi mzuri au Maendeleo ya uchumi pasipo ujasusi.
Kama wewe ni mfanyabiashara mkubwa huwezi kuwa mfanyabiashara mkubwa pasipo ujasusi.
 

Huyo anafikiri ujasusi kazi yake ni mambo ya upolisi Polisi pekee.
Hapo ndipo anapokwama,
 
Nchi ikitaka kuwa kinara wa korosho, chai, tumbaku au bidhaa nyingine yoyote katika masoko ya nchi nyingine kinachotakiwa ni kuzalisha na kufikisha bidhaa bora zinazokidhi hayo masoko kwa gharama za chini kuliko wazalishaji wengine, sera nzuri za biashara na kodi ambazo zina support biashara za kimataifa na mahusiano mazuri ya kidiplomasia kati ya nchi. Huhitaji TISS au chombo cha ujasusi kufanikisha haya, ni mambo basics kabisa. Labda kama taifa linataka kupora uranium au mafuta kutoka taifa lingine au kuuza silaha ndio litahitaji majasusi rogue wanaofadhiliwa na corporations katika uhalifu huo.
 
DGIS mpya Ndugu Said Masoro si mtu maarufu katika korido za Ujasusi Dar es Salaam ukimlinganisha na mtangulizi wake Athuman Diwani ambae umaarufu wake ulijengwa akiwa Intelijensia ya Polisi, DCI na katibu Tawala, Masoro anaweza kuwa chachu ya magezi ya chombo hiki muhimu na uti wa mgongo wa taifa letu ikiwa hataruhusu kumezwa na siasa chafu za Dar na Dodoma.
 
Kwa kifupi elewa hivi Kazi kuu ya ujasusi ni kusaidiq kuweka mazingira salama ya raia kufanya maisha yao kwa ufanisi, iwe biashara au jambo lingine lolote, sio kazi ya taasisi za ujasusi kutuoa muelekeo wa uchumi, kuelekeza au kuingilia jinsi uchumi wa nchi unavyopaswa kwenda. Hii ni kazi ya wanasiasa viongozi na watunga sera.
Kufikiria kwamba taasisi ya ujasusi inaweza kuwa mwarobaini katika kuukwamua uchumi wa nchi ndio kituko kikubwa zaidi.

Zipo models nyingi za maendeleo duniani ila hakuna hata model moja ya maendeleo ya uchumi kutokana na nguvu ya spy agency.
 

Upo sahihi Kabisa.

Hata uongozi Bora pekee sio mwarobaini as kuikwamua nchi kiuchumi.
Siku zote mambo yanategemeana
 
Hahaha kasome tanzania intelligence and security service Act 1996. Ujue kazi za hii idara ni nn... Nandomana Kuna kitengo kinaitwa FIU(financial intelligence unit) Kipo BOT kama left wing ya TISS na uzijue kazi za hii FIU hasa ni nn

Sent from my 701SO using JamiiForums mobile app
 
Kudos 👌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…