Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa TISS, Said H. Masoro, na Mtazamo wangu

Ujasusi wa kiuchumi ni muhimu na hujumlisha sayansi na diplomasia ya uchumi na statecraft.
 
Usalama wa nchi siyo bunduki tu. Hata pesa ikikosa thamani au biashara za ndani na nje zikadorola na hilo ni tishio la usalama
 
Hakuna mzee mwenye mtazamo tofauti na uliomkuza. Yeye anaamini CCM itatawala milele. Mtu kama huyo hana mtazamo tofauti na huo. Sana sana ataishia kuleta porojo.
Tindo umeathiriwa sana na propaganda za uvyama mpaka inafikia mahala watu wakijadili mpira wewe unaingiza uvyama, wakijadili mziki wewe unaingiza uvyama, wakijadili mambo mengine ya taifa vilevile unakimbilia kuingiza uvyama.

Kwa aina hii ya maisha unayoishi, usipokuwa makini ipo siku utakuja kujiuwa kisa chama chako kimeshindwa uchaguzi fulani, afu wale walioshindwa kwenye chama chako husika wakiendelea na maisha yao ya kula bata.

Hii inanikumbusha baba yangu mdogo fulani (ambae sasa ashafariki) alitakaga kuchoma nyumba yake mwenyewe na yeye mwenyewe akiwa ndani, kisa team yake ya Simba imefungwa na Yanga miaka ya 90.
Isingekuwa watu kuwahi kuuzima moto na kuvunja mlango ili wamtoe, jamaa angekuwa amewahi kujiuwa kabla ya muda wake wa kufa haujafika. Wakati huo huo viongozi wa team ya Simba na wachezaji wao walikuwa wanaendelea na maisha yao ya kula bata bila kujali kufungwa kwao.
Hili ninalokwambia ulitafakari, bila hivyo kwa aina hii ya wanasiasa wetu wa bongo waliojaa janja janja ya kupiga pesa za umma, au kulamba asali ili kujiandalia maisha yao na ya vizazi vyao kuna siku utakuja kuumia, au kupata ugonjwa wa moyo ambao haukuwa nao before.

Lazima ujue kuna maisha nje ya siasa na mtu ukaishi vizuri tu bila presha wala shutuma kwa mtu mungine.
 
Kitengo kilicho BoT ni kitengo chini ya BoT sio chini ya TISS. JWTZ wote wana kitengo cha Military Intelligence, polisi wana kitengo chao cha uchunguzi, mamlaka ya kuzuia dawa za kulevya wana kitengo cha cha upelelezi na ufuatialiji, hata Immigration wanaweza kuwa na kitengo cha cha uchunguzi n.k hivi vitengo vyote viko chini ya hizo taasisi zao kutimiza wajibu wa taasisi zao.
Sio kila kitengo cha uchunguzi katika idara ya serikali ni cha TISS, kwa makusudi au bahati mbaya nchi nyingi tofauti na za magharibi huwa wanapenda kuona muundo, miongozo na namna ya utendaji wa vyombo vya ujasusi unabaki gizani na hii imezifanya hizi taasisi kutoelewaka zinaanzia au kuishia wapi.
 
Ata ktk mabenki ya kawaida ya kibiashara zipo hizo unit
 
Jibidiishe kusoma maandiko mbali mbali utaelewa na Kukubaliana na mtoa uzi.

Idara Ya Usalama wa Taifa ina cover almost sector zote ambazo zinafanya Ustawi wa Taifa na zinazochangia Maendeleo na au "Stability" ya Taifa.
 
You said it all Mkuu! [emoji122][emoji122][emoji122]
 
Jibidiishe kusoma maandiko mbali mbali utaelewa na Kukubaliana na mtoa uzi.

Idara Ya Usalama wa Taifa ina cover almost sector zote ambazo zinafanya Ustawi wa Taifa na zinazochangia Maendeleo na au "Stability" ya Taifa.
Lengo mama ni nini?

Lengo la kuanzishwa polisi?
Lengo lq kuanzishwa TRA
Lengo la kuanzishwa takukuru
Lengo la kuanzisha jwtz
Lengo la kuanzisha zomamoto
Lengo la kuanzisha tamisemi

Lengo kuu kabla ya kwenda kwenye malengo ya ziada
 
Punguza Ubishi ndugu, be sober!
 
Ni ngumu kumeza Mzee !! Bandiko lote linaanzia na kuishia pale ulipoeleza Tanu youth league na Uvccm !! Iko hivi kwa maoni yangu huo mfumo uliwekwa makusudi kukilinda chama kinachotawala tangu Uhuru mpaka leo hii ni chama hicho hicho ndicho kiko madarakani au niseme ni vyama ndugu hivyo hivyo!! Sasa ngumu kumeza ni kwamba unategemea nani anaweza kubadili hali hiyo kama ulivyoshauri ?!! Jibu litakuwa ni Katiba mpya ! Sawa lakini up to now who is holding the four aces katika kuibadili hiyo katiba ili irekebishe yale ambayo umeona hayako sawa kwa mustakabali mpana wa Taifa letu ??!! Who is holding the four aces ndio swali kuu. !! Sorry huo ni mtazamo wangu tu !!
 
Wee bhana unapromote kitabu chako tu. We una mafunzo gani kitaalam ya ujasusi kama sio ubabaishaji tu? Usifikiri hadidhi ya kitabu ni sawa na hali halisi.
 
Kiukweli Bwana Yericko lazima nikupe hongera kwa kuandika kitabu maana kuandika kitabu siyo mchezo. Lakini kwa sababu kitabu chako hukuandika kama matokeo ya utafiti kwa ajili ya taaluma, maelezo yako hayajasanifiwa (hayana peer review ya wataalam wa somo hilo). Kwa hiyo kitabu chako ni kama barua kwa wasomaji. Hii haina ubaya wo wote ila tu usitegemee kitabu kitumike kufanya mabadiliko makubwa.
Kwanza, suala la Usalama, ni suala la utawala. Kwa bahati mbaya sheria hiyo ilipotungwa uwezo unaotokana na uzoefu wa kiutawala katika ngazi za juu sana ulikuwa umeshatutoka. Pili, baada ya Siasa ya Vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992, malengo ya kitaifa ya muda mrefu hayapewi kipaumbele na unajua suala la Usalama wa Taifa linahusu mstakabali waTaifa; ni la muda mrefu, si suala la kushinda uchaguzi ujao. Tatu, Usalama wa Taifa unahusu kuwa na mipango, mbinu za muda mrefu za, kulinda, kudumisha na ustawi wa nchi na watu wake. Sasa mambo muhimu hapo ni mengi: mipaka, afya ya jamii, elimu na vipaji vya jamii, sayansi na kuangalia masuala ya sasa yatakavyoathiri Taifa baadaye na kupendekeza mikakati. Nne, utaona hapo kuwa kila nchi usalama wake utatokana na historia ya nchi na taifa lilivyozuka, umakini wa watawala kuhusu mustakabali wa Taifa na uwezekano wa kuwa na uongozi, uendeshaji na zana ambazo ni zaidi ya wastani wa Taifa katika Idara yenyewe. Mwisho, itategemea hao viongozi wa kisiasa wa awamu mbalimbali wamejaliwa vipi katika kuelewa na kutambua masuala haya ya muda mrefu.
Kwa hiyo uchumi ni kipengele kimoja cha kati. IQ ya Mtanzania inashuka au inapanda pengine ndiyo suala la kwanza; na kama haipandi sababu ni nini? lishe, elimu, uongozi au hujuma!?
 
TISS inabidi iwe na uwezo wa kupata wapi la kupata ujuzi wa kutengeneza injini kwa namna yoyote ile. Ndio vitu duniani wanafanya, China mara nyingi tu unasikia wameiba TB za data kuhusu kitu fulani. Survival of the fittest

China waliendelea kwa mageuzi makubwa ya uchumi wao na uongozi imara. China haijaendelea kwa kuiba teknolojia za Magharibi bali imeanza tabia za wizi wa teknolojia za biasahara baada kupata maendeleo makubwa.
Njia bora ya kupata maendeleo makubwa ni kutengeneza mazingira mazuri ya kuchochea innovations, ku-retain na kuvutia talents badala ya kufikiria wizi wa teknolojia ambazo hata mkipewa bure kabisa hamtaweza kuzifanyia chochote cha maana.
Kenya inakuwa kituo kikubwa cha teknolojia mbalimbali Africa Mashariki sio kwa sababu ya ujasusi bali kwa sababu ya elimu, sera na mazingira ya biashara yanayovutia innovation na uwekezaji wa teknolojia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…