mose
JF-Expert Member
- Jun 5, 2009
- 422
- 395
SAHIHI.Kiukweli Bwana Yericko lazima nikupe hongera kwa kuandika kitabu maana kuandika kitabu siyo mchezo. Lakini kwa sababu kitabu chako hukuandika kama matokeo ya utafiti kwa ajili ya taaluma, maelezo yako hayajasanifiwa (hayana peer review ya wataalam wa somo hilo). Kwa hiyo kitabu chako ni kama barua kwa wasomaji. Hii haina ubaya wo wote ila tu usitegemee kitabu kitumike kufanya mabadiliko makubwa.
Kwanza, suala la Usalama, ni suala la utawala. Kwa bahati mbaya sheria hiyo ilipotungwa uwezo unaotokana na uzoefu wa kiutawala katika ngazi za juu sana ulikuwa umeshatutoka. Pili, baada ya Siasa ya Vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992, malengo ya kitaifa ya muda mrefu hayapewi kipaumbele na unajua suala la Usalama wa Taifa linahusu mstakabali waTaifa; ni la muda mrefu, si suala la kushinda uchaguzi ujao. Tatu, Usalama wa Taifa unahusu kuwa na mipango, mbinu za muda mrefu za, kulinda, kudumisha na ustawi wa nchi na watu wake. Sasa mambo muhimu hapo ni mengi: mipaka, afya ya jamii, elimu na vipaji vya jamii, sayansi na kuangalia masuala ya sasa yatakavyoathiri Taifa baadaye na kupendekeza mikakati. Nne, utaona hapo kuwa kila nchi usalama wake utatokana na historia ya nchi na taifa lilivyozuka, umakini wa watawala kuhusu mustakabali wa Taifa na uwezekano wa kuwa na uongozi, uendeshaji na zana ambazo ni zaidi ya wastani wa Taifa katika Idara yenyewe. Mwisho, itategemea hao viongozi wa kisiasa wa awamu mbalimbali wamejaliwa vipi katika kuelewa na kutambua masuala haya ya muda mrefu.
Kwa hiyo uchumi ni kipengele kimoja cha kati. IQ ya Mtanzania inashuka au inapanda pengine ndiyo suala la kwanza; na kama haipandi sababu ni nini? lishe, elimu, uongozi au hujuma!?
Na >'jicho la kuona kote na mote'< ni kitu chenye nasibu ya 'kucheza Mungu'...
Ndiyo maana taasisi zote za namna hii duniani huvutia watu wema na wabaya; na wetu wengi wangalipenda kuwa taasisini kwa ajili ya 'mambo ya upendeleo' kwa wale watu walio nyuma ya pazia...
Siku za mbele, ushamba wa 'usiri wa mambo' na 'siasa za nyuma ya pazia' vitakoma. Kuna mambo yamekuwa ni sanaa na taaluma za >'Taasisi Jicho--Taasisi Mwewe'<--vile kuona mapana na vipenyo kana vile kutoka juu, isivyo wa wengi walio tambarareni; tena juu ya sera za nchi zenye kutawala uhai wa taifa, yatakuwa maarifa ya kawaida ya kila mtu, kila raia, kila 'mja mwema'...
Tupo kwenye >zama mpya< ya maendelo na hatua za kibinadamu ambamo 'tabia za kishirika' zenye kufanyakazi na kustawi kwa 'sanaa na usiri/siri' zitakuwa si zenye 'manufaa' ya ukweli ila 'mning'inio' wa vilevi vya kizamani...
Kwa hivyo ni kweli, suala la maendeleo yakweli na bora--pia makusudi kwa stawi za mapana ya jamii ni hitaji kwa dhamira ya dhati katika kujipambanua kutoka kwenye 'siasa za tawala' kuelekea kwenye 'uongozi wa kweli' wa jamii...
Amerika, Merekani, wametaasisha idara zao za uono mifumo kwa alama ya >'Tai' na 'Nyota'<, lakini hiyo ni duru ya kwanza ya uhai wa mjumuiko wa 'taasisi ya akili-dola' kujihami na mataifa mengine yenye kustawi--na kila baada ya mapana fulani ya maendeleo na ustawi, wao huongeza idara...
Afrika bado kidogo taasisi-jicho zetu zinaushamba wa kuiga na kuzuga; hili linakwenda kubadilika siku za usoni.
Kwa hiyo tuzungumze na kujadili juu ya mifumo na huku tukitafuta kuelimishana zaidi, na basi mengi yanaweza kubayanishwa na kuleta chachu ya mageuzi--na mageuzi yana kitovu cha utashi, pia ushawishi, kote kote katika umma na pia watawala...
Kwa muktadha huu, jambo adhimu linalosubiri ni utashi wa umma juu ya mifumo, na kwa watawala-- hitaji kwa maarifa sahihi na upeo kwa 'machaguo ya kitaasisi' yaliyobora katika kujinasibu na mageuzi ya kijamii kwa kupitia 'fanusi-jamii' za namna mpya...
Pasipo taasisi imara za jicho--zenye kukomaa na 'kumbukumbu/uzoefu' na tena upeo na maarifa ya nyongeza kwa sura na mienendo ya jamii, tutaishi na kadiri ya >watawala na si viongozi<... Basi, taasisi jicho zinahitaji 'kuzaliwa upya' ili zisiishie tu kuwa 'mikondo ya taarifa-kisogo' kwa ajili mifumo mibovu ya tawala na utumishi...
Hii inawezekana kupitia jitihada sahihi za >ELIMU 2.0 na ELIMU 3.0<