Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa TISS, Said H. Masoro, na Mtazamo wangu

Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa TISS, Said H. Masoro, na Mtazamo wangu

Tindo umeathiriwa sana na propaganda za uvyama mpaka inafikia mahala watu wakijadili mpira wewe unaingiza uvyama, wakijadili mziki wewe unaingiza uvyama, wakijadili mambo mengine ya taifa vilevile unakimbilia kuingiza uvyama.

Kwa aina hii ya maisha unayoishi, usipokuwa makini ipo siku utakuja kujiuwa kisa chama chako kimeshindwa uchaguzi fulani, afu wale walioshindwa kwenye chama chako husika wakiendelea na maisha yao ya kula bata.

Hii inanikumbusha baba yangu mdogo fulani (ambae sasa ashafariki) alitakaga kuchoma nyumba yake mwenyewe na yeye mwenyewe akiwa ndani, kisa team yake ya Simba imefungwa na Yanga miaka ya 90.
Isingekuwa watu kuwahi kuuzima moto na kuvunja mlango ili wamtoe, jamaa angekuwa amewahi kujiuwa kabla ya muda wake wa kufa haujafika. Wakati huo huo viongozi wa team ya Simba na wachezaji wao walikuwa wanaendelea na maisha yao ya kula bata bila kujali kufungwa kwao.
Hili ninalokwambia ulitafakari, bila hivyo kwa aina hii ya wanasiasa wetu wa bongo waliojaa janja janja ya kupiga pesa za umma, au kulamba asali ili kujiandalia maisha yao na ya vizazi vyao kuna siku utakuja kuumia, au kupata ugonjwa wa moyo ambao haukuwa nao before.

Lazima ujue kuna maisha nje ya siasa na mtu ukaishi vizuri tu bila presha wala shutuma kwa mtu mungine.
Well said mkuu
 
Nilitegemea kuona cv yake mteule huyo. Mwisho nimeambulia tangazo la kitabu cha Ujasusi wa kidola.
Bandiko si baya lakini limehama kuwa tangazo la biashara. Labda wale wanao comment ndio wanajaribu kuongelea vitu sio mtu
 
Hiki ulichoandika hapa sio kazi kuu za Idara za Usalama wa Taifa/Ujasusi duniani. Kazi za majususi ni ulinzi na usalama wa nchi masuala ya uchumi na biashara yataingizwa huko katika majuku yao kama ni kitisho cha usalama wa nchi zao au kama yataleta matokeo fulani kiusalama.

Hizi kazi za uchumi na biashara katika nchi ni kazi kuu za Wizara ya Fedha na Benki Kuu.
Loh! Naona uko mbali na Dunia ndg yangu. Ujasusi ni kila kitu. Vipi unautoa uchumi katika ujasusi. Kama unaelewa concept ya pro- activity basi hawa ndo wanatakiwa wawe hivyo. Wanayaona mambo yote katika broader view na kushauri other bodies, the government for that matter. Umenifahamu?
Kwa taarifa yako uchumi ndiyo usalama wenyewe!

,
 
TISS na Jeshi hawawezi kuukwamua uchumi wetu, hakuna maendeleo yoyote duniani ya kiuchumi yamepatikana kwa njia hii.
Huo wizi ulioiutaja hapa hauhusiani na uchumi. Maendeleo ya uchumi yanahitaji uongozi na mfumo mzuri wa kisiasa pamoja wachumi nguli wanaopewa uhuru kutimiza majukumu yao.
Chombo chochote cha ulinzi/usalama ili kiwe na weledi na ufanisi katika kazi yake lazima kiwe na watu wenye weledi kwenye fani zote, wahandisi, madaktari, mafundi mchundo, wahasibu, ICT, wauguzi nk nk. ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi na weledi hadi kifikie malengo kwa ustawi wa taifa na watu wake.

Vv
 
Nimesema ni kazi yao mojawapo. Hakuna nchi inatenganisha intelligence services na uchumi.
Kwani kipi hakihitaji uongozi na mfumo mzuri wa kisiasa, ni michezo, utalii au nini. Au kipi hakihitaji wasomi nguli wa fani hiyo kupewa uhuru wa kutimiza majukumu, tuseme afya, elimu au jeshi. Au kitu gani TISS ikiwa strong kinaharibika. Kwanza TISS haifanyi kazi yoyote ikiwa yenyewe bali inasaidiana na wizara au taasisi nyingine, kama kuna kesi ya rushwa TAKUKURU watahusika, kama kuna taarifa za kijasusi juu ya mgeni fulani mwenye hatari Uhamiaji watahusika. Sasa iweje unataka tuitenge na uchumi.

"An intelligence agency is a government agency responsible for the collection, analysis, and exploitation of information in support of law enforcement, national security, military, public safety, and [foreign policy objectives]"

Hizo foreign policy objectives hata uchumi upo, kama mfano tunataka kuwa vinara kwenye biashara ya korosho, tunataka kuwa soko la chai Afrika Mashariki hizo ni agenda ambazo intelligence agency inatakiwa ihusike.

Mojawapo ya kazi ni "Covertly influence the outcome of events in favor of national interests, or influence international security".
Hiyo influence in favour of national interests hata uchumi unahusika. Unless useme kama Tanzania haina mpango wowote kiuchumi inazubaa tu.
Unajuwa tatizo letu ni kuwa tunaposikia usalama wa taifa tunakimbilia kwenye makosa yanayohusu mambo ya serkali, siasa, na viongozi wake. Tunasahau kuwa usalama ni totality ya uhai wa nchi katika kila nyanja. Raia aliye na njaa sia salama. Raia mgonjwa siyo salama. Uchumi mbovu siyo salama, n.k. Hii ndiyo maana usalama wa taifa unatakiwa kuwa na wabobezi katika nyanja zote. Popote TZ usalama ni muhimu.
 
Alichoandika sio kazi kuu ya usalama wa taifa, ila ni kazi mojawapo. Mambo mengine yanafanyika, ulinzi na usalama wanafanya bado ujasusi wa kiuchumi.
Hao unaosema BoT na Finance hawawezi kufanya crandestine operations.

Wasovieti walioiba blueprints za atomic bomb kutoka Los Alamos pale Marekani sio wanasayansi wala watumishi wa jeshi, serikali ya Stalin ingeamua kusubiri jopo la wanasayansi lifanye testing na kila kitu wangetumia gharama kubwa mno na muda mwingi zaidi kupata breakthrough.

Wamarekani walioiba Lunik ya USSR ikiwa kwenye world tour hawakuwa wanasayansi wa NASA, walipiga picha na kukamilisha kazi yao kisha NASA wakatumia hizo taarifa.

Basically TISS isingekuwa na maana kama haitakiwi kufanya kazi fulani maana kila kazi ina wizara. Ulinzi na usalama si zina wizara zake, mambo ya ndani na ile ya ulinzi. TISS kamilifu inatakiwa iweze kusaidia popote pale, hata kampuni ya hapa nchini ikitaka kutengeneza pikipiki ikakwama kutengeneza injini, TISS inabidi iwe na uwezo wa kupata wapi la kupata ujuzi wa kutengeneza injini kwa namna yoyote ile. Ndio vitu duniani wanafanya, China mara nyingi tu unasikia wameiba TB za data kuhusu kitu fulani. Survival of the fittest
Madini,,,,,,,,,
 
Back
Top Bottom