Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa TISS, Said H. Masoro, na Mtazamo wangu

SAHIHI.

Na >'jicho la kuona kote na mote'< ni kitu chenye nasibu ya 'kucheza Mungu'...

Ndiyo maana taasisi zote za namna hii duniani huvutia watu wema na wabaya; na wetu wengi wangalipenda kuwa taasisini kwa ajili ya 'mambo ya upendeleo' kwa wale watu walio nyuma ya pazia...

Siku za mbele, ushamba wa 'usiri wa mambo' na 'siasa za nyuma ya pazia' vitakoma. Kuna mambo yamekuwa ni sanaa na taaluma za >'Taasisi Jicho--Taasisi Mwewe'<--vile kuona mapana na vipenyo kana vile kutoka juu, isivyo wa wengi walio tambarareni; tena juu ya sera za nchi zenye kutawala uhai wa taifa, yatakuwa maarifa ya kawaida ya kila mtu, kila raia, kila 'mja mwema'...

Tupo kwenye >zama mpya< ya maendelo na hatua za kibinadamu ambamo 'tabia za kishirika' zenye kufanyakazi na kustawi kwa 'sanaa na usiri/siri' zitakuwa si zenye 'manufaa' ya ukweli ila 'mning'inio' wa vilevi vya kizamani...

Kwa hivyo ni kweli, suala la maendeleo yakweli na bora--pia makusudi kwa stawi za mapana ya jamii ni hitaji kwa dhamira ya dhati katika kujipambanua kutoka kwenye 'siasa za tawala' kuelekea kwenye 'uongozi wa kweli' wa jamii...

Amerika, Merekani, wametaasisha idara zao za uono mifumo kwa alama ya >'Tai' na 'Nyota'<, lakini hiyo ni duru ya kwanza ya uhai wa mjumuiko wa 'taasisi ya akili-dola' kujihami na mataifa mengine yenye kustawi--na kila baada ya mapana fulani ya maendeleo na ustawi, wao huongeza idara...

Afrika bado kidogo taasisi-jicho zetu zinaushamba wa kuiga na kuzuga; hili linakwenda kubadilika siku za usoni.

Kwa hiyo tuzungumze na kujadili juu ya mifumo na huku tukitafuta kuelimishana zaidi, na basi mengi yanaweza kubayanishwa na kuleta chachu ya mageuzi--na mageuzi yana kitovu cha utashi, pia ushawishi, kote kote katika umma na pia watawala...

Kwa muktadha huu, jambo adhimu linalosubiri ni utashi wa umma juu ya mifumo, na kwa watawala-- hitaji kwa maarifa sahihi na upeo kwa 'machaguo ya kitaasisi' yaliyobora katika kujinasibu na mageuzi ya kijamii kwa kupitia 'fanusi-jamii' za namna mpya...

Pasipo taasisi imara za jicho--zenye kukomaa na 'kumbukumbu/uzoefu' na tena upeo na maarifa ya nyongeza kwa sura na mienendo ya jamii, tutaishi na kadiri ya >watawala na si viongozi<... Basi, taasisi jicho zinahitaji 'kuzaliwa upya' ili zisiishie tu kuwa 'mikondo ya taarifa-kisogo' kwa ajili mifumo mibovu ya tawala na utumishi...

Hii inawezekana kupitia jitihada sahihi za >ELIMU 2.0 na ELIMU 3.0<
 
Tapeli tu wewe
 
Ukiangalia mataifa yote, Usalama wa Taifa una play part kubwa sana kwenye uchumi wa nchi bila wao ni kazi bure View attachment 2468361

Mkuu umenena vizuri! Baadhi ya tradition thinkers wao wanadhani ujasusi wa kiuchumi sio sehemu ya TISS ! ni kama ideology flani ya Wajamaa, ila wale wanao enda na β€œupepo wa mageuzi ya kiuchumi” hutumia taasisi hizi kuzinufaisha nchi zao kiuchumi na kiteknolojia!
 
Jibidiishe kusoma maandiko mbali mbali utaelewa na Kukubaliana na mtoa uzi.

Idara Ya Usalama wa Taifa ina cover almost sector zote ambazo zinafanya Ustawi wa Taifa na zinazochangia Maendeleo na au "Stability" ya Taifa.

Mkuu kuna Wakati nenda dm uulize. Unaweza kuwa unabishana na Bosi wa TISS na wewe unatoa nadharia na mwenzako anatoa uhalisia.
 
Wengi wanafikiri Usalama wa Taifa hauhusiani na uchumi basi hata hawakumbuki Magu akiwa anasisitiza vita vya kiuchumi ni mbaya ?

Wapeni elimu zaidi mkuu
 
Alichosema Tindo ndio hali halisi yenyewe
 
Mi nirifikili unamchambua boss mpya wa TISS,uwezo wake,katoka wapi,kasoma wapi,CV yake,
Kumbe una promote kitabu chako!!
Unatembelea kwenye fulsa,
Hii ni opportunisticim ya hali ya juu
 
Magu alikuwa na kamsemo kake " hakuna vita mbaya kama vita ya uchumi". TISS wangelikuwa makini na hiyo kauli, jamaa tungekuwa naye hadi sasa.

Kifo cha Magu kinaonesha wazi kwamba TISS wako sharrow kwenye ujasusi wa kiuchumi na wamejikita zaidi kwenye ujasusi wa kisiasa. Magu ali out smart hiyo taasisi kwani maamuzi ya Magu yalikuwa mbele zaidi ya TISS.

CIA, M16, MOSSAD, KGB , etc ndo taasisi zinazofanya biashara kubwa duniani kama madini, mafuta, madawa e.t.c. hawa jamaa wanatoa funds kwa local private companies ili ziweze kuwapatia data za kibiashara. TISS yetu imelala usingizi wa pono kwenye upande wa uchumi ila wako active kuwakamata wanasiasa na kulinda chama.

Projects kama Kabanga Nickel, SGR na Bwawa la nyerere zikisimamiwa vizuri zitaleta impact kubwa kwenye uchumi wa nchi ila zinaendeshwa kisiasa na sidhani kama zitatoboa.

Kiukweli hii nchi ili iweze kusonga mbele, TISS inabidi wabadilike, wajikite zaidi kwenye uchumi. Waende sambamba na tech startup companies zenye innovations ila hazina mitaji wazisimamie ziweze kwenda na vizuri na kasi ya dunia.

Rwanda na Kenya wanajitahidi katika ujasusi wa kiuchumi ndiyo maana wanapeta kwenye nyanja za kimataifa.
 
Umeamua maksudi kutoelewa?
Ni namna gani unaweza kutofautisha mfumo wa intelligentsia wa nchi na uchumi wa nchi?
Kila nchi inayojielewa hapa duniani inaimarisha sana Intelligence Agency zao:

Mossad wapo busy pamoja na mambo yite wanayoyafanya kuimarisha diplomasia ya kimataifa ili products za Israeli ziuzike duniani kote.

Tawi la CIA, yaani USAID wapo busy kuanzisha miradi inayoonekana (au kuaminika) ya kijamii yaani humanitarian lakini ajenda nyuma na kuexplore dunia yote na kupenyeza influence ya Marekani kiuchumi duniani kote.

Ndivyo wanavyofanya nchi zote duniani zenye maono.

Ni kweli Benki Kuu na taasisi zinginezo zina nafasi yake katika uchumi wa nchi. But nafasi yao I think ni kuregulate, kupredict na kuconsult on fiscal policies na macro/microeconomics za nchi husika.

Lakini linapokuja suala la kuwa na uchumi shindani, kuwa wa kwanza on the market, kupenya na kuteka masoko mbalimbali asee njia intelligence system ya nchi ambayo nikiri inapaswa kuwa system tambuka lakini coordinated, lazima ihusike.

Vinginevyo mtabaki na TISS yenu inayohangaika na wenyeviti wa vijiji na makatibu kata ili CCM ishinde na kujizolea asilimia 100. Japo kuna njia bora za kushinda uchaguzi bila kuwa na mawazo ya kitoto namna hiyo.
 
Naona umeamua kutulazimisha kurejea kitabu chako bila kugusa serious analysis as the title claims

don’t be a trumpet, be the brains
 
Be positive mkuu

Hata hizo investments unazozitaja ziko supported na hao unaowakandya
 
Yoda bwana! Unafikir vita nyingi duniani husabanishwa na nini? Nyingi ni uchimi, Ukraine, Ghuba, Syria kote huko ni uchumi.
Lakini pia kumbuka mtu mmoja alitangaza vita ya kiuchumi hakutoboa, laiti tungekuwa na taasisi iliyojiimarisha huko ingesaidia.

Sent from my Infinix X693 using JamiiForums mobile app
 
Lakini linapokuja suala la kuwa na uchumi shindani, kuwa wa kwanza on the market, kupenya na kuteka masoko mbalimbali asee njia intelligence system ya nchi ambayo nikiri inapaswa kuwa system tambuka lakini coordinated, lazima ihusike.
Jamaa umetema madini sana
 
Wewe ni mtu feki tu! Unaleta hadithi za kutunga ili ziendeshe nchi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…