Uchaguzi 2020 Uteuzi wa Van Zeland kuwa Mgombea Ubunge Mvomero kwa upande wa CCM, haujatutendea haki wananchi wa Wilaya ya Mvomero

Uchaguzi 2020 Uteuzi wa Van Zeland kuwa Mgombea Ubunge Mvomero kwa upande wa CCM, haujatutendea haki wananchi wa Wilaya ya Mvomero

Nategemea kwa kuwa kuna mabadiliko ya uongozi.Mimi sichagui chama,nachagua mtu.Na frankly sioni chama chote chote ambacho kina uongozi imara na makini wa kuiletea Tanzania maendeleo.Niseme hivii,even when CCM is weak,it is still stronger than other parties.
Shida umeshazizoea mkuu
 
CCM iliungana na ASP na kuzaa CCM 05.02.197. Lakini uko sahihi kuhusu maendeleo, tulipoteza nguvu zetu kuwaita watu makaburu, tukamwita mwingine nduli na katika hayo tulitumia pesa zetu nyingi. Sasa hivi nchi hizo zinatupotezea ile mbaya. Hatujakaa sawa tukaita wengine mabeberu. Badala ya kuwa na strategic partnership tunasema tuko kwenye vita vya kiuchumi!

Kazi yetu imekuwa ni propaganda tuuuu!!! CCM haiwezi kutukwamua hapa tulipo, labda ishindwe kwanza uchaguzi na kisha irejee!!
Like 5
 
Mvomero sio Wilaya kongwe,na kwa hiyo kimaendeleo iko nyuma sana.Wilaya hii ina matatizo mengi, ya msingi yakiwa upatikanaji wa maji,migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imedumu kwa miaka mingi sasa.Awamu zote zinaonekana kushindwa kabisa kutatua tatizo hili,sababu kubwa ikiwa viongozi kuwa mgongano wa kimaslahi. Lipo pia tatizo la kilimo,hasa upande wa ugani na umeme.Lipo pia tatizo la miundombinu ya elimu, ambalo limefanya wananchi wengi wa Wilaya hii kukosa elimu na hivyo kuwafanya wawe nyuma sana kimaendeleo.

Lipo tatizo kubwa mama la uongozi katika Wilaya hii.Sina haja ya kusema awamu zilizopita uongozi ulikuwaje,itoshe tu kusema kwamba Wilaya hii tangu kuanzishwa kwake haijawahi kupata viongozi committed kwa maendeleo ya Wilaya hii,tangu ngazi za chini kabisa mpaka juu.Si ajabu kwa hiyo kwamba maendeleo ya Wilaya hii ni duni sana.

Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi,tena uchaguzi wa mhula wa pili awamu ya tano.Tulitegemea basi kwamba Wilaya yetu ingeangaliwa kwa jicho la pekee,ili ipate viongozi makini na wazuri ambao watasukuma mbele maendeleo yetu.Kilichotokea hata hivyo ni tofauti kabisa.Van Zealand ambaye ameteuliwa kugombea kwa tiketi ya CCM hawezi kutusaidia kabisa.

Huyu bwana amekuwa mwenyekiti wa Halmashauri kwa muda mrefu,na katika kipindi chake chote alichokuwepo hali ya Wilaya yetu haijaboreka na matatizo ya wananchi yapo pale pale, au hata kuzidi. Katika hali ya kawaida kabisa, hili lingetosha kumuengua. Na kwa nini ameteuliwa yeye kupeperusha bendera ya CCM wakati aliyepita kwenye kura za maoni ni Makala?

Niseme wazi, kwetu Makala angekuwa bora zaidi kuliko Zeland,ingawa of course naye ana matatizo yake.Van Zeland tunamjua, yuko kimaslahi zaidi na naamini ameingia huko kwa ajili ya maslahi yake binafsi,na wala sio kuwatumikia wananchi.

Ipo minong'ono mingi kuhusu michezo michafu,na inasemekana hata tambo zake mwenyewe zinaashiria hili. Katika hili naiomba TAKUKURU iingilie kati,huenda labda ikatunusuru.

Mwisho,binafsi najiuliza sana,hivi kwa nini CCM ilitangaza hadharani kwamba si lazima anayepita kwenye kura za maoni ateuliwe yeye kupeperusha bendera ya CCM?Hivi chama hakikuona kwamba mwanya huu ungeweza kutumiwa vibaya na watu wasio waaminifu kama ilivyotokea Mvomero, ingawa nia ilikuwa njema?
Subiri uone utendaji wake. Mapovu ya nini
 
areafiftyone kwa upande wa Turiani kwa saa hivi naona TuRUwAsa wamejitahidi sana maji yakutosha.
Tunataka iwe maeneo yote sio maeneo fulani fulani tu.Maeneo mengi Wilaya ya Mvomero wananchi wanatumia maji ya mabwawa ambayo si salama kabisa.Mradi wa Wami Dakawa kwa mfano,is a laughing stock,na pale ni Wilayani kabisa,lakini viongozi hawajali kwamba wananchi wanateseka.We demand change.
 
Nime-compare two evils,kuna a better evil.Makala is a better evil.Kama nia yao ilikuwa kwamba tupate mchapa kazii,which is what we want,wangetupatia Maganga.Unajua Makala angalau wananchi walimchagua,huyu amepitishwa kiana aina tu,kitu ambacho kina maswali mengi ya kujiuliza.Kwa maneno yaliyopo mtaani na mazingira yaliyopo,mizengwe imetumika kumteua Zeland.Let me tell you,chama chetu kijue,wananchi wa Mvomero hatujafurahishwa na jinsi chama kilivyotufanyia.Ni heri wangemuacha Makala.
Hamjafurahishwa lakini mtampigia kura Van Zeland. Na bado mnategemea kuwa siku nyingine wataogopa kupingana na uamuzi wenu!

Amandla...
 
Ni mtanzania na alikuwa diwani kasaidia sana huyo
Pale hakuna mtu...anachojua yeye ni kudai posho tu hata katika kutimiza majukumu yake. bila kumpatia posho hupati huduma kwa yule jamaa. Mvomero wanaendelea kudondokea pua tena kwa miaka mitano ijayo kama watamchagua huyu jamaa kuwa mbunge. Bora wachague wa upinzani
 
Hamjafurahishwa lakini mtampigia kura Van Zeland. Na bado mnategemea kuwa siku nyingine wataogopa kupingana na uamuzi wenu!

Amandla...
Kwa jinsi hali ilivyo kumhusu Van Zealand apa Wilayani,ni vigumu sana watu kumchagua.Hata hivyo aliyefanya mizengwe yote mpaka Zealand akapita kwa kuwa bado yupo(na tunamjua!) kwenye nafasi yake,naamini atafanya mizengwe tena ili apite.Hata hivyo tunaamini kwamba Zimwi likujualo halikuli likakwisha,ingawa linabaki kuwa Zimwi.Na ikumbukwe kwamba sio lengo.
 
Subiri uone utendaji wake. Mapovu ya nini
Nyota njema huonekana asubuhi mkuu.Huyu bwana alikuwa Mwenyekiti wa Halimashauri,lakini mambo yalikuwa hovyo kabisa.Na mbona tabia yake tunaijua?Huwezi kupata uongozi kwa kuzunguuka mbuyu, mkuu halafu uka-perform,that is unthinkable.Tatizo ni kwamba Madiwani wake kama akina Sosa ni magarasa,kwa hiyo chini hana msaada.
 
Pale hakuna mtu...anachojua yeye ni kudai posho tu hata katika kutimiza majukumu yake. bila kumpatia posho hupati huduma kwa yule jamaa. Mvomero wanaendelea kudondokea pua tena kwa miaka mitano ijayo kama watamchagua huyu jamaa kuwa mbunge. Bora wachague wa upinzani
Ashapita Bila kupingwa huyo. Mwache na yeye akaenjoy maana mtu kama Murad Saddiq hana lolote Papaa Makala mzee wa Bata.
 
Back
Top Bottom