Uteuzi wa Wakurugenzi unafanyika lini? Mambo mengi yamesimama Wilayani

Mama Anajenga Kwanza UCHUMI ameomba Apewe Muda baada ya UCHAGUZI MKUU 2025
 
Kwani hakuna wakurugenzi?
 
Nami nmo.
 

Samahani mkuu nimekupa Like
 
Mkeka utakuwa unasukwa upya kuwaengua wale makada waliooshindwa uchaguzi ndani ya chama na kupoozwa kwa u-DED na mwendazake. Kwa sasa sifa na vigezo vya anayetakiwa kushika nafasi ya DED au DAS vitazingatiwa ili kuharakisha maendeleo zaidi, makada tunaomba mkae kidogo kwa kutulia...
 
Pesa ya kufanya huo mchakato hipo. Tulieni tunajenga uchumi kwanza.
 
Mitanzania tumekuwa Wajinga Sana, Yaani mtu anakaa siku, miezi akiwaziwa Uteuzi tu.Daah! Katiba Mpya Itapunguza Ujinga huu kwa maana hizi ni Miongoni Mwa Nafasi Zinazohitaji weledi so application and interview itakuwa sehemu ya Kuwapata Watu sahihi. Hatutaki Mtu Kupewa nafasi kwa sababu ana Kadi na Jezi ya CCM. Kwenye Dai la Katiba Mpya Tuwaunge Mkono CHADEMA ili Kukomesha Ujinga huu.
 
Huu ndio mushkeli mwingine nchini. maDED walitakiwa kuwa waajiriwa wa Halmashauri (serikali ya mtaa); si wateule wa kisiasa wa Rais. Tena wanatakiwa kuchujwa kiushindani kwa vigezo vya kitaaluma, uzoefu na utendaji. Katiba inatakiwa kuainisha mfumo sahihi wa utawala.

Nchi inaendeshwa kisiasa kupita kiasi, Rais ana mkono kila mahali: maRC, maDC, maRAS, maDAS, maDED, halafu mnategemea maendeleo na utawala bora? Wenye sifa ni wale makada wenye kelele nyingi kwenye media na hasa katika kupambana na wapinzani?
 
Tunasubiri kwa hamu kubwa sana! Tenda miujiza basi Rais wetu!
Uteuzi wa Ma DED ni kupunguza hali ya utumishi wa Umma, Hawa wapandishwe vyeo ndani ya mfumo wa serikali za Mitaa, Watendaji wakuu wa Wizara wasimamie hili, Rais ataeue mpaka wakuu wa Wilaya tu.
 
Tulia wewe,kwani hujui kama suala la miamala ya simu limebadilisha upepo?
 
Teuzi hazina maana sana kwa sasa kinachoangaliwa ni miamala ya simu tu , wametengeneza tatizo sasa wanataka kulitatua waonekane miamba, ila viongozi wa Tanzania Mungu anawaona sana tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…