Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Hahahaha hahahaha vita vya panziJapo mie siipendi CCM Ila amechemka this time. Amebeba watu hata ambao hawapo kwenye siasa sio sawa, kuna watu wanahangaika na chama kila uchwao na wanatumia Hadi gharama zao kiukweli asingeweza kuchukua wote Ila nafasi hizi ndio huwa za kueapooza japo wapate jina.
Pia aleta watu ambao hawajawahi hata kujua minute sheet inaandikwaje mtu ametoka shule hajawahi kukaa kufanya kazi kidogo. In short secretary ndio anageuka mwalimu wa DC kumuelekeza namna ya kuendorse mafaili.
Kachemka sana na kwa huu mwendo nimeanza kumchoka mapema sana.
Ni swala la kuwaelekeza misingi ya kazi yao na majukumu ya ukuu wa wilaya..Nafasi wapewe lakini sio ukuu wa wilaya. Wanaelewa nini kwenye utumishi na ulinzi na usalama.
Mkuu mbona POVU jingi hivyo? Kama povu limezidi hebu vua tamang'eo yake ufulie. Wewe shambulia hoja usimshambulie mtoa hoja. Hapa ndipo watanzania wengi mnapokwama.Wewe nani mpaka useme hivyo cha kushangaza wewe ni mateka wa Mbowe unataka Rais Samia, akufurahishe? Nyie kupinga ndiyo kazi mliotumwa na Mfalme Mbowe, Rais kawambia mpo huru kufanya mikutano yenu nchi nzima au nyie mnafanyie JF.
Kuna jamaa yangu kateuliwa wilaya flani kanda ya ziwa mkoa unaanzia na S. Yaan huyu jamaa ni 0 brain wa kutupwa, yes ana kadegree ila akili nzito hajui kila kitu, ana 40+ hana mke, hana nyumba yaan maisha ya kuungaunga, mlevi kupindukia. Sijui wateuliwa kama wanafanyiwa vettingInasikitisha sana Tanzania sijui inaelekea wapi. DC ni nafasi nyeti ya kuunganisha watendaji na jamii inayowazunguka. Kusimamia mambo ya ulinzi na usalama. Hii ni nafasi ya waandamizi kutoka katika utumishi au chama, wakiwa wamejaa utu uzima na busara za kumwagika. Leo unaenda kuokoteza wasanii na watu mitandaoni.
Naona Tanzania inapoteza uelekeo kabisa. Hawa jamaa wanatupa kazi sana kuirudisha Tanzania kwenye reli.
Mimi sijawahi kushuhudia uteuzi wa hovyo kama huu toka nizaliwe.
Kiufupi rais kaelemewa na majukumu
Maprofessor wamefanyia nini hii nchi miaka yote hiyo mambo yamebadilikaAisee uteuzi mbovu 75% .Yaani vyuo vya adminstrative vina changamoto,Kuna ma professor ,wahitimu weredi wakubwa wa siasa na uongozi.
Leo hii bongo movie,bongo fravour,Journalist wawe ma DC.
Nchi Bado inasafari ndefu Sana ,acha waendelee kututukana mpaka tuishike adabu
Wanamkoma maana walijitoa akili. Ila nawaonea huruma sema wakome hawana nidhamuHahahaha hahahaha vita vya panzi
MATAGA ni kama vile leo hawapoWanamkoma maana walijitoa akili. Ila nawaonea huruma sema wakome hawana nidhamu
Kimsingi huyo mama hana jinsi ya kuacha kuwapa vyeo baadhi ya watu waliowatoa upinzani. Ifahamike mbinu za ccm kuendelea kubaki madarakani ni pamoja na kuwachukua wapinzani na kuwapa vyeo, ili kushusha imani ya wapinzani na upinzani nchini. Hivyo iwapo wapinzani wenye uchu wa madaraka wanaoribuniwa na kuingia ccm baadhi yao wasipopewa vyeo, wengine hawatahamia ccm, na ccm itaendelea kujikuta katika wakati mgumu sana wa ushindani wa kisiasa.Kwa mara ya kwanza katokota..watu kama kina Msando hao wanamsaidia nini? Au la yuko kwa system
Kununa hawawezi sababu new supporters wa mama wakiboreka nae wao wanalazimika kujifanya wanaomsifia ili aharibu zaidi lakini mionyoni mwao wanaumia sana.MATAGA ni kama vile leo hawapo
Hakuna uteuzi mwiba kwa bavicha kama huu.Ulichoumia ni wale wafuasi wenu wa zamani kupewa vyeo hamna lingine.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huu uteuzi bavicha wana hali ngumu hatariHivi Makonda hajachukuliwa??
Naomba tupe mfano wa aliyeweza kwa vigezo vyako ili tupime huko kushindwa kwa jokate.Joketi kaweza kipi .Watu wa kisarawe wengi wao ni wakulima Bora kama angewasaidia kupata masoko ya mazao yao hapo tungeona kaweza.Eti mnadai kajenga shule .sasa kama ni shule mbona zimejengwa nchi nzima.nachokiona kwake anabebwa na midia tu ,Hana ubunifu wowote.
Chadema wameumia sana kuwaona kina Lijuakali, nasari na wengineo wamekula teuzi!Aisee hizi ni chuki binafsi kila mtu ana haki ya kuwa kiongozi kama ana akili timamu
Vyeti vyake vinaonyesha alijiendeleza. Alisoma Esami. Usimzungumzie mtu kwa uhakika jambo ambalo huna hakika nalo.Ester Mahawe ni F4 lakini kawa DC anaenda kuongoza watu na degree zao
Acha zako wewe!Kimsingi huyo mama hana jinsi ya kuacha kuwapa vyeo baadhi ya watu waliowatoa upinzani. Ifahamike mbinu za ccm kuendelea kubaki madarakani ni pamoja na kuwachukua wapinzani na kuwapa vyeo, ili kushusha imani ya wapinzani na upinzani nchini. Hivyo iwapo wapinzani wenye uchu wa madaraka wanaoribuniwa na kuingia ccm baadhi yao wasipopewa vyeo, wengine hawatahamia ccm, na ccm itaendelea kujikuta katika wakati mgumu sana wa ushindani wa kisiasa.
Kiuhalisia ccm imeshapoteza ushawishi kwani tayari ni chama cha kizazi kilichopita. Hivyo inabidi kutumia mbinu za kughilibu wapinzani hasa kwa njia ya vyeo, ili kupunguza nguvu ya upinzani. Mbinu hizi ni za kawaida sana kwa vyama vyote vilivyo madarakani hasa kwenye nchi masikini, ambapo watu wengi wako kwenye siasa kwa ajili ya maslahi binafsi, kisha itikadi baadae. Hivyo chama kinachokuwa madarakani hutafuta wapinzani wenye uchu wa madaraka na kuwapa vyeo, kisha kuwatumia kuchafua taswira ya upinzani ili kujijengea imani.