Kimsingi huyo mama hana jinsi ya kuacha kuwapa vyeo baadhi ya watu waliowatoa upinzani. Ifahamike mbinu za ccm kuendelea kubaki madarakani ni pamoja na kuwachukua wapinzani na kuwapa vyeo, ili kushusha imani ya wapinzani na upinzani nchini. Hivyo iwapo wapinzani wenye uchu wa madaraka wanaoribuniwa na kuingia ccm baadhi yao wasipopewa vyeo, wengine hawatahamia ccm, na ccm itaendelea kujikuta katika wakati mgumu sana wa ushindani wa kisiasa.
Kiuhalisia ccm imeshapoteza ushawishi kwani tayari ni chama cha kizazi kilichopita. Hivyo inabidi kutumia mbinu za kughilibu wapinzani hasa kwa njia ya vyeo, ili kupunguza nguvu ya upinzani. Mbinu hizi ni za kawaida sana kwa vyama vyote vilivyo madarakani hasa kwenye nchi masikini, ambapo watu wengi wako kwenye siasa kwa ajili ya maslahi binafsi, kisha itikadi baadae. Hivyo chama kinachokuwa madarakani hutafuta wapinzani wenye uchu wa madaraka na kuwapa vyeo, kisha kuwatumia kuchafua taswira ya upinzani ili kujijengea imani.