Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika Juni 2021 umeshusha hadhi ya nafasi hiyo

Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika Juni 2021 umeshusha hadhi ya nafasi hiyo

Aisee uteuzi mbovu 75% .Yaani vyuo vya adminstrative vina changamoto,Kuna ma professor ,wahitimu weredi wakubwa wa siasa na uongozi.
Leo hii bongo movie,bongo fravour,Journalist wawe ma DC.
Nchi Bado inasafari ndefu Sana ,acha waendelee kututukana mpaka tuishike adabu
Shule yao ni Ole Sabaya kwahiyo hawawezi kurudia makosa, watakuwa waadilifu!! Wapewe ushirikiano tu
 
Inasikitisha sana Tanzania sijui inaelekea wapi. DC ni nafasi nyeti ya kuunganisha watendaji na jamii inayowazunguka. Kusimamia mambo ya ulinzi na usalama.

Hii ni nafasi ya waandamizi kutoka katika utumishi au chama, wakiwa wamejaa utu uzima na busara za kumwagika. Leo unaenda kuokoteza wasanii na watu mitandaoni.

Naona Tanzania inapoteza uelekeo kabisa. Hawa jamaa wanatupa kazi sana kuirudisha Tanzania kwenye reli.

Mimi sijawahi kushuhudia uteuzi wa hovyo kama huu toka nizaliwe.

Kiufupi rais kaelemewa na majukumu
Uongozi ni tatizo kubwa duniani hasa nchi maskini. Ni hatari uongozi unapogeuka ni zawadi.
 
Ingia kwenye website ya bunge jaribu kama utaikuta. Ukiikosa jaribu kitengo cha uteuzi na vetting ya wakuu wa wilaya watakupa information zake.
Huyu mtu aligombea ubunge mwaka jana akajaza ana f4+ cheti cha ualimu daraja A, alienda kusoma degree saa ngapi?
 
Tungesubiri utendaji wao kwanza ndio tuwahukumu, msanii na usanii na yenyewe ni kazi so tusihukumu kwa kazi zao, tuwape muda then tuwakuhumu kwa utendaji wao. Kuna madokta na maprofesa kibao wamekaa kwenye nafasi kubwa na ndogo but hawakuwahi kuonesha impact yeyote zaidi ya kujisifia na elimu zao, wenye degree moja tumewaona, wanajituma, wabunifu na wafuatiliaji so lets wait, time will tell brother
 
Huyu mtu aligombea ubunge mwaka jana akajaza ana f4+ cheti cha ualimu daraja A, alienda kusoma degree saa ngapi?
Unataka kujua vetting yake in details? Tuarrange live meeting nitakupatia information zake. Inbox me your contacts.
 
Hazina hadhi kabisa thus kina sabaya walipewa.
Kama nchi atujafikia kukosa wasomi hadi kuokoteza.
Nafasi za UDc ilifaa zitangazwe watu waombe kisha wachujwe wapatikane wenye sifa na sio hii ya yeyeto tu anapewa
 
Nafasi za UDC zinatumika kama mtama kwa watoto kuwavuta vijana toka Chadema waende CCM.
 
Back
Top Bottom