Uteuzi Wanafunzi wa vyuo Vikuu hadi Sept 22 -TCU

Uteuzi Wanafunzi wa vyuo Vikuu hadi Sept 22 -TCU

Status
Not open for further replies.
Hawa jamaa wanaudhi kweli. mpaka sasa hivi hamna lolote!!!!






Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU)imefunguka na kuweka wazi kuwa mpaka sasa hawajatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga katika vyuo mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2014-2015 kama ambavyo watu wanakuwa


New-Media.jpg
Afisa habari Mwandamizi toka TCU, Edward Mkaku akichat Live katika ukurasa wa Facebook wa EATV.

wakidai kuwa tume hiyo imatangaza,Afisa habari Mwandamizi toka TCU, Edward Mkaku amesema hayo leo alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa mashabiki wa ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita mchana mpaka nane mchana.
"Mimi mwenyewe nimesikia kuwa watu wanadai Tume ya vyuo vikuuu imetangaza majina ya wanafunzi waliochanguliwa kwa mwaka wa masomo 2014-2015 lakini nashindwa kuelewa hizo tetesi au hayo majina waliyoyaona yametoka wapi?maana mpaka sasa Tume kama tume badao haijatoa majina hayo ya wanafunzi na tunategeme kuyatoa kwenye tarehe 22 ya mwezi huu,baada ya Joint Admission Comitee kupitia na kupitisha majina hayo."
Mbali na kueleza juu ya siku ambayo Tume ya vyuo vikuu itatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa vyuo mbalimbali lakini pia Edward Mkaku alijaribu kufafanua kuwa hawajachelewa kutoa majina ya wanafunzi kujiunga vyuo kwa kuwa miaka yote vyuo vilivyo vingi hufunguliwa mwezi wa kumi hivyo ni kawaida kwa majina hay9o kutoka mwezi wa tisa ili ifikapo mwezi wa kumi wawezi kujiunga bila matatizo,pia alidai kuwa hiyo imekuwa kawaida kwa Taasisi hiyo kutangaza matokeo mwezi wa tisa kwani hata miaka miwili iliyopita yalitangazwa mwezi huo huo.
"Nadhani kila mtu anatambua kuwa vyuo vikuu vingi hufunguliwa mwezi wa kumi hivyo imekuwa kawaida kwetu kutangaza majina ya wanafunzi waliodahiliwa katika vyuo mwezi wa tisa maana hata mwaka jana na mwaka juzi ilikuwa hivihivi ndugu"
ADA ELEKEZI
Katika masuala ambayo yamekuwa tatizo kubwa kwa wanafunzi wengi na wengine hata kupelekea kushindwa kumaliza masomo yao ni suala la Ada na kumekuwa na utofauti mkubwa sana katika masuala ya ada kutoka chuo kimoja mpaka chuo kingine hususani katika vyuo vya watu binafsi au taasisi.lakini kwa mujibu wa Afisa habari Mwandamizi toka TCU, Edward Mkaku amesema kuwa kwa mwaka huu wa masomo 2014-2015 Taasisi ya Vyuo
Vikuu imekuja na mfumo elekeze wa ada kwa vyuo vyote na wanapaswa kuufuata,yaani kila chuo kimepangiwa Ada inayostahili kulipwa na wanafunzi kulingana na uwezo wa chuo husika na huduma itolewayo katika chuo husika.
Kitendo cha Tume ya Vyuo Vikuu kuja na mfumo elekeze wa Ada kwa vyuo vikuu itasaidia kushuka kwa Ada kwa baadhi ya vyuo vilivyokuwa vikichaji Ada kubwa kuliko huduma wanayoitoa.pia itasaidia hata wanafunzi kuweza kumudu Ada hizo katika vyuo hivyo.
"Mkaku kuanzia mwaka huu kuna utaratibu wa Ada elekezi ambapo Tayari kila chuo kinapaswa kuufuata"
 
wee jamaa mpumbavu kwel,wa2 wanataka msaada co majungu, afu km hujui english umeingia kwenye hl jukwaa kufanya nn! idiot
 
xaxa lengo lako nn mpaka unawaombea mabaya madogo et wakoxe mkopo.unataka ukaxome ww hvyo vyuo? au ulitaka wazungumzie mada gan kwenye hl jukwaa.au umepost k2 hawajachangia.ukiona wamepost k2 hakikuhuxu temana nacho ingia hta jukwaa la xheria au udaku kama ndo unakufaa

Hapa sijui kimeandikwa kitu gani!
 
dah....nlikua sitegemei kabisa kuchaguliwa TEKU...nliijaza tu..

kwa anaepajua vizuri anisaidie
 
Bandungu! Hebu tufikirie kabla ya! We jambo la kusikia unanyanyukanalo tu! Pata uhakika kwanza coz wengine afya mbovu
 
Upu*vu tu, xa kila mmoja uzi tcu achen upuuz, mnaboa kiukwel mnakua kma vitoto vya ps
 
wewe uliyeandika habari ya tcu nahic umekosa kazi ya kufanya, nenda ukalime.
 
http://www.cas.tcu.go.tz/2/selected_applicants

ingien mwangalie saiv
 
Nimepita ubungo plaza pale nikweli nimekuta kuna magari mengi ya vyuo tofauti Tanzania
so haka kasms kanakotembea ka trh 24 ka kanaukweli hivi lakini sitaki kuamini.
 
mwenye taarifa kamili kuhusiana na post kutoka tar:17.oct naomba atujuze maana hawa jamaa mimi siwaelew....!!!
 
wadau kwa yeyote atakayepata chochote kinachoendelea kwa hawa waheshimiwa yaani TCU & NACTE atujuze kwa sababu walitujulisha kuwa leo ndio ile siku ya kujua mbivu na mbichi.

#GOD BLESS US....!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom