Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli

Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli

Hata aruke sarakasi ajuazo ukweli elimu kakomaa yeye mwenyewe sehemu kubwa.
Lakini huku chini msingi akumbuke jina alilotumia kwa kununua kwa ngombe tisa na biashara ikaisha na mwenye jina hana tatizo maana kachukua chake.
Utaratibu huu ulikuwepo huko nyuma na wengi wameutumia kwenda sekondari. Ikiwa serikali ikiamua kufanya follow up hapa nusu ya watumishi twaweza kuwakosa.
Mwigulu yuko sahihi kueleza hayo ni ujasiri maana wazungu husema being silence means yes. Sasa ikiwa atakaa kimya mtajua ni kweli. Kujitokeza ni ishara ya kukataa hata kama ni kweli.
Yeye kalitendea jina haki kwa kusoma na kufaulu but kuna ukakasi mkubwa kwa majina yake.
Hakuna dhambi ndogo zote ni sawa, nashauri serikali iwalipe pensheni zao wale iliowatumbua maana hizo hela zipo na waliozikalia wengine wana majina sahihi ila elimu feki n.k.
Haya yamejadiliwa sana humu kuhusu mwigulu wapo wanaomjua sawasawa walileta post humu.
Mwigulu nahis ni jina la Kisukuma maana yake Mbinguni sjui labda kweli alinunua hizo ng'ombe maana miaka ya nyuma wasukuma walithaminisha mifugo kuliko ELIMU.
 
Sijawahi kua na mashaka na mwiguli, alisoma na jamaa yangu akawa anasema alikua anapita ananyoosha vidole 3 juu akimaanisha div 1.3 form 6 ila bahati mbaya alipata II.10.
Ndo uwezo wake sio bahat mbaya.
I ya point 3 mchezo?
 
Mr Pasco huenda kweli Mwigulu jina siyo lake ni kweli , tusijifanye hatujui miaka ya nyuma watu walikuwa wanarudia shule zaidi ya mara mbili Kwa Kutumia majina ya watu na ukifuatilia watu wengi wasomi Wa miaka ya 2004 kurudi miaka ya nyuma majina walionayo wengi siyo ya kwao, Pili miaka ya nyuma primary hapakuwa na pastort kwenye vyeti Kwa hiyo ilikuwa ni rahisi sana Kwa mtoto Wa maskini kuchukuliwa jina lake Na mtoto Wa Taita , Hayo ndo yapo Kwa akina Bashite na Mwigulu.Lakin Kwa leo hii ni vigumu kutumia cheti cha MTU mwingine kutokana na utaratibu ulioopo.
Mbona bashite mtoto wa juzi tu katumia jina sio lake ni vyeti vya miaka ya juzi tu[emoji196]
 
Ametumia jina sio lake
Jina ni lake kabisa maana alipewa hospitali, kwa vile hakuna majina yake aliyopewa alipozaliwa, wala hakuna majina ya wazazi wake, then ni majina yake aliyopewa, ila majina bandia ya kupewa tuu, hivyo sii kweli kuwa sii majina yake, ni yake ila bandia. Hata haya majina mengine yote tunayotumia, ni majina ya watu ambaoyo nasi tulipewa tuu kama na yeye alivyopewa!.

P
 
Mkuu Iparamasa, ni kweli kutumia jina la mtu mwingine ni kufoji ila hayo majina ya Mwigulu Nchemba sio majina ya mtu yoyote ni just given names, kama alivyoeleza mwenyewe, siku mtoto anapoandikishwa shule huwa kuna fomu ya majina ya wazazi, kwenye fomu zile za kumuandikisha shule huyu kijana wa Kinyiramba Lameck Madelu Mkumbo, wazazi wake walimuandikisha kwa majina yao kabisa ya Kinyiramba ila wakaomba utawala wa shule kumuandikisha mtoto wao kwa given names za Nesi wa Kisukuma Mwigulu Nchemba na hapo hakuna jinai yoyote kwa sababu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mtu unaruhusiwa kutumia jina lolote mfano Pasco wa JF ni Mashokolokubangashe as long as sio impersonation ya Mashokolokubangashe original.
Pasco

kwa mawazo yangu bado mm sioni tatizo mtu kutumia majina ya kupewa na mtu mwingine.zamani ilikuwa kawaida tu labda baba au mama wana urafiki na mtu wa kabila jingine wakaamua kuwapa majina ya watoto wao kutokana na ukaribu wao.
mtu mwingine anaamua tu hataki kutumia majina ya kikristo kama akina ngugi wa thiongo hivyo mm sitetei lakini sioni tabu kutumia majina mengine ilimradi tu yasiwe ya mtu yeyote yule bali yameumbwa tu kwa mila na desturi ya makabila fulani na yawe yanamainisha kumbukumbu fulani ktk jamii.
 
Okoso majina ni kitu given, mtu uko huru kutumia given names zozote, na kwenye registration unaruhusiwa kuji register kwa majina yoyote ili mradi kwenye ile fomu majina halisi ya wazazi wako lazima yawepo na hakuna sheria ya kulazimisha kuyatumia ila Polisi, Uhamiaji na Nida ni lazima majina ya wazazi yawepo na yatajwe with given names hata kama ni majina kumi. Hivyo ukweli wa majina halisi ya wazazi wake yapo shule alipoandikishwa, yapo immigration na Nida ambayo yanaonyesha Mwigulu Nchemba ni given names.
Pasco
Pasco unasumbuka na watanzania wanadhani majina ni big deal. U k watu wanabadilisha majina bila hata figisufigisu kuna jamaa mzimbabwe rafiki yanguvkishabadilisha mara tatu. Na kila akibadilisha anapeleka application kubadilisha leseni yake passport na bank account. Kutoka Tongai Mchekesi mpaka kuitwa Tony Makenzie na sasa karudi na jina jingine Makoni. Kinachotakiwa ni kujaza fomu halali za kufanya hivyo na zi idhinishwe job done. Na hiyo form inaitwa Deed poll unaweza kufanya hata online
 
Jina la pili, ni lazima liwe ni jina la kwanza la mzazi wako, na hapa hakuna excuse, kama mwanzo kwenye given name, umetumia jina la nyumbani, la kilugha, then jina la pili lazima liwe jina la ubatizo, ukitangulia na jina la ubatizo, then jina la pili au liwe ni jina la kwanza, la mzazi wako, au ukitumia fast name ya majina mawili yote ya kwako, then jina la tatu ni lazima liwe ni jina la kwanza la mzazi wako!, na jina la nne ni lazima liwe ni jina la ukoo wenu yaani sir name.
Paskali, bila shaka ulisoma HGL kidato cha tano na Sita....Hapa umeandika ukichanganya Kiswahili na Kiingereza. Una maana gani hapo nNILIPOWEKA RANGI? FAST Name....SIR Name. Kama naelekea kukuelewa, una maaanisha FISRT Name na SURNAME?
 
Wanabodi,
Katika zoezi la kusaka vyeti bandia, kuna watu wanashindwa kutofautisha kati ya vyeti bandia na majina bandia.

Cheti bandia ni cheti ambacho ama hakipo kabisa hivyo kimetengezwa cheti fake kwa forgery ama ni cheti cha kweli lakini anayekitumia sii mwenyewe mwenye cheti halisi, hivyo kufoji cheti cha mtu mwingine, hili ni kosa kubwa la jinai na huu ni wizi!.

Jina bandia ni kutumia majina ya kuunga unga ambayo sio majina yako halisi, lakini aliyeingia darasani kusoma ni wewe, aliyehitimu ni wewe, hivyo hicho cheti ulichokipata ni cheti halali na sio cheti bandia ila jina ndilo jina bandia.

Nimesoma utetezi wa Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kuhusu tuhuma za kuwa na cheti bandia, nimejiridhisha kabisa tena pasi shaka kuwa vyeti vya Mhe. Mwingulu Nchemba sio vyeti fake ila majina ya Mwigulu Nchemba ndilo jina bandia.

Sio kila jina bandia ni forgery, kuna majina bandia yanayoitwa Nick Names sio forgery bali ni just given names. Given names hizo zinapokuwa registered kwenye vyeti, vyeti hivyo ni halali ila jina la mwenye cheti ndilo jina bandia ambalo halina kosa lolote kisheria.

Uthibitisho huu ni kufuatia utetezi huu wa Mhe. Mwingulu Nchemba umethibitisha jina la Mwigulu Nchemba ni jina bandia la mtu halisi aitwae mwenye given name ya Lameck Madelu Mkumbo ambaye hata majina hayo,hakuna jina lolote la wazazi wake wala jina la ukoo wake, kama anavyojieleza yeye mwenyewe.


Mkuu Mhe. Mwigulu, kwa vile hili bandiko nimelikutia page 33, na sijaweza kusoma mabandiko yate ya nyuma, hivyo siwezi kujua kama ulijibu haya, ila kwanza kwa heshma na taadhima, nakupongeza sana kujitokeza kujibu tuhuma, ila very unfortunately, majibu yako, hayajitoshelezi kabisa!, hakuna kitu chochote ulichojibu hapa, you leave more questions than answers and there is something fishy!.

Majina yana formula ya majina, na hayawezi kuijiibukia tuu hivi hivi, na formula hiyo ni universal, dunia nzima.

Jina lina given name, yaani jina ulilopewa wewe, hili given name linaweza kuwa moja au hata kumi, haijalishi, kwenye given name, ni lile jina unaloitwa, liwe la utoto, ubatizo, etc, Kiingeza linaitwa fast name!.

Jina la pili, ni lazima liwe ni jina la kwanza la mzazi wako, na hapa hakuna excuse, kama mwanzo kwenye given name, umetumia jina la nyumbani, la kilugha, then jina la pili lazima liwe jina la ubatizo, ukitangulia na jina la ubatizo, then jina la pili au liwe ni jina la kwanza, la mzazi wako, au ukitumia fast name ya majina mawili yote ya kwako, then jina la tatu ni lazima liwe ni jina la kwanza la mzazi wako!, na jina la nne ni lazima liwe ni jina la ukoo wenu yaani sir name.

Kwenye majina yako, sijaweza kuona jina la mzazi na jina la ukoo, huwezi kutumia majina yote ya given name bila jina la mzazi na jina la ukoo!.

Naomba wenye acess na immigration, fatulieni DN ya Mhe. Mwigulu Mchemba muone imeandikwaje, kwa sababu bila jina la mzazi na jina la ukoo mtu huwezi kupata passport kwa majina ya kuokotezwa!.

This is the begining of opening a pandora box, we have to reach to the bottom of this, ila asante sana kujitokeza na kujibu, kwa sababu uwongo, ukisemwa sana na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hugeuka kuwa ni ukweli.

Kwa kuwasaidia wengine wasio jua, hakuna kosa lolote la jinai kujiita jina lolote la bandia na kuitumia popote.

Japo jina la Mwigulu Nchemba ni jina bandia ila vyeti vyake vyote ni vyeti halali.

Kutumia jina bandia, given name sio kosa kisheria na hakuna jinai yoyote! .

Hata mimi Pasco wa JF naweza kuisajili kama Mashokolokubangashe na nikatambulika kama Mashokolokubangashe na vyeti vyangu vyote vikasomeka Mashokolokubangashe na nikawa sijafanya kosa lolote la jinai, ila ikitokea kwenye ujazaji wa fomu zozote za kisheria kama hati ya kusafiria au cheti cha kuzaliwa lazima nitaonyesha majina halisi ya wazazi wangu, na ikitokea kule nako nimejiorodhesha jina la Mashokolokubangashe kuwa ni moja ya majina ya wazazi wangu, then hivyo inageuka forgery, cheating na ni kosa la jinai.

Hivyo natoa wito kwako wanaomtuhumu Mwigulu kudanga wapate uthibitisho toka NIDA na Uhamiaji, watayaona majina halisi wazazi wa Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba.

Finally, wewe mwana Ilboru mwenzangu, ujege mara moja moja humu jf sio mpaka tuu kuja kujibu tuhuma, na ile shule iliokufikisha hapo uikumbukege!.
NB. Tukilimaliza vizuri hili zoezi la vyeti bandia, tunaweza kuamua kuanzisha msako wa wenye majina bandia, na kisha hata kwenye asili za watumishi wa umma, maana kuna a very interesting story ya kijana mmoja wa kabila la Kihaya, mwenye jina la Katto.
Asante.
Pasco
Rejea, kati ya wagombea wote wa urais wa CCM, Mhe. Mwingulu, ndie aliye ni impress sana kuliko wote kwa kuwa the most genuine kumbe...
Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President ...
Na kuhusu Makonda je?
 
Na kuhusu Makonda je?
Alizaliwa DAB, akazungusha, akafoji vyeti vya Paul Christian, ila darasani aliingia yeye, kusoma alisoma yeye, na kuhitimu alihitimu yeye, huyu amefoji jina, na kufoji vyeti, lakini shahada zake zote ni za halali, alipomaliza kuhitimu, akaenda kuapa, kuhalalisha hilo jina, hivyo sasa as we speak, haya ni majina yake halali na vyeti vyake halali.

P.
 
Kuapa Kwa jina bandia ni kosa la kisheria! Sema sheria za bongo zina macho! Zinaona ni nani wa kukomalia na ni nani wa kupotezea!
 
Alizaliwa DAB, akazungusha, akafoji vyeti vya Paul Christian, ila darasani aliingia yeye, kusoma alisoma yeye, na kuhitimu alihitimu yeye, huyu amefoji jina, na kufoji vyeti, lakini shahada zake zote ni za halali, alipomaliza kuhitimu, akaenda kuapa, kuhalalisha hilo jina, hivyo sasa as we speak, haya ni majina yake halali na vyeti vyake halali.

P.
Hicho cha f4? Kama sio chake hiyo ni nini?
 
Hicho cha f4? Kama sio chake hiyo ni nini?
The end always justify the means, ukiweza kufoji jina na cheti, ukaingia chuo kikuu, ukasoma, ukahitimu, then aliyesoma ni wewe na shahada yako ni halali, hata kama mwanzo ulifeli, justification ya kuhitimu chuo kikuu ni kupasi UE na sio uliingiaje, ndio maana hata mtu wa darasa la saba, anaweza kusoma chuo kikuu bila kusoma sekondari.

P
 
Dar mnavyo tumia nguvu nyingi kuwatetea ila mjue Mungu anawaona, nikumbuka figisufigisu za mwigulu wakati sijui katibu mwenezi ni lazima kwenye marudio ya uchaguzi afe mtu, sasa ndio awe rais, nazani sizonje atakuwa cha mtoto, nyie endeleeni kuwafagilia.
 
Back
Top Bottom