Uthibitisho wa uwepo wa MUNGU bila kutumia vitabu vya dini

Uthibitisho wa uwepo wa MUNGU bila kutumia vitabu vya dini

DAN LOKOMOTIVE

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2016
Posts
1,528
Reaction score
1,955
Nimejaribu kuleta mjadala wa kichwa husika hapo juu.tujadili.kwakutumia logic ya kawaida pamoja na laws of nature ilikuonesha uwepo wa Mungu bila kuhusisha kitabu chochote cha dini fuatilia.

Kila kitu kilichopo ulimwenguni kina kuwa na opposite yake mfano uongo kuna ukweli giza kuna mwanga njaa kuna shibe kila kitu kina kinyume chake ,,,sasa hakuna mtu aliyewahi kumouna Mungu wala kuthibitisha lakini kuna nguvu za giza ama uchawi hiyo hata wewe utakua ulisha shuhudia uchawi kuna mambo ya kuuana, vinyongo , kutupiana mapepo na yote haya kila mtu anaproove. Kwa kutumia hii sheria twende sasa.

Sasa turudi kwenye principle yetu kwamba kila kitu kina opposite yake maana yake kuna nguvu opposite inayopingana na nguvu za giza tuiite ''nguvu ya mwanga''hii nguvu ndio Mungu mwenyewe nikimaanisha nini kila kitu ulimwenguni kina asili yake kama kuna asili ya nguvu ya giza basi kuna asili ya nguvu ya mwanga{mungu} ukishaelewa hapo unakuja sasa kwa kutumia nature laws.
Kwamba kila nguvu ama kitendo lazima kibalance ili ulimwengu uendelee ndio maana unaona watu ukitaka kujenga unachimba mchanga uatakata miti hii inamaanisha nini kwamba dunia ama ulimwengu hauwezi kulalia upande mmoja ndio maana tunachukua vya ulimwengu tunavitengeneza ngua, magari kwa hiyo kila kitu lazima kibalance...sasa tunakuja kwenye suala la nguvu za giza na nguvu za mwanga {Mungu} je tujiulize zimebalance.

Kwa kutumia akili ya kawaida kulinganisha nguvu mbili tofauti tunaangalia effects zake ama matokeo yake na maanisha nini kwamba ilikujua gari moja ina uwezo mkubwa kuliko nyingine itabidi zipewe kazi moja ili kuangalia matokeo mfano watazifunga kamba zivutane, au zitawekewa mzigo kuangalia ipi itakua fasta...vivo hivyo kwenye kila kitu ulimwenguni kuanzia simu,computer, wakimbiaji, watu wenye akili, vifaa vya kijeshi n,k.

Sasa turudi kwenye topic kati ya nguvu giza na nguvu mwanga{Mungu} ipi inanguvu tunaangalia effects zake katika maisha ya binadamu tukianza ya giza tumeona tumesikia ikisababisha ajali, magonjwa ,mapepo lakini jiulize je ukilinganisha je ni binadamu wangapi wana mapepo au wameingia katika mtindo wa kinguvu za giza ni wengi lakini huwezi kulinganisha na wasiokua na mapepo au kukumbwa na uchawi. kwa hiyo nguvu mwanga inaonekana kuwa kubwa kuliko nguvu ya giza,

Kama hii nguvu giza ingelikua na effects kubwa kuliko Mungu basi Binadamu wengi tungekua na mapepo ama wachawi. Lakini pia tujiulize kama nguvu giza inakua na masharti tumesikia kuna kafara, namna ya kufanya namna ya kuiomba vile vile nguvu mwanga{Mungu} nayo kuna masharti yake ambayo yanapingana kabisa na mashari ya nguvu giza nguvu mwanga{Mungu) hii ina masharti yake kama kupendana, usimchukie mwenzako, na mengine mengi ambayo opposite na nguvu giza.

Nawasilisha pinga kwa kutumia hoja
 
Ushasikia black holes.. Yanameza mwanga, unasemaje hapo.

Sikia mimi naamini uwepo wa mungu(MUISLAM wa toka nitoke)
Mungu yupo KIIMANI zaidi, uthibitisho wa mungu kuwepo bila kuamini hakuna..
Nguzo tano(misingi inayomfanya mtu aitwe muislam,) ya kwanza kabisa ni kushuhudira kuwa hapana mola apaswae kuabudiwa kwa haki ila yeye allah pekee na Muhammad ndio mjumbe wake kwa ummah huu.

Kisha kuna nguzo za imani
1.Kumuamini Mwenyezi Mungu.
2.Kuamini Malaika wake.
3.Kuamini Vitabu Vyake.
4.Kuamini Mitume Wake.
5.Kuamini siku ya Mwisho.
6.Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu.

Umeona hapo namba moja ni kumuamini mwenyezi mungu.

Sasa mtakuwa mnabishana na maATHEIST mpaka mwisho wa dunia, ila kumthibitishia kuwa 2x+3x=10.. X ni 1, kuthibitisha aone haiwezekani, mungu haonekani.

Sikatazi kuendelea kutoa darsa, ila msiwalazimishe, mungu mwenyewe katika quraan kasema hakuna kulazimishana kwenye dini.
Kuna aya pia nimeisahau anazungumzia pia kuwa haya yanayotokea ni dalili tosha kwa wenye kuzingatia, siijui fikra nimeisahau.

Tueleweshane, Ikishindikana kila mtu atabeba msalaba wake..
Mtume alihangaika na baba yake mdogo weee, lakini wapi, alikuwa na hoja nzito nzito lakini hakutaka kuamini, sana sana alikuwa akimtangazia mchawi, kuna kipindi nafsi inakuwa imeelekea kwenye maovu, hii sisi hatuna jeuri ya kuishitua, haishituki hata mungu mwenyewe atokee na bado atabisha,sana sana anaweza sema no zimwi ama jini

Huu ndio mchango wangu mdogo.
 
Wanaopinga uwepo wa Mungu wangetuambia kwanini viumbe vimekuwa ke na me? Kwanini isingekuwa tu wa aina moja kama ke tu au kama me tu au wawe Hermophradite kisha wakaongezeka kama miti inavyozaa matunda.

Ni natural occurance gani inayotambua iumbe Me au Ke?
 
Back
Top Bottom