Kwenye ulimwengu ambao mchakato wake ni wa vurugu na usio na mpango wala lengo (kama wakana Mungu wanavyodai), hamna nafasi ya kupata ukweli wala maarifa kwani tunakuwa tumefungwa kwenye mchakato wa visababishi vya kimwili (physical determinism).
Yani kama tuchukue kopo tuweke herufi tatu ndani A,B,C tulitingishe kisha tuangalie all the possible combinations, ambazo zitakuwa ni ABC, ACB, BAC, BCA, CAB, CBA. Mtu ataweza kusema combination sahihi hapo ni ipi? Kwa misingi gani mtu aseme ABC ndo sahihi?
Ndo sawa na Ulimwengu huu, kama kilichopo ni matter, space and time peke yake na hakuna kingine kinachoishi nje ya hivi basi hakuna chochote tunachoweza kusema ni cha maana au kweli, kila kitu kinakuwa kweli au kila kitu kinakuwa uongo.
Mawazo yetu yote, hesabu zetu zote, kanuni zetu za mantiki zote ni batili. Ziwe kweli kwa misingi ipi? Wakati tumeishafungwa kwenye mchakato wa visababishi vya kimwili (physical determinism)?
So hata tuseme Mungu yupo, hayupo, kuua ni sawa sio sawa, kutesa wengine ni sawa sio sawa, useme 1+1 =4 na 1+1=2, useme mama yako ana miaka miwili wakati wewe una miaka 40 n.k vyote vinakuwa ukweli au vyote uongo.
Mpaka hapa, tukubaliane kwanza na mkana Mungu kuwa hatuwezi kupata ukweli wa jambo lolote lile ila kutoka kwa chanzo kingine kilicho nje na ambacho hakitegemei ulimwengu huu wa time, space, and matter, ambacho kinasimama thabiti na milele na hakibadiliki, ambacho ndo chanzo chetu cha ufahamu na hata mioyo yetu wote itashuhudia kuwa viwango vyake ni vya kweli na ndo msingi wetu wa kupimia ukweli wa mambo.
(Usomaji wa dakika 25) PRAISE OUR LORD JEHOVAH!!! PRAISE JESUS!!! Whatever name you have for him (him being a symbol for Order), we all recognize him. It took me being a Mum and going through crap to come to this realization. Ikanibidi nikubaliane na maneno niliyasikia kwa Dr. Jordan...