Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

HABARI WAKUU LEO NAANZA KUWAPA UPDATES JUU YA BIASHARA YANGU YA KUCHOMA MAHINDI KAMA NILIVYOWAKILISHA WAZO LANGU KWENYE POST NAMBA 30

Kwanza nimshukuru mleta mada Mr Bonde la Baraka na mfadhili wangu ambae ameniwezesha kiasi ambacho alinipatia Mr Silicon Valley Hongereni kwa mioyo yenu

Biashara nilianza tarehe 9 kutokana na matatzo ya kifamilia ninauguza mdogo wangu hivyo inanibid nitenge muda Wa jioni kifanya biashara hii

Awali nilisema katiaka mchanganuo wangu kuwa nitauza muhindi 1@ sh 800/= lakn nimekutana na changamoto ya ushindani kwan sehemu nayofanya mm biashara pia kuna watu 2 nao wanachoma hvyo imenibid nishushe toka 800 had 600 kwan sokon mhind Mkubwa ulioshiba ni tsh 250-300 hvyo sio mbaya kwa mhindi 1 napata faida ya tsh 300

Biashara bado haijachanganya sana lakn kma hz mvua zitaendelea kunyesha kunyesha mchana na jion kukata kwa sisi wauza mahind huwa muda Wa neema sana

Sehemu nayochoma mahind pia nimeongeza mtaji Wa maji ya kufunga ya mia mia ambayo huwa naweka kwenye dell na barafu hapa kuna jamaa anauza mahind pia hvyo mchana huwa namuachia yeye mm asubh nawah sokon baada ya hapo hospital saa Tisa huwa nakuwa nsharudi naanza mishe za kuchoma Mahindi

Kifupi bado haijachanya biashara ila muelekeo si haba ntawajuza zaidii



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sanaa ndugu na mgonjwa Mungu amsaidie apone Mapema... Pia nashukuru sana kwa kuleta mrejesho, umefanya jambo jema sana kwan watu wengi wanapenda kuona wazo la biashara linatendeka vipi katika mazingira halisi, changamoto zake na namna ya kuzikabili...

Ubarikiwe sana, ufanikiwe vyema!
 


Good..hongera kwa uthubutu..tegemea changamoto zaidi so jiandae kuzikabili shikilia hapo hapo
 
Pamoja sana Mkuu ndio npo mzigon hapa nachakata mda huu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana kwa uthubutu pia pole kwa mgonjwa
La mwsho tunakupongeza kwa kurudi kutuupdate

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
 
Naomba tuingie ubia kiongozi
 
Weka wazo lako tuona kama tutaweza hata kurudisha pesa
I need to do things literally based to my hobby and knowledge.
Some stuff related to Information Techs. I need 1M, Ajira ngumu Connection nazo hakuna With or Without, I have to.
 
Reactions: amu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…