Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Mkuu msaada, hebu elezea jinsi ya kuandika hayo majina,vitu utavotumia na jinsi ya kupatikana kwake nk, nimeipenda hii

Sent using My phone
 
Kuna biashara ya kuuza kuni visiwani(wavuvi)wanaoweka kambi kwa ajili ya kuvua dagaa nikitulia ntakuja niitolee mchanganuo ila 50 ndogo kwa wazo hili

Biashara hii iko hivi,,

Pesa ya kununulia miti( inategemeana bei ya mti na kijiji ulipo) nilipo miti ni kwa 10000 mpaka 20000

Gharama za kukata miti na kuichana ili kupata vipande vya kuni(kama mtu yuko njema kimwili anaweza kufanya mwenyewe ama kutumia mashine yako binafsi kama unayo ni) njia rahisi waweza kukodi mashine (bei ya hapa siijui ila kwa kukadiria haiwezi kuzidi 50,000) kwa miti 50
Mashine nayoizungumzia hapa ni zile zinazokata miti na kuchana mbao zipo ndogo kati na kubwa sina uzoefu na hizi mashine ila naamini wengi tunazifahamu hasa wanaoishi kwenye miji midogo

Gharama nyingine ni ya kusafirisha kuni kwa gari/pikipiki kutokea zilipo mpaka kwenye mwalo tayari kupakia tena kwenye boti mpaka kisiwa husika,, hapa ukipachungulia kuna usafiri mara mbili kwa gari na boti pia kupakia na kupakua( kwa sehemu nilipo zote hizi ni shilingi elfu 80,,,, yaani usafiri tu pasipo ununuzi wa miti ama kukata na kuchana)

Kadirio ni mti mmoja kutoa vipande 50 vya kuni, kwa kuanzia ili kuweza kujaza canter ni wastani wa miti 50 ambapo ukizidisha hapo utapata jumla ya vipande 2500 vya kuni ( wazoefu mnisaidie kujua kama canter kwa pisi 2500 ni mkubwa, mdogo au saizi halisi)

Bei ya kipande kimoja cha kuni visiwani ni shilingi 700-1000

mzigo kama huu kuwa umeisha ni siku 7-10 (ukizoeleka au ukawa na kambi nyingi za kuuzia siku zinapungua hapa nimehesabia siku hizo kwa kambi moja kubwa ama ndogo ndogo 3)

Gharama jumla ni mil 1.3

Mauzo kwa shilingi 700 kwa kipande kimoja kuzidisha 2500= 1,750,000 kuna faida ya shilingi 620,000
Mara nyingi malipo hufanyika mwisho wa giza ama papo hapo inategemea na mazungumzo yako wewe na mteja wako

NB; Kama mashine ni yako gharama zinapungua vilevile faida inapanda

Kama ni nguvu zako mwenyewe kukata mti na kupasua hizi kuni kutokana na wingi basi itakuchukua muda mrefu kuweza kumaliza kazi hivyo kupunguza faida njia hii ni ngumu kuliko ugumu wenyewe

Siko vizuri katika kuandika hesabu za kwenye karatasi tuvumiliane
 
Kuuza Karanga za Kukaanga na Sigara

Mahitaji :

Jiko la mkaa : 3500
sufuria : 5000
pakti : 5000
Mkaa : 1000
Ungo : 2000
Ports : 3400
Embassy : 4300
SM : 3400
Karanga 1kg : 5000

JUMLA : 32,600 (katika 50,000 nitabaki na 17,400 kilinda mfuko)

Karanga nitafunga size 3 tofauti,za 200 za 300 na 500,nitauza mchanganyiko mbichi na za kukaanga mteja atachagua yeye anataka pakti gani.

Hii biashara nina uwezo wa income ya faida above 5000 per day x 30 = 150,000,hapo ni karanga tu,sijapiga hesabu ya sigara. Hiyo 50,000 yako nina uhakika ndani ya mwezi itakua imerudi mkuu.

NOTE :

natoa mawazo Bure kabisa ila mkopo huo apewe mwingine,wapo wengi waliochini wanatamani kuinuka,nikisema nikomae nipate hiyo 50,000 kwakweli yawezekana nitaipata ila Hapana sipo tayari kudhulumu nafasi mwingine.

Hongera kwa wazo lako la kusaidia wengine,naamini kila ataepita kwenye hii thread atapata chochote kitu hata kama hatopata huo mkopo ila hatatoka Bure.
 
Safi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
DAAH MKUU UMETISHA

Hii ndio biashara kiukweli kuna mdau anasema hii kaz inatakiwa uache aibu kuna jamaa Yangu anifanya hii ndio inamuweka mjin na familia inapata mahtj yote kupitia biashara hii

Kama jamii forums ingekuwa hvi kusaidiana tungefka mbali sana elfu 50 inaonekana ndogo lkn unaweza ukaifanya iwe million kama utakuwa na mipango mizur katika biashara na tatzo La ajira linvekuwa historia

WITO WANGU wadau jitokezen ili tuwainue vijana hapa jamii forums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wa matolori, wewe ni Master wa biashara ndogo ndogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alichosema ni ukweli mtupu...shida yetu iko hapo hatufikirii na changamoto na hatuko tayari kuzikabili!
Ukifikiria sana changamoto hakuna biashara utafanya. Be positive minded, ukishaingia kwenye game utapambana nazo.

Faida na hasara ni vitu vya kawaida, kikubwa usikate tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu naendelea kukupa kongole

uko real sana bila kumsahau

Zero IQ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu mbona Mo hayo mnayoyasema anayafanya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alichosema ni ukweli mtupu...shida yetu iko hapo hatufikirii na changamoto na hatuko tayari kuzikabili!
uko sahihi vijana wajaribu kufikiria zaid kuhusu challenge kuliko faida

maana naona mawazo mazur lakin wanapiga zaid maximum profit ila hawazungumzii challenge na navojua mm business nyingi huwa na challenge nyingi hasa mwanzon

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…