Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Kwa mtaji huo boss mito ya baraka unapendeza kwa biashara ndogo ndogo.
Mimi nitafanya hivi:

Nitanunua cakes zile zinazokaa 10pcs per dozen then nanua creams zinazotumika kuandika kwenye cakes.

So hapa kila pc naandika jina la mteja au ujumbe mfupi atakao taka mteja.
Hii biashara nitifanyia maeneo ya shule ya msingi.

Japo sijaweka mchanganuo wa costs but Tzs 50k inatosha.

NB
Keki hizi ni zile zenye vikaratasi zinauzwa sana kwenye terminal
Mkuu msaada, hebu elezea jinsi ya kuandika hayo majina,vitu utavotumia na jinsi ya kupatikana kwake nk, nimeipenda hii

Sent using My phone
 
Kuna biashara ya kuuza kuni visiwani(wavuvi)wanaoweka kambi kwa ajili ya kuvua dagaa nikitulia ntakuja niitolee mchanganuo ila 50 ndogo kwa wazo hili

Biashara hii iko hivi,,

Pesa ya kununulia miti( inategemeana bei ya mti na kijiji ulipo) nilipo miti ni kwa 10000 mpaka 20000

Gharama za kukata miti na kuichana ili kupata vipande vya kuni(kama mtu yuko njema kimwili anaweza kufanya mwenyewe ama kutumia mashine yako binafsi kama unayo ni) njia rahisi waweza kukodi mashine (bei ya hapa siijui ila kwa kukadiria haiwezi kuzidi 50,000) kwa miti 50
Mashine nayoizungumzia hapa ni zile zinazokata miti na kuchana mbao zipo ndogo kati na kubwa sina uzoefu na hizi mashine ila naamini wengi tunazifahamu hasa wanaoishi kwenye miji midogo

Gharama nyingine ni ya kusafirisha kuni kwa gari/pikipiki kutokea zilipo mpaka kwenye mwalo tayari kupakia tena kwenye boti mpaka kisiwa husika,, hapa ukipachungulia kuna usafiri mara mbili kwa gari na boti pia kupakia na kupakua( kwa sehemu nilipo zote hizi ni shilingi elfu 80,,,, yaani usafiri tu pasipo ununuzi wa miti ama kukata na kuchana)

Kadirio ni mti mmoja kutoa vipande 50 vya kuni, kwa kuanzia ili kuweza kujaza canter ni wastani wa miti 50 ambapo ukizidisha hapo utapata jumla ya vipande 2500 vya kuni ( wazoefu mnisaidie kujua kama canter kwa pisi 2500 ni mkubwa, mdogo au saizi halisi)

Bei ya kipande kimoja cha kuni visiwani ni shilingi 700-1000

mzigo kama huu kuwa umeisha ni siku 7-10 (ukizoeleka au ukawa na kambi nyingi za kuuzia siku zinapungua hapa nimehesabia siku hizo kwa kambi moja kubwa ama ndogo ndogo 3)

Gharama jumla ni mil 1.3

Mauzo kwa shilingi 700 kwa kipande kimoja kuzidisha 2500= 1,750,000 kuna faida ya shilingi 620,000
Mara nyingi malipo hufanyika mwisho wa giza ama papo hapo inategemea na mazungumzo yako wewe na mteja wako

NB; Kama mashine ni yako gharama zinapungua vilevile faida inapanda

Kama ni nguvu zako mwenyewe kukata mti na kupasua hizi kuni kutokana na wingi basi itakuchukua muda mrefu kuweza kumaliza kazi hivyo kupunguza faida njia hii ni ngumu kuliko ugumu wenyewe

Siko vizuri katika kuandika hesabu za kwenye karatasi tuvumiliane
 
Kuuza Karanga za Kukaanga na Sigara

Mahitaji :

Jiko la mkaa : 3500
sufuria : 5000
pakti : 5000
Mkaa : 1000
Ungo : 2000
Ports : 3400
Embassy : 4300
SM : 3400
Karanga 1kg : 5000

JUMLA : 32,600 (katika 50,000 nitabaki na 17,400 kilinda mfuko)

Karanga nitafunga size 3 tofauti,za 200 za 300 na 500,nitauza mchanganyiko mbichi na za kukaanga mteja atachagua yeye anataka pakti gani.

Hii biashara nina uwezo wa income ya faida above 5000 per day x 30 = 150,000,hapo ni karanga tu,sijapiga hesabu ya sigara. Hiyo 50,000 yako nina uhakika ndani ya mwezi itakua imerudi mkuu.

NOTE :

natoa mawazo Bure kabisa ila mkopo huo apewe mwingine,wapo wengi waliochini wanatamani kuinuka,nikisema nikomae nipate hiyo 50,000 kwakweli yawezekana nitaipata ila Hapana sipo tayari kudhulumu nafasi mwingine.

Hongera kwa wazo lako la kusaidia wengine,naamini kila ataepita kwenye hii thread atapata chochote kitu hata kama hatopata huo mkopo ila hatatoka Bure.
 
Safi
Hiyo elfu 50 mchanganuo, wake kwa biashara ya mishikaki.

Naenda kwa Fundi kuchomelea aniandalie Jiko elfu 25,

Natafuta kijiwe kizuri sehemu wanayopita watu wengi,

--Sokoni nyama kg 2 steki tupu =16000,
--mkaa wa 1500
-Viungo vyake 5000(hiyo siyo vya siku moja ukinunua ni vingi mpaka viishe vitakaa kaa kidogo. )
-vijiti vile vistiki vyake 2000.

Naandaa mishikaki yangu ya wastani tu ya kuuza mia 2 mia 2 tu,

Kwenye kg 2 nina uhakika wa kupata faida ya 10K kila siku hapo baada ya kutoa matumizi ya mkaa, vijiti na Nyama.

Ndani ya wiki tayari nimekurudishia 50k yako.


NB:
Nilishawahi kufanya hii kazi hivyo nina uhakika nayo. Ndio kazi iliyonipa mtaji wa kibanda cha kuchakata viazi kuwa Chips.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nitaigawa hio 50,000 mara 50 ili nipate elfu 1..

Kwakua hii week ninya Uefa na Europa nitaweka mikeka 25 kwa umakini mkubwa na uchambuzi wa hali ya juu.. mwisho wa week nitakuwa na pesa ambayo sio chini ya 150k.

Ile 25k iliyobaki ambayo sikuweka mkeka itakuwa kama plan B incase mikeka ikifeli yoote..
Hii 25k nitanunua unga wa ngano na mafuta nitengeneze maandazi na chapati (nina hiki kipaji cha kupika) nitayapeleka haya maandazi na chapati weekend kwenye hostel za wanachuo (weekend wengi wanaona uvivu kuamka asubuhi kununua chai ) .. nitawasambazia maandazi hayo hadi saa 6 mchana na pesa yangu itakuwa imerudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Mkuu

Mimi nitaitumia 50000/= katika mchanganuo ufuatao kupitia biashara ya mahindi ya kuchoma

Naishi temeke stereo jirani na soko hapo wanauza mahindi mabichi nami ndiyo biashara niliyowah kuifanya Tandika sokoni

Mchanganuo
Mahindi 50@300= 15000
Usafiri = 500
Mkaa. = 1500
Chumvi. = 300
Ndimu. = 300
Ushuru. = 500
Pilipili. = 300

JUMLA. 18900


MAUZO

Nitauza mhindi 1 kwa shilingi 800 hiyo kwa mahindi 50 kwa siku n shilingi ( 50×800= 40000)

jiko ninalo hivyo sihitaji kununua

JUMLA YA MAUZO - JUMLA YA MCHANGANUO.


40000 - 18900= 21100

kwa hyo ninauhakika wa kurudi na elfu 21100 kila siku kumbuka situmii nauli kurudi nyumbani

Ninauwezo wa kuuza mahindi 50 kwa sababu Tandika n sehemu ambayo inawatu wengi ni soko kubwa hvyo mwingiliano wa watu ni Mkubwa

Baada ya siku 7 ninauwezo wa kuwa na shilingi 147700

Pia kumbuka katika elfu 50 ya mtaji baada ya matumizi ya siku ya kwanza ilibaki (50000-18900= 31100) itabaki shilingi 31100 nitaitumia kuongeza mtaji taratibu kwa siku zinazofuata maana biashara sio siku zote huwa nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
DAAH MKUU UMETISHA

Hii ndio biashara kiukweli kuna mdau anasema hii kaz inatakiwa uache aibu kuna jamaa Yangu anifanya hii ndio inamuweka mjin na familia inapata mahtj yote kupitia biashara hii

Kama jamii forums ingekuwa hvi kusaidiana tungefka mbali sana elfu 50 inaonekana ndogo lkn unaweza ukaifanya iwe million kama utakuwa na mipango mizur katika biashara na tatzo La ajira linvekuwa historia

WITO WANGU wadau jitokezen ili tuwainue vijana hapa jamii forums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BIASHARA YA KUCHOMA MAHINDI

Mahitaji :

Jiko = 20,000
Mkaa (chenga mixer) = 3000
Wavu = 5000
Nauli = 2000
Mahindi = 10,000
Ndimu = 1000
Chumvi = 3000
Kiroba (cha kufatia mahindi) = 2000

TOTAL = 46,000

Kwenye ile 50,000 nitakua nimebakiwa na 4000,ambayo hii hela itakua ni pesa yangu ya kula na maji kama nikisikia kiu nikiwa kazini.

Mahindi sokoni yanauzwa 200-300,mimi nitachukua mahndi mchanganyiko nitachanganya ya 300 na 200 Jumla nitapata si chini ya mahindi 35 kwenda mbele.

Nitakuja kuchoma mahindi yangu na katika muhindi 1 wa 300 nitatoa vipande vi 3 vya kuuza 300(kipande),maana yake muhindi wa 300 utanipa 900 (toa 300 = 600 Faida)

Hii 600 Mungu akasaidia nikauza mahindi yangu 35 nitakua na 600 x 35 = 21,000

21,000 - 10,000 (mtaji) = 11,000

Kesho nitafata mahindi yangu tena ya 10,000 + 2000 (nauli) = 9000

9000 X 30 = 270,000 (kwa mwezi)

Mwisho wa mwezi nitarudisha 50,000 yako kisha nitabaki na mtaji wa 220,000,kisha nitaendelea na biashara yangu ya kuchoma mahindi.Muda huu sitokua nanunua mahindi ya 10,000 nitakua nimeji ongeza nitafata mzigo wa mahindi hata ya 20k-30k.

Nafata mahndi kidogo ili yaishe kwani mahindi yakiwa mengi yakichelewa kuisha(yakabaki) hukauka na kuwa magumu wakati wa kuchoma wateja hawatoyapenda na wateja wengi wa sasa hupendelea mahindi ya kuchoma malaini.

MWISHO nitakushukuru kwa msaada wako na Sitoacha kurudi JamiiForums kutoa asante zangu kwa kunikutanisha nawe.

wako katika ujenzi wa TAIFA

CONTROLA
Mzee wa matolori, wewe ni Master wa biashara ndogo ndogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alichosema ni ukweli mtupu...shida yetu iko hapo hatufikirii na changamoto na hatuko tayari kuzikabili!
Ukifikiria sana changamoto hakuna biashara utafanya. Be positive minded, ukishaingia kwenye game utapambana nazo.

Faida na hasara ni vitu vya kawaida, kikubwa usikate tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili wazo lenye uhalisia sana na ndio ninaloliendea sasahivi, labda uwe umejikita kwenye biashara za kuzalisha si zakutoa Huduma maana wote naona wanaleta mawazo yakuzalisha.

Hii ni FREE CARWASH
_Naoshea maeneo ya posta hiyo 50,000/= inafikishwaa kwa siku 2 cash as profit na siku kama ya leo na kesho magari yapo full packed na wengi wametoka kuuatumia siku za weekend hata kwasiku moja if Odds in my side that day.

MCHANGANUO
_Hii biashara ipo hivi gari unaosha kwa 2000/= mpaka 10,000/= inategemea umemuoshea nani maana wanaosha mpaka ma Range Rover, V8 sasa mtu ukimuoshea anakupa tu “chukua hii 8000/= Nipigie maji” unajikuta kwa siku mbaya 30,000/= kawaida.

ENEO LA BIASHARA
_Posta maeneo ya Golden jebelee tower, kuna ofisi nyingi kubwa maeneo ya nje ndio inapofanyika Huduma hii ubaazi wa SERENA HOTEL unaosha magari non-stop kutwa mzima.

MTAJI
_Hii biashara haitaji Mtaji mkubwa kwasababu unahitaji vifaa ambayo madumu na vitambaa ILA kwenye inabidi ujiunge kwenye kikundi kwa 70,000/= hili uwe mwanachama nishawapa 20,000/= ndio nahaso iyo 50,000/= niwakamilishie.
_kwa kuongeza thamani ya Huduma nanunua matauro meupe, mafuta Air freshener, Polish ya dash board n.k ili kumfurahisha zaidi mteja hii itafanya niweze kumpandishia bei mteja na kupata faida maradufu.

UHALISIA
_Leo ndio natoka kuwapa 20,000/= nakupeleka dumu zangu asubui tu hata SAA 2 bado wakaamua wanipe nauri yakurudi kwakupewa gari moja nioshe nimekula 5000/= cash hiyo kabla ya saa 2 ijafika imagine kutwa nzima.

So, kwahuwo Mtaji wa 50,000/= ambao kwangu ni mtaji wa kujiunga uwanachama na kuonheza matauro na mafuta siku 2 tu naitengeneza.

NB: hii dunia ya leo mawazo ya kutoa Huduma yanapesa hata ukianza chini.

IDEA IN PROGRESS...NEED BACKUP CAPITAL

CONT : 0716321462

Faida kabla saa 2 leo.View attachment 1360449

Vifaa vya kazi
View attachment 1360451

Portfolio | 2020
mkuu naendelea kukupa kongole

uko real sana bila kumsahau

Zero IQ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja MaBillionaire ni watu wa hovyo kabisa.

How come, MO ana utajiri wa Trillion 4 roundly hivi akitenga only 1B tu sawa na million 1000/= akawawezesha vijana kwa vigezo purposefully 1M kila mmoja sawa na vijana 1000 Tz kwa 1B moja tu ambayo haitekenyi hata itajiri wake Hell.

Hell.

Portfolio | 2020
mkuu mbona Mo hayo mnayoyasema anayafanya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alichosema ni ukweli mtupu...shida yetu iko hapo hatufikirii na changamoto na hatuko tayari kuzikabili!
uko sahihi vijana wajaribu kufikiria zaid kuhusu challenge kuliko faida

maana naona mawazo mazur lakin wanapiga zaid maximum profit ila hawazungumzii challenge na navojua mm business nyingi huwa na challenge nyingi hasa mwanzon

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom