Mkuu kwa sasa nafikiria kupata fedha kiasi kadhaa niboreshe hilo wazo,
Kwanza nataka niuze mishikaki vizuri siyo local tena kama mwanzo,
Nataka nitafute sehemu nzuri niweke meza flani hivi nilishadizine,
Then kwa juu naweka katent flani hivi na bango kubwaa,
Hapo itakuwa ni mishikaki ya Nundu plus Nyama ,
Then pembeni kutakuwa na ndizi za kuchoma pamoja na kukaanga ,chachandu flani hivi ya kuvutia,
Mavazi ,nitakuwa na mavazi flani special Tshirt ya kuprint yenye logal mbele na maandishi Nyuma,chini laba flani hivi na jinsi Nyeusi ya kuchomekea(lengo kuwa Nadhifu muda wote wa kazi)
Nje ya meza kutakuwa na Viti vya kudizine vitakavyowezesha kukaa watu nane tu (kila upande watu wanne,)
Yaani nataka niifanye kiaina flani hivi ambayo ata wewe mwenye Suti yako usione Aibu kushuka kwenye gari yako kuja kununua mishikaki ,
hapo kwa haraka haraka mchanganuo wangu mpaka sasa ulikuwa hivi.
Hiyo meza niliyodizine nilishaongea na fundi inacost kama 300k (ni ya chuma alafu itakuwa na umbo kama L )
Carpet yake ya kutandika meza (vile ninavyotaka mimi)35.
Majiko mawili 80k (kubwa 45k, dogo la karahi 35k)
Karahi 1. 9k
Meza na viti vile navyotaka kudizine vitanicost 150k,
Chuma nne za kusimama 120k (kila moja 30k)
Za juu 40k ,turubahi la kuweka 30k (hapo tent ) fundi sijajua bado
So hapo kwa haraka haraka 800k - 900k inatosha Biashara itakuwa kama vile ninavyotaka mimi,
Nilishaweka kiasi kadhaa na bado nazidi kuweka Akiba, wazo langu halina haraka sana nategemea kuanza ikifika mwezi wa Sita hivi ,
Eneo ninalotegemea kuweka ni mapito ya watu wa aina tofauti
Biashara yenyewe.
Nitakapoanza biashara nategemea kuanza kwa bei ya kawaida tu ,
Kila mshikaki utauzwa shilingi 500,
Ndizi ya kuchoma shilingi 500,
Na ndizi ya kukaanga shilingi 400,
Pembeni ya jiko kutakuwa na mishikaki pia midogo ya shilingi mia 2, mia 2 kwa ajiri ya wanafunzi na watoto.
Ongezeko la bidhaa itaongezeka kulingana na ongezeko la wateja watakaokuwa wanakuja mfano.
Naweza kuweka mihogo,maziwa fresh kwa Jioni, maini na firigisi za kuku Nk.
ila tu sitaweka chipsi nataka nidili na hivyo Vitu tu na nitasimamia mwenyewe.
Nb.
Kwenye banda langu la kiepe kama kawa watu wapo wa kufanya kazi mimi binafsi nataka nigeukie huko kwanza
Cc Zero IQ
Sent using
Jamii Forums mobile app