Utiaji saini Mikataba ya DP World: Hakukuwa na haja ya kuwatupia vijembe TEC

Utiaji saini Mikataba ya DP World: Hakukuwa na haja ya kuwatupia vijembe TEC

Waarabu wametumia pesa ya mafuta na TEC wakatumia ushawishi wa kanisa kutokea vatican.
Pesa ikaelea juu ya maji na ushawishi wa kukomboa mateka ukazama chini ya maji.
Maana yake ni moja kuu,
Masikini hana hiari linapokuja suala la uhitaji wa mlo.
Hajui kama kesho yake utapatikana mlo hivyo hula kilafi leo hata kama ameshiba.
Hii ni kukaba penalty ambayo kikanuni ni kosa.
Hivi ndivyo watanzania tumeiuza haki yetu ya uzaliwa wa kwanza katika ardhi yetu kwa waarabu.

Ona hili bado linaganda mawazo ya nyuma [emoji23]wenzio washabadili gia we bdo umeachwa na masuala ya kuuzwa nchi
 
Halikuwa jambo la kiungwana. Wahusika mnisikie na kunielewa. Jana, pale Ikulu Chamwino kwenye utiaji saini mikataba mitatu ya uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kati ya Serikali/TPA na DP World vilirushwa vijembe kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Tuliofuatilia tunajua kuwa pale ukumbini alikuwepo Askofu Liberatus Sangu kama mwakilishi wa TEC. Wahusika mkaanza kumtumia Mrisho Mpoto kurusha vijembe. Badala ya kughani au kuimba kama ilivyotarajiwa, Mpoto alitoa hotuba na kutamba alivyotaka.

Akadai kuwa kwakuwa mikataba sasa iko vizuri 'hata waliokuwa wanapinga wamehudhuria pale na watakula nao chakula'. Kila mmoja anajua kuwa waliotoa Tamko ni TEC. Na jana walikuwepo pale. Kwanini uwepo wao uonekane ni kuunga mkono mikataba iliyosainiwa jana?

Kiukweli, vijembe vya Mpoto na wengineo vilimkosesha amani na utulivu Askofu Sangu. Akajiweka 'busy' na kuchukua 'notes' huku akishindwa hata kuwatazama wazungumzaji au majirani zake. Askofu Sangu alikuwa kwenye wakati mgumu. Hakukuwa na haja ya mambo yale.

Kama maoni ya watanzania yamezingatiwa, tuonesheni mikataba iliyosainiwa jana!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mpwapwa, Dodoma)
Subiri matusi kwa wafia dini
 
Waeza kujiona una weruvu kwa kuamini kitu ila usiwe sahihi
Wamesema wameubadili?
Uliambiwa mkataba ni wa milele lakin kipengele cha muda ukuona
Afu leo unajipa moyo kua umebdilishwa [emoji23]
Wanaposema muda ni miaka 30 unaelewa nini?
 
Turudie, ni ushindi wa TEC na ndiyo maana wakakaribishwa kushuhudia uangushaji wa wino.
Huu ujinga wa kuchagua upande kwenye maslahi mapana ya taifa mtaacha lini?Kwani walioalikwa ni hao tu uliowataja?Waalikwa wengine hawahusiki?Mnajipa umuhimu wakati mlipinga?
 
Halikuwa jambo la kiungwana. Wahusika mnisikie na kunielewa. Jana, pale Ikulu Chamwino kwenye utiaji saini mikataba mitatu ya uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kati ya Serikali/TPA na DP World vilirushwa vijembe kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Tuliofuatilia tunajua kuwa pale ukumbini alikuwepo Askofu Liberatus Sangu kama mwakilishi wa TEC. Wahusika mkaanza kumtumia Mrisho Mpoto kurusha vijembe. Badala ya kughani au kuimba kama ilivyotarajiwa, Mpoto alitoa hotuba na kutamba alivyotaka.

Akadai kuwa kwakuwa mikataba sasa iko vizuri 'hata waliokuwa wanapinga wamehudhuria pale na watakula nao chakula'. Kila mmoja anajua kuwa waliotoa Tamko ni TEC. Na jana walikuwepo pale. Kwanini uwepo wao uonekane ni kuunga mkono mikataba iliyosainiwa jana?

Kiukweli, vijembe vya Mpoto na wengineo vilimkosesha amani na utulivu Askofu Sangu. Akajiweka 'busy' na kuchukua 'notes' huku akishindwa hata kuwatazama wazungumzaji au majirani zake. Askofu Sangu alikuwa kwenye wakati mgumu. Hakukuwa na haja ya mambo yale.

Kama maoni ya watanzania yamezingatiwa, tuonesheni mikataba iliyosainiwa jana!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mpwapwa, Dodoma)
Mkuu

kilichofanyika Ikulu ni utapeli mwingine kama kawaida yao. TICTS ilipewa mktaba wa miaka 20 plus na walikuwa tathimini kila baada ya miaka mitano lakini ufanisi ulikuwa haukidhi je, waliwatoa wakati walifikisha mpaka miaka 22?

Hakuna cha maana kitakachowanufaisha wananchi hapo eti watawanyanyua wananchi masikini wapatao milioni 15 kupitia mapato ya bandari.....are you fox serious?
 
Kwa mtazamo wangu hili jambo limekuwa la kidini zaidi badala ya kuangalia maslahi ya Taifa.

Kuna watu wanalazimisha wawekezaji kwa kuangalia origin yao.
 
Kwa mtazamo wangu hili jambo limekuwa la kidini zaidi badala ya kuangalia maslahi ya Taifa.

Kuna watu wanalazimisha wawekezaji kwa kuangalia origin yao.
Na kuna watu hawataki wawekezaji kwa kuangalia origin yao na hili kundi limepofuka kwa udini uliokithiri.
 
Na kuna watu hawataki wawekezaji kwa kuangalia origin yao na hili kundi limepofuka kwa udini uliokithiri.
Yaani imekua shida tupu.

Tunaaminishwa wawekezaji wanauwezo mkubwa kisa tu ni waislamu na wanaopinga basi wanaambiwa wanawakataa wawekezaji kwakua wao ni wakristo na hawapendi waislamu.

Ila historia ni shahidi Mzuri ipo siku tutaongea lugha moja kuhusiana na performance ya hawa jamaa.
 
Hakuna anayedai wana uwezo kwa sababu ni waislamu bali wanaunga mkono kwa sababu wanaopinga wanapinga kwa sababu TU wawekezaji ni waislamu na sio uwezo wao kiutendaji.Propoganda za kijinga kwa sababu DP World wapo na wanaendesha bandari kwenye Nchi nyingi duniani zilizoendelea kuliko sisi.
 
Pongezi nyingi kwa TEC tumeona juhudi kubwa mlizofanya mpaka kukamilisha vyema suala nyeti la bandari
 
Huu ujinga wa kuchagua upande kwenye maslahi mapana ya taifa mtaacha lini?Kwani walioalikwa ni hao tu uliowataja?Waalikwa wengine hawahusiki?Mnajipa umuhimu wakati mlipinga?
Mkuu mimi siyo mjinga. Wamekaribishwa wengi. Hoja yangu ni kuwa TEC wamekaribishwa kwa sababu ya mchango wao. All things being equal ni mchango wa TEC uliokuwa unaeleweka na ni public.
 
Back
Top Bottom