Utiaji saini Mikataba ya DP World: Hakukuwa na haja ya kuwatupia vijembe TEC

Utiaji saini Mikataba ya DP World: Hakukuwa na haja ya kuwatupia vijembe TEC

Kwa mtazamo wangu hili jambo limekuwa la kidini zaidi badala ya kuangalia maslahi ya Taifa.

Kuna watu wanalazimisha wawekezaji kwa kuangalia origin yao.
Na sharti la waarabu ni kujenga misikiti eneo la kazi na haya wanaweza lazimisha huku Afrika tu na si ulaya,amerika...jiulize kama kisheria petrol station hakutakiwi msongamano wa watu inakuwaje misikiti inafumbiwa macho kujengwa?Kuna nguvu kubwa sana ya upotoshoji wa kiimani na sidhani kama hawajui.
 
Tusubirini kauli ya TEC, naamini wataongea kitu, kushuhudia utiaji saini haimahanishi kuwa TEC wameridhia 100% mara nyingine hukudhuria hafla kama hizi huwa ni 'protocol' huwezi kualikwa ukakataa, itakuwa kuigomea serikali wakati bado una maslahi mengi kwao!
Hakika itapendeza wakitoka kauli.

Kuna mahali nimesoma kwamba wamekubaliana kidogo😄

Baada ya sintofahamu nyingi waliitwa wote waliokuwa na hoja na maoni wakarekebisha ndio kimetokeza hicho kilichotokea japo nahisi bado kuna dosari.

Wanaowabeza kuhudhuria hafla hawajua mambo ya protol
 
TEC ilikwishatoa TAMKO hata mkiendelea kuwabembeleza haitasaidia.
 
Yaani unalinganisha petrol station na misikiti?Kweli uwezo wako wa kufikiri umekufikisha hapo?Yaani hujui kwanini petrol station hairuhusiwi kujengwa kwenye maeneo ya watu wengi?
 
Hili ndio tatizo la CCM kupenda kualika manunda na mahayawani kwa ajili ya kutukana, kukebehi na kupuuza wengine tena wenye akili nyingi kuliko wao! Ni tabia hovyo sana na hulka ya watu mufilisi vichwani.
 
Nimeangalia clip moja humu mitandaoni nimeshangaa Sana!! Na Kwa akili hizi sijui nchi imefikia wapi!?

Msanii jina limenitoka ( ila Huwa namuona anatembea pekua) ,amealikuwa kwenye kikao Cha NEC, anaosikia akiwashambukia na kuwakebehi wazi wazi NEC, ambao wakitoa maoni tofauti kuhusu mkataba wa bandari, msanii huyo alishangiliwa na kuchangiwa " manoti ya kutosha!?

Alisikika akisema"walioupinga mkataba huu wamo humu na wameitikia mwaliko wako na tutakula nao chakula Cha mchana!!"

Hakika binafsi sikupenda kauli za kebehi namna hii!! Hili linawezewa likasababisha Wakati mwingine mualiko wa Mh Rais ukasusiwa na watu wenye mawazo tofauti.

Sidhani kama msanii huyu kakurupuka ,la hasha!! Ilakuwa katumwa kuwadhihaki hawa viongozi tena Kwa chakula!?

Poleni TEC! Hii ndio CCM
 
Back
Top Bottom