Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Nisiwachoshe sana.
Kataa CCM kwani inamiliki jeshi, polisi na TISS kwa maslahi yake na si ya nchi...
Msanii
- Matukio ya watu kupotea ndani mikono ya polisi.
- Matukio ya watuhumiwa kuteswa na kutwezwa wakihojiwa na polisi
- Matukio ya mauaji ndani ya vituo vya polisi ni mengi
- Matukio ya watu kutekwa na vyombo vya dola kisha kutoweka ni mengi
- Matukio ya kutishia wakosoaji na kuwabambika kesi ili kuwanyamazisha ni mengi
- Dhamana ya kutoka mahabusu ya polisi ni baada ya rushwa na kuzungushwa
- Sasa unakuta, polisi wanatuma barua ya wito na raia anatii wito bila shuruti lakini anapofika kituo cha polisi anashughulikiwa kama mhalifu na si mtuhumiwa
- Usiitikie wito wa polisi ukiwa peke yako. Nenda na ndugu aua jamaa waliobeba dhamana.
- Usikubali kuitikia wito wa polisi siku ya ijumaa maana wana mpango wa kukulaza ndani hadi jumatatu
- Polisi wanapokuja kukukamata eneo lolote hakikisha PGO inahusika na watu wanaokuhusu wajulishe hapo hapo kabla hamjaenda kituoni.
- Polisi yeyote mkamataji arekodiwe namba yake na jina lake. Pia tumia smart phone kumpiga picha na kutuma kwa jamaa zako ama waachie simu zako ili viwe ushahidi
- Akija mtu kukukamata na akajitambulisha ni polisi huku akigomea kutoa utambulisho wake, piga kelele kuomba msaada maana huyo ni muuaji kama wauaji wengine
- Hakikisha unajiweka mbali na jirani ambaye ni polisi. Polisi wengi ni wasaliti wa raia na siyo walinzi wa raia na mali zao
- Unapokuwa kituo cha polisi kufuatilia dhamana ya jamaa yako hakikisha unawarekodi polisi wanaozungumza nawe kuhusu jamaa ama nduguyo
- Vujisha taarifa za changamoto za polisi hapo kituoni kwa jamii ama watu wa karibu ili hatua zichukuliwe
- Usimuamini polisi yeyote na usiamini uwapo mikononi mwa polisi kuwa upo salama
- Kwenye simu yako weka S.O.S. namba za watu watatu unaoamini wanathamini uwepo wako.
Kataa CCM kwani inamiliki jeshi, polisi na TISS kwa maslahi yake na si ya nchi...
Msanii