hivi ww mbona mkuda sana, unakereka nini mtu kuchangia harusi! Hayo ni matumizi yake halali ya hela yake mwenyewe mwalimu vipi? Ni maamuzi yake huru, na haimaanishi kwa kuwa kachangia harusi basi umuibie kwa kumuwekea mcchango usiokuwa na mbele wala nyuma.
Ww mwenyewe ulichangiwa harusi, au umesahau ulivyokuwa unabembeleza watu wakuchangie na ulivyoweka bifu na wale walioshindwa kukuchangia!
swala siyo 200 bali ni kero inayoambatana na michango ya kinyemela isiyoratibiwa. Unataka kusema kwa sasa shule hazina fungu la kuwezesha wanafunzi kutahiniwa. Yaani ktk hayo ma 'trilioni' yaliyotakiwa kupelekwa mashuleni hakuna badget ya majaribio?
Kama hivyo ndivyo basi waziweke kwenye ada tutatoa lakini siyo wizi wa kupumbafu huu wanaofanya na kuwasumbua watoto wetu hata kuwachapa!
ww una mtindio wa ubongo ww! Aliyekuambia huwezi kutoa jaribio ubaoni na wanafunzi wakaandika kwenye daftari maalumu la majaribio ni nani vile! Hakuna cha photocopy wa bibie copy hapo huu ni upigaji mpya, na ni wizi kama ulivyo wizi mwingine!
Isitoshe ili kuhakikisha kuwa lengo la mchango siyo kumpima mtoto unakuta majaribio yenyewe yanafanyika ili liende na hakuna tija ktk hayo majaribio!
Yaani uandike jaribio ubaoni?
Hiyo itakua ni exercise au jaribio?
Au itakua ni Quiz na sio jaribio
Huko mashuleni kuna hali mbaya sana huwezi amka from no where unasema nataka nitoe copy niwape wanafunzi jaribio
Utaambiwa pepar za printing hamna au utaambiwa wino umeisha au utaambiwa wasubili midterm au terminal
Sasa wewe kama mwalim huwezi subili paka midterm lazima utafute alternative wanafunzi wafanye jaribio
Yaani ndio maana private school zitazidi kuongoza kuliko shule za umma
Maana mambo yenyewe ndio hayo sasa mzazi analalamika sh.200 ya jaribio[emoji23][emoji23].
Nyie ndio wazazi mkiitwa na uongozi wa shule jaman hakuna mwalim wa somo fulani pengne Physics au mathematics mkiambiwa changieni hata 1000 kila mwezi kwa kila mzazi ili mtafutiwe walimu wa kusaidia watoto wenu mnabaki mnalalamika.
Mnabaki msubili paka serikali iajiri
Hapo anaeumia ni pengne mtoto wako na sio serikali.
So ni the same to hayo majaribio mwalimu hawezi kaa kujitesa kuandika ubaoni
Kwanza akiandika ubaoni kuna vitu kwenye jaribio kama alitaka viwepo anaweza kuviskip maana unaweza andika ubao mzima na usitoshe
Kutokana na ulichotaka kupima