Utitiri wa michezo ya ubashiri kwenye vyombo vya habari

Utitiri wa michezo ya ubashiri kwenye vyombo vya habari

Dr PL

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2024
Posts
688
Reaction score
1,039
Kumekuwa na michezo mingi sana ya ubashiri kwenye vyombo vingi vya habari hasa redio na television.

Michezo hii imepewa majina mbalimbali kulingana na chombo cha habari husika, mfano:
-Pakua mkwanja
-Cheza pesa
-Mshiko faster
-Pesa mkwanja nk

Hata hivyo mtindo wa uchezaji ni mmoja (utofauti ni majina tu) ambapo watu hucheza au hubashiri kupitia mitandao yote ya simu kwa kutoa kiwango cha Tsh. 1,000/- tu.

Vyombo vingi vya habari hasa redio huendesha michezo hiyo muda wote, yaani katika vipindi vyao vyote mchezo wa ubashiri huwepo.

Hii ina maana kwamba kuna watu muda wote (saa 24) wanafanya tu kazi ya kubashiri kupitia vyombo vya habari ambavyo pengine vingetumia muda na vipindi vyao kuelimisha na kuandaa jamii kujishughulisha katika shughuli za uzalishaji na si ubashiri/kamari.

Kadri siku zinavyokwenda michezo hii imeimarishwa kweli kweli ambapo sasa washiriki huzawadiwa kiasi fulani cha pesa (mfano chombo kimoja kuna wakati washiriki 10 hupewa Tsh. 50,000/- kila mmoja kama mtaji wa kuendelea kubashiri).

Kwa hiyo vyombo hivi sasa vinawafanya watu wabaki muda wote wakibashiri tu kwa kuwapatia mitaji ya kubashiri. Sasa tunaandaa jamii/taifa la aina gani?

Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusu hiki kinachoendelea kwenye taifa letu.

Mosi, ninajiuliza hii michezo ya ubashiri ni nani anayemiliki au kayaanzisha? Serikali au watu binafsi?

Pili, pesa inayotumika kuendesha michezo hiyo au kutolewa kwa washiriki inatoka wapi?

Tatu, je huu au hiki kinachoendelea kama michezo ya ubashiri kupitia vyombo vya habari si utakatishaji wa fedha?

Nne, ni nani anayehusika kusimamia michezo hii na uendeshaji wake? Leo hii redio stations nyingi zinaendesha michezo hiyo muda wote, je hii ni sahihi kweli?

Tano, je taifa linafaidika vipi na hii michezo?

Sita, kwa nini vyombo vya habari karibu vyote vinaendesha michezo hii? Wanapata faida kubwa sana au kuna nini kwao?

Saba, walioanzisha, wanaosimamia na wanaoendesha michezo hii wanajua athari (negative) zake kwa washiriki na taifa kwa ujumla?

Maswali ni mengi sana....

Mwisho, sijui kama waziri wa habari na michezo alizungumzia hili kwenye uwasilishaji wa bajeti ya wizara yake (sikufuatilia).

Pengine serikali au wizara husika ituambie au itoe mchanganuo wa faida unaotokana na utitiri wa michezo hiyo wa ubashiri inayoendeshwa kupitia vyombo vya habari nchi nzima.

Kwa maoni yangu nafikiri hiki kinachoendelea hakina afya kwa taifa letu. Miaka mitano au kumi ijayo tutakuwa na watu au taifa la aina gani kama vyombo vya habari vyenye nguvu na jukumu la kuelimisha jamii vitaendelea kuhimiza na kuendesha michezo ya ubashiri? Nafikiri tuliangalie hili kwa jicho la kipekee.
 
Ni hatari, we acha tu hili taifa kila mwenye nguvu anafanya kulingana na power yake
 
Kodi Ya Betting Nayo Eti Ni Tegemeo Kwa Serikali
 
Sisikilizi redio siku hizi kabisa yaan sisikii ladha ya redio siku hizi nilishazoea vipindi vya zamani vipindi vingi vya zamani havipo kwa hio watangazaji siwaelewi nimejaribu asubuhi nimeshindwa nikazima labda

Wapo Redio hakuna hio mitangazo na ile redio ya Wasabato Hope redio Upendo fm sijui huwezi kuta mitangazo ya kamari redio ya kiislamu redio Imani hukuti mitangazo ya kamari redio ya wakatoriki redio Maria redio Tumaini hukuti matangazo ya kamari, sasa huko kwenye kamari unafuata nini? Si tune hizo redio ambazo hazina kamari usikilize
 
Kumekuwa na michezo mingi sana ya ubashiri kwenye vyombo vingi vya habari hasa redio na television.

Michifa letu. Miaka mitano au kumi ijayo tutakuwa na watu au taifa la aina gani kama vyombo vya habari vyenye nguvu na jukumu la kuelimisha jamii vitaendelea kuhimiza na kuendesha michezo ya ubashiri? Nafikiri tuliangalie hili kwa jicho la kipekee.
SITAKI UPUZI HII NCHI LAZIMA NIDHAMU IWEPO LA SIVYO TUTAENDELEA KUDIDIMIA. DISCIPLINE NA KAZI LAZIMA IWEPO NINAANZA HUMU HU JAMII FORUM. SITAKI NA SIPENDI UPUZI.

GACHAGUA LAZIMA AWE RAIS WA

Kumekuwa na michezo mingi sana ya ubashiri kwenye vyombo vingi vya habari hasa redio na television.
ina afya kwa taifa letu. Miaka mitano au kumi ijayo tutakuwa na watu au taifa la aina gani kama vyombo vya habari vyenye nguvu na jukumu la kuelimisha jamii vitaendelea kuhimiza na kuendesha michezo ya ubashiri? Nafikiri tuliangalie hili kwa jicho la kipekee.
SITAKI UPUZI HII NCHI LAZIMA NIDHAMU IWEPO LA SIVYO TUTAENDELEA KUDIDIMIA KAMA TAIFA. DISCIPLINE NA KAZI LAZIMA IWEPO NINAANZA HUMU HUMzU JAMII FORUM. SITAKI NA SIPENDI UPUZI.

FREE TUNDU LISSU NOW

GACHAGUA LAZIMA AWE RAIS WA KENYA.

adriz de mbusii
 
Sisikilizi redio siku hizi kabisa yaan sisikii ladha ya redio siku hizi nilishazoea vipindi vya zamani vipindi vingi vya zamani havipo kwa hio watangazaji siwaelewi nimejaribu asubuhi nimeshindwa nikazima labda

Wapo Redio hakuna hio mitangazo na ile redio ya Wasabato Hope redio Upendo fm sijui huwezi kuta mitangazo ya kamari redio ya kiislamu redio Imani hukuti mitangazo ya kamari redio ya wakatoriki redio Maria redio Tumaini hukuti matangazo ya kamari, sasa huko kwenye kamari unafuata nini? Si tune hizo redio ambazo hazina kamari usikilize

Ni sahihi kabisa kwamba baadhi ya radio stations hasa zinazomilikiwa na taasisi za dini hii michezo haipo, binafsi sijasikia ikiendeshwa kupitia vyombo vyao.

Mkuu hili ni tatizo kubwa ambalo suluhisho siyo kuchagua redio za dini bali kulishughulikia kwa kukomesha kabisa.

Binafsi sishiriki michezo hiyo lakini watu wengi sana (mijini na vijijini) wanashiriki, sasa tuwasidieje? Tuwaambie wasikilize redio za dini ambazo nyingi unakuta zinasikika tu maeneo machache? Kuna radio stations ambazo zinasikika nchi nzima na ndio vinara wa kuendesha hiyo michezo.

Je kuacha kusikiliza vyombo hivyo ni suluhisho sahihi la hili tatizo?

Jamii inahitaji msaada ambayo nafikiri ni kukomesha kabisa hiyo michezo.
 
Waache tu mkuu, Matangazo yamepungua sana redioni na TV show, betting company ndo inawaokoa.
 
Bila hayo matangazo ya betting na waganga wa kienyeji redio nyingi zinakufa
 
redion hazina mapato kutokana na kuwa na mrengo wa kichawa kila mara kusifia sirikali hivyo zinakosa mapato ya advertisment
 
Back
Top Bottom