Kuelekea maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani,wafanyakazi nchini wako kwenye mjadala wa kikokotoo,bima ya afya,nyongeza ya mishahara,kupanda n.k. huku wakikosa umoja na mtetezi atakayesimama kuwasemea ili kufika pale wanapotaka.
Kwa miaka kama tisa au kumi tangu utawala wa Rais Kikwete,wafanyakazi nchini hawajawahi kuongezewa mishahara licha gharama za maisha kuongezeka mara tano zaid ya kipindi cha JK,hakuna anyewasikiliza, hii inatokana na kukosa umoja kutokana na utitiri wa vyama vya wafanyakazi vinavyofikia 33+ ambavyo badala ya kuwatetea,viko kwa ajili ya kuwanyonya wafanyakazi.
Wakati mjadala wa nyongeza ya mishahara ukiendelea likaibuka suala ya bima ya afya kukataliwa kwenye baadhi ya hospital, binafsi sikuona chama cha wafanyakazi kilichosimama kukemea hilo.
Kabla hakujapoa kwenye bima likaibuka Kikokotoo,huu mjadala no moto hauna mwisho lakini ungemalizwa na vyama vya wafanyakazi kama wangekuwa imara ,hatujaona malumbano kati ya Tucta wakiibana serikali kufuta sheria ya kikokotoo ambayo haina maslahi kwa mstaafu.
Wafanyakazi nchini wanapitia kipindi kigumu kutokana kukosekana kwa mtetesi, mtetesi wao wamegawanyika kutokana na utitiri wa vyama huku wengi wa viongoz na makada wa chama tawala na wako kwa ajili ya kuwanyonya wanachama kupitia michango na sio kutetea maslahi ya wanachama.
Yawezekana serikali ikaweka mapandikizi kwenye vyama hivi vya wafanyakazi na ndio maana unaweza ukaona serikali ikiyafumbia madudu yanayofanywa na CWT ambayo yamepelekea uundwaji wa Chama kipya cha walimu,siku hizi kuna vyama vya manesi,najiuliza iko wapi nguvu ya vyama ya vya wafanyakazi?
Nitawashangaa sana kama wataimba ule wimbo wa SOLIDARITY siku ya Mei Mosi.