Utoaji wa mimba ni uuaji na dhambi

Utoaji wa mimba ni uuaji na dhambi

P J O

Senior Member
Joined
May 3, 2024
Posts
189
Reaction score
264
Kisayansi Yai na sperm ni cell inayoishi hivyo huitwa LIVING things.

Wale wanaodai kua mtoto ambae hajazaliwa si binadamu ni wauaji kama wauaji wengine. Samahani Kwa kuwaumiza Moyo, lakini Mimba ni mbegu hai mbili zilizokutana na kuumba kiumbe kamilifu yani binadamu. Utoaji wa Mimba ni uuaji wa kiumbe hai.

wanasayansi walifanya uchunguzi kupima maumivu watoto hupitia wanaotolewa Mimba na inaonyesha wazi watoto wale Wana feel extreme pain hata wakiwa tumboni.

MWISHO nanukuu neno la kwenye Biblia

Zaburi 139:16 BHN
[16] Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga, hata kabla ya kuweko ile ya kwanza.

Kama Mungu alitujua tukiwa Bado tumboni na kupanga siku zetu zote za maisha yetu, Kwa Nini basi binadamu mwingine aje atoe uhai wa kiumbe hiki Cha Mungu.

Usitoe MIMBA
 
Biblia haina chochote cha kunifundisha kuhusu hilo swala, rejea hadithi ya Mungu alipo agiza wana waisraeli waue vitoto vichanga na mifugo kwa maadui wa Israel!!!

Pia rejea wazaliwa wa kwanza katika hadithi ya farao na musa walipo uwawa kwa agizo la Mungu

Hizo hadithi zinajichanganya zenyewe kuhusu hilo swala.
 
Usome kwa kutulia habari yote.Ukikwama sehemu,omba kueleweshwa na wajuvi zaidi.
 
Unapewa agizo,unatakiwa ulitimize bila kuhoji.Kuhoji au kusita kufanya kwa ukamilifu maagizo ni utovu wa heshima,imani na upotofu wa adabu.Kila amri ilikua na malengo yake.
Hiki ndio kichaka na utapeli wa dini , waandishi waligundua kabisa watu wakitumia akili watashtuka , ndio maana wakaweka hilo angalizo.
 
Hiki ndio kichaka na utapeli wa dini , waandishi waligundua kabisa watu wakitumia akili watashtuka , ndio maana wakaweka hilo angalizo.
Na ndiyo maana,hakuna dini inayolazimisha awaye yote kuingia imani kwa lazima.Ukiona ni njema unachoma ndani.Ukiona ni miyeyusho unasepa kispoti.Rahisi tu na si kuanzisha malumbano.
 
Back
Top Bottom