Utoaji wa mimba ni uuaji na dhambi

Utoaji wa mimba ni uuaji na dhambi

Dini zote za kigeni walitumia mabavu kuzilazimisha Watu wazifuate Mpaka kufikia Hapa tulipo Dini ndîo imeua Watu wengi Kuliko kitu chochote baàda ya vita.

Dini ilikuwa siasa Zamani.
Kwa Sasa haulazimishwi Kwa sababu tayari mfumo ulioko umeshafiti matakwa ya Dini
Naam.Na itoshe kutofautisha nyakati hadi nyakati.
 
Hakuna cha kuelewa , biblia ni kitabu chenye mikanganyiko , ambacho kinatetewa kwa vitisho vya jehanam na ahadi ya mbinguni .
Kama waiona biblia hivyo na haukujiumba wewe mwenyewe sawa, lakini kama uliumbwa na haujui nani analiinua jua Kila siku, alituweka ubongo kichwani mwako, alinipa bahari mipaka na kufanya binadamu apumue hewa na samaki apate oxygen Majini basi usiidharau biblia. Jipe nafasi usome uelewe na ukue.

Usiwe mjinga siku zote. Ubarikiwe
 
Kama ndio hivyo hiyo nguzo ya upendo mnayosisitiziwa mtaitekeleza vipi katikati ya chuki na utengano wa kiimani?
Hakuna atengenezaye chuki na utengano isipokua wapokeaji wa ujumbe wa imani kushindwa kutetea hoja zao kwa ushawishi na upendo.Ndipo hapo sasa wanaposhindwa kushawishi wa upande mwingine,wanaishia kuanzisha mizozo na/au mapambano.
 
Kama waiona biblia hivyo na haukujiumba wewe mwenyewe sawa, lakini kama uliumbwa na haujui nani analiinua jua Kila siku, alituweka ubongo kichwani mwako, alinipa bahari mipaka na kufanya binadamu apumue hewa na samaki apate oxygen Majini basi usiidharau biblia. Jipe nafasi usome uelewe na ukue.

Usiwe mjinga siku zote. Ubarikiwe
Bado unahubiri tu , kwa nini ninapaswa kujiuliza nani kaniumba ila sipaswi kuuliza nani kamuumba huyo Mungu?
 
Dini zote za kigeni walitumia mabavu kuzilazimisha Watu wazifuate Mpaka kufikia Hapa tulipo Dini ndîo imeua Watu wengi Kuliko kitu chochote baàda ya vita.

Dini ilikuwa siasa Zamani.
Kwa Sasa haulazimishwi Kwa sababu tayari mfumo ulioko umeshafiti matakwa ya Dini
Lakini kumfata Yesu alituletea habari njema nayo ni Upendo. Sheria kuu kuliko yote ni Upendo. Vita ni kutokana na ukaidi wa Mwanadamu na kumkataa Mungu ndio maangamizi hufanyika. Hata wewe, ukiwa ndani ya Yesu Kila njia Yako itafanyika Kwa mapenzi yake, sio ajali
 
Naam.Na itoshe kutofautisha nyakati hadi nyakati.

Hoja ya min -me ni double standards zilizopo kwèñye hicho KITABU cha Biblia.

Niliwahi andika àndiko Hapa kuhusu uandishi wa Biblia na waandishi wake walivyowamba Ngoma kuvutia Kwao, kuanzia Musa.

Akiua Suleiman siô dhambi, Akiua Daudi siô dhambi, Akiua Musa siô dhambi, Kwa sababu wôte hao ndîo waandishi wamejipa uhalali na Haki ya kuua
 
Thibitisha huyo mungu kama yupo kweli .
Sawa nitathinitisha, wewe ulipo hapo unaamini una akili kichwani mwako wakayi ubongo wako hauoni? Unaamini kuna hewa kweli wakati Kwa macho Yako hauoni hewa?
 
Unatoa risala badala ya kudhibitisha kweli Mungu yupo!!
Bado unahubiri tu , kwa nini ninapaswa kujiuliza nani kaniumba ila sipaswi kuuliza nani kamuumba huyo Mungu?
Hapo ni kutojipa jukumu la kujichosha ili uupate ukweli uutakao.Kwa nini kila siku uwe wa kuhitaji wengine tu wakupe majawabu?Na cha kufurahisha,unatoa maswali ya kuongoza unapotaka jibu litokee.Hakuna majibu mepesi kwa maswali yenye mchanganyiko wa mitazamo.
 
Kisayansi Yai na sperm ni cell inayoishi hivyo huitwa LIVING things.

Wale wanaodai kua mtoto ambae hajazaliwa si binadamu ni wauaji kama wauaji wengine. Samahani Kwa kuwaumiza Moyo, lakini Mimba ni mbegu hai mbili zilizokutana na kuumba kiumbe kamilifu yani binadamu. Utoaji wa Mimba ni uuaji wa kiumbe hai.

wanasayansi walifanya uchunguzi kupima maumivu watoto hupitia wanaotolewa Mimba na inaonyesha wazi watoto wale Wana feel extreme pain hata wakiwa tumboni.

MWISHO nanukuu neno la kwenye Biblia

Zaburi 139:16 BHN
[16] Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga, hata kabla ya kuweko ile ya kwanza.

Kama Mungu alitujua tukiwa Bado tumboni na kupanga siku zetu zote za maisha yetu, Kwa Nini basi binadamu mwingine aje atoe uhai wa kiumbe hiki Cha Mungu.

Usitoe MIMBA
Anzia kwenye punyeto kwanza Ni dhambi au sio dhambi?

Halafu ndo tuje kwenye utoaji mimba. Father mbona unayumba sana
 
Hoja ya min -me ni double standards zilizopo kwèñye hicho KITABU cha Biblia.

Niliwahi andika àndiko Hapa kuhusu uandishi wa Biblia na waandishi wake walivyowamba Ngoma kuvutia Kwao, kuanzia Musa.

Akiua Suleiman siô dhambi, Akiua Daudi siô dhambi, Akiua Musa siô dhambi, Kwa sababu wôte hao ndîo waandishi wamejipa uhalali na Haki ya kuua
Hao wote ni wauaji tu pamoja na Mungu anaejinadi ni waupendo , kuua ni kuua tu , bado naona sipaswi kujifunza kutoka kwao ,utashi wangu unatosha bila wao.
 
Hapo ni kutojipa jukumu la kujichosha ili uupate ukweli uutakao.Kwa nini kila siku uwe wa kuhitaji wengine tu wakupe majawabu?Na cha kufurahisha,unatoa maswali ya kuongoza unapotaka jibu litokee.Hakuna majibu mepesi kwa maswali yenye mchanganyiko wa mitazamo.
Kwamba tutafute majibu? Min me katafuta majibu kapata conclusion Mungu hayupo

Mimi huwa sijichoshi kufikiria hayo naamini Mungu yupo kwa sababu kuu 2
1. Kama kuna ulimwengu wa giza basi Ulimwengu wa mwanga nao upo

2. Huwa naomba kwa jina la Mungu na ninapata majibu.
 
Lakini kumfata Yesu alituletea habari njema nayo ni Upendo. Sheria kuu kuliko yote ni Upendo. Vita ni kutokana na ukaidi wa Mwanadamu na kumkataa Mungu ndio maangamizi hufanyika. Hata wewe, ukiwa ndani ya Yesu Kila njia Yako itafanyika Kwa mapenzi yake, sio ajali

Habari Njema iliyoletwa Kwa Upanga na umwagaji damu?

Uliwahi kuona hiyo habari Njema popote pale?
Yàani Mtu akuletee habari Njema alafu ameshika Upanga ukikataa unauawa?

Kwani mataifa mengine yakifanya uhalifu mtauita uhalifu lakini Wayahudi wakifanya uhalifu mnaupa uhalali?
 
Hao wote ni wauaji tu pamoja na Mungu anaejinadi ni waupendo , kuua ni kuua tu , bado naona sipaswi kujifunza kutoka kwao ,utashi wangu unatosha bila wao.

Mungu Muumbaji hawezi kuwa MUUAJI ila Ipo mîungu yenye Sifa za kibinadamu àmbayo ndiyo hiyo inayotaka kuabudiwa na usipoiabudu inakupa adhabu au inaagiza WAFUASI wake wakupe adhabu.
 
Hoja ya min -me ni double standards zilizopo kwèñye hicho KITABU cha Biblia.

Niliwahi andika àndiko Hapa kuhusu uandishi wa Biblia na waandishi wake walivyowamba Ngoma kuvutia Kwao, kuanzia Musa.

Akiua Suleiman siô dhambi, Akiua Daudi siô dhambi, Akiua Musa siô dhambi, Kwa sababu wôte hao ndîo waandishi wamejipa uhalali na Haki ya kuua
Kila jambo lilitegemea lifanyike au kutokea(na kutofanyika au kutotokea) kwa lengo lipi!Na ndiyo maana,kuna simulizi za baadhi tu ya watu,jamii au nchi fulani kama kuwakilisha na si simulizi ya kila mtu,kila kiumbe,kila jamii au nchi zote.
 
Back
Top Bottom